read

Aya 174-176: Wafichao Aliyoyatermsha Mwenyezi Mungu.

Maana

Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo.

Inasemekana kuwa Aya hii imewashukia wale walioficha sifa za Muhammad (s.a.w.w) na Utume wake. Kwa vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya, makusudio yatakuwa ni kwa kila mwenye kujua kitu chochote katika haki akakificha kwa kuleta tafsiri nyingine au kubadilisha kwa manufaa yake binafsi; awe ni Myahudi, Mkristo au Mwislamu. Kwa sababu tamko ni lenye kuenea na linalozingatiwa ni kuenea tamko si kuhusika sababu za kushuka kwake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtisha mpotevu huyu katika Aya nyingi; miongoni mwazo ni zile zilizotangulia (Aya ya 146 na 159) na zitakazofuatia katika Sura Al-Imran, Nisa, Maida na Aya hii tuliyonayo. Zote hizo ni hasira za Mwenyezi Mungu na kiaga kikali cha adhabu na mateso. Kwa sababu ni wajibu haki itukuzwe na kutangazwa kwa kila njia na kuondoa mikanganyo yote ya kutofahamika. Vile vile kumpiga vita mwenye kuipinga kwa nguvu zote na kujitoa mhanga kwayo. Kwani hakuna msimamo wa dini, wala nidhamu au uhai isipokuwa kwa haki.

Hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto.

Yaani adhabu wanayostahili katika moto. Hiyo ni katika kuelezea kinachosababishwa ambacho ni moto na kinachosababisha ambacho ni kula haramu. Ametaja matu-mbo, ingawaje inajulikana kuwa kula hakufanywi isipokuwa kwa ajili ya tumbo, ili kuonyesha kuwa linalowashughulisha wao ni kujaza matumbo yao tu.

Wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya Kiyama.

Ni fumbo la kuachana nao na kuwakasirikia wala hatawatakasa na madhambi kwa kuwasamehe.

Hao ndio walionunua upotevu kwa uongofu.

Upotevu ni kufuata matamanio na uongfu ni kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu. Kubadilisha upotevu kwa uongofu ni kuathirika na batili kuliko haki.
Basi ni ujasiri ulioje wa kuvumilia moto?

Huku sio kuelezea ujasiri wao kwa moto wala sio kustaajabu kunakotokana na kutojua sababu ya jambo, hilo haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kwani anajua kila kitu. Isipokuwa makusudio hapa ni kuonyesha namna ya kujitia ujasiri kwao kwa kuacha hukumu zake na mipaka yake, na kufuata upotevu na batili.

Kwa hiyo makusudio ni kuleta picha ya hali yao hiyo na kufananisha marejeo yao ambayo haiwezekani kuyafanyia ujasiri kwa vyovyote. Razi anasema: “Walipojiingiza kwenye lile linalowajibisha moto, wamekuwa kama wenye kuridhia adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwa majasiri wa adhabu hiyo; sawa na kumwambia yule anayejiingiza kwenye lile linalo kasirisha serikali: Ni ujasiri ulioje wako kufungwa jela?

Unaweza kuuliza: Tumejua hiyo ndiyo hali ya yule mwenye kuijua haki na akaificha; sasa ni ipi hali ya asiyejua chochote katika yalivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, lakini pamoja na hayo anasema: Hii ni haramu na hiyo ni halali, na wala hana chochote cha kutegemea isipokuwa dhana na kuwazia tu?

Jibu: Huyu ana hali mbaya zaidi kuliko yule anayeijua haki na akaificha. Kwa sababu yeye amejiweka daraja ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kujifanya ndio msingi wa sharia, wa kuhalalisha na kuharamisha.

Mvutano Kati Ya Haki Na Batili

Mwenye tafsir ya Al-Manar amemnakili Sheikh Muhammad Abduh kwamba amesema katika kuifasiri Aya hii:

“Katika Waislamu kuna wanaoficha yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa kugeuza na kuleta taawili, sawa na wanavyofanya Mayahudi kuficha sifa za Mtume. Waislamu hawa wanatambua mivutano miwili inayopingana mvutano wa haki waliyoijua na mvutano wa batili waliyoizoweya. Hayo yanawatingisha na kuwaathiri, na haya yanawapa kiburi na chuki.

Akili zao zimeshinda yale waliyoyajua na nyoyo zao zimeshinda yale waliyoyazowea, wakathibiti kwenye yale waliyoyazua; wakawa katika vita kati ya akili na dhamiri.

Wakifikiria kesho (akhera), starehe za sasa (duniani) zinawatokea puani, lakini wanapoonja utamu wa wanayofanya wanasahau yatakayokuja. Je, huku kuhisi kuitweza haki na kuinusuru batili sio moto unaowaka mbavuni mwao? Je thamani ya haki wanayoila si miti ya miba ambayo hainenepeshi wala kuondoa njaa?”

Hayo ni sahihi kwa upande wa baadhi ya wale wanaojitilia shaka katika dhamiri zao na kujilaumu, wakiwa wanafanya dhambi. Lakini wengine wamezoweya batili mpaka ikawa ni tabia yao, na kuliona adui kila lenye harufu ya haki na utu.

Wakati ninapoandika maneno haya ni mwezi June 1967. Katika mwezi huu ulio na shari, Israil imevamia baadhi ya sehemu za miji ya Waarabu kwa msaada wa Uingereza na Marekani, na wamewatoa watu majumbani mwao, wakawafukuza zaidi ya watu laki mbili na nusu (250,000), wakawachoma wake kwa waume na watoto kwa mabomu ya Napalm.

Wengi wameunga mkono fedheha hii na kufurahishwa nayo; wanatamani lau Israil ingeendelea na uovu wake. Mapenzi ya nafsi yamezidi akili na dhamiri zao mpaka zikaisha zote bila ya kubaki athari yoyote, wakawa sawa na wanyama. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaita kuwa ni watu wasio na akili; wasiofahamu na kwamba wao ni wanyama, bali ni wapotevu zaidi kuliko wanyama.

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki.

Hayo ni ishara ya adhabu itakayowashukia wale wanaoficha haki. Na, kauli yake Mwenyezi Mungu: “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu”, ni kubainishwa sababu za adhabu ambazo ni kuthubutu kwao kuwa wajasiri wa kuihalifu haki iliyokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Na wale waliohitalifiana katika kitabu wamo katika upinzani ulio mbali.

Wafasiri wamehitalifiana katika makusudio ya kauli hii. Wafasiri wengi, aki- wemo mwenye Majmaul Bayan wamesema ni makafiri; na namna ya kuhitalifiana kwao hao makafiri ni kwamba kuna katika wao waliosema kuwa Qur’an ni uchawi, wengine wakasema ni utenzi na wengine wakasema ni vigano vya watu wa kale.

Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya waliohitalifiana ni Waislamu, kwamba wao baada ya kuafikiana kuwa Qur’an inatoka kwa Mwenyezi Mungu, wamehitilafiana katika kuifasiri na kuleta taawili; wakagawanyika kwenye vikundi. Ilitakiwa wao wawe na tamko moja kwa vile Qur’an ni moja.

Inawezekana kuwa makusudio ni makafiri, lakini sio kwa kuwa wengine walisema kuwa Qur’an ni uchawi, utenzi au vigano, bali ni kwamba wao ndio sababu pekee ya kuhitilifiana, kupigana na kuacha kuafikiana na tamko la haki kati yao na wale walioamini Qur’an.

لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ {177}


Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu, lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na malaika na Kitabu na manabii; na akawapa mali, akiwa aipenda ,jamaa na mayatima na masikini na mwananjia na waombao,nakatikaukombozi wa watumwa; na akasi- mamisha swala na akatoa zaka; na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wanaokuwa na subira katika shida na dhara na katika


wakat


i


w


a


vita


.


Ha


o


ndio


waliosadikishanandiowenye takuwa.