read

Aya 177: Anatoa Mali Akiwa Aipenda

Lugha

Kila amali ya heri ni wema. Mwananjia ni msafiri asiyesafiri kwa maasia, akaishiwa na mali asiweze kurudi kwake. Madhara ni kila linalomdhuru mtu, iwe ni maradhi au kumkosa mpenzi, n.k.

Maana

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameyataja mambo aliyoyazingatia kuwa ni nguzo ya wema, uchaji Mungu na imani ya kweli. Mambo hayo kuna yanayofungamana na itikadi, yanayofungamana na kutoa mali, yanayofungamana na ibada na yale yanayofungamana na akhlaq. Kabla ya kufafanua ameanza kwa kusema:

Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu.

Maneno haya waanaambiwa watu wote, hata kama sababu ya kushuka ni mahsusi. Kwa sababu, la kuzingatia ni hayo maneno kwa ujumla sio sababu za kushuka kwa Aya.

Makusudio ni kuwaambia waumini na wanaoswali, kwamba kuswali tu upande maalum, sio heri ya dini iliyokusudiwa. Kwa sababu swala imewekwa kwa ajili ya kuwa mwenye kuswali amwelekee Mwenyezi Mungu peke yake na kuachana na wengine.

Baada ya utangulizi huu, ameingilia kubainisha misingi ya itikadi ambayo ndiyo nguzo ya wema, na ameikusanya katika mambo matano ambayo yamekusanywa na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na Malaika na kitabu na Manabii.
Kumwamini Mwenyezi Mungu ndio msingi wa amali njema inayo sababisha kumtii Mwenyezi Mungu katika yote aliyoyaamrisha na kuyakataza. Kuamini Malaika ni kuamini wahyi ulioteremshwa kwa Mitume; na kuwakana Malaika ni kuukana wahyi; Mwenyezi Mungu anasema:

نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ {193}

عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنْذِرِينَ {194}


“Ameiteremsha Roho mwaminifu juu ya moyo wako, ili uwe miongoni mwawaonyaji.”(26:193-194).

Kuamni Kitabu ni kuamini Qur’an na Manabii na kuamini sharia zao. Mambo yote haya matano yanarejea kwenye mambo matatu; Kuamini Mwenyezi Mungu, Utume na siku ya mwisho.Kwa sababu kuamini Utume kunachanganya kuamini Malaika na kitabu.. Baada ya hayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaashiria taklifa za kimali kwa kauli yake:

Na akawapa mali akiwa aipenda

Imesemekana kuwa dhamiri katika kupenda inamrudia Mwenyezi Mungu, kwa vile limetangulia jina lake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika kauli yake: “Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu” Na imesemekana kuwa dhamiri inarudia mali na inakuwa kama kauli yake Mwenyezi Mungu:

لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ {92}


“Hamtapatawemampakamtoekatikavilemnavyovipenda...”(3:92).

Vile vile kauli yake:

وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا {8}


“Na huwalisha chakula masikini na mayatima na mateka na hali ya kuwawenyewewanakipenda.” (76:8).

Kauli hii ndiyo iliyo dhahiri zaidi, kwa sababu dhamiri inamrudia wa karibu zaidi, sio wa mbali. Kisha makusudio ya kutoa mali hapa sio zaka ya wajibu, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameunganisha na kutoa zaka na kuunganisha kunahukumilia kubadilika.

Aya imetaja aina sita za wale ambao inatakikana kuwapa:

1. Jamaa - Nao ni jamaa wa mwenye mali, kwa sababu wao ndio wenye haki zaidi ya kuwatendea wema. Mwenyezi Mungu anasema: “Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutoawapa akraba” (24:22). Ni wajibu kumlisha jamaa aliye karibu, ikiwa ni mzazi na mtoto, ikiwa wanashindwa kujilisha. Ama wasiokuwa hao inakuwa kuwapa ni Sunna sio wajibu, kama wanavyosema Mafaqihi.1

2. Mayatima - ambao hawana mali wala mlezi wa kuwatunza. Kwa hiyo itakuwa ni wajibu kwa wenye uwezo kuwalea, ikiwa hakuna hazina ya Waislamu (Baitul-maal).

3. Maskini - wale wenye haja ambao hawawanyooshei watu mkono wa udhalili (hawaombi).

4. Mwananjia - Yule ambaye ameishiwa safarini asiyeweza kurudi kwao bila ya msaada.

5. Wenye kuomba wale ambao wanawanyooshea watu mikono ya udhalili. Jambo hilo limeharamishwa kisheria isipokuwa kwa dharura ya hali ya juu; sawa na dharura ya kula mfu. Dalili tosha ya uharamu wake ni kwamba ni udhalili na utwevu, na udhalili huo wenyewe ni haramu uwe umetokana na mtu mwengine au na yeye mwenyewe. Kuna Hadith inayosema: “Si halali kupewa sadaka tajiri na mwenye nguvu aliye mzima wa mwili.”

6. Watumwa- Yaani kununua watumwa na kuwaacha huru kwa kuwakomboa utumwani. Lakini maudhui haya hayapo siku hizi kutokana na kutokuwepo utumwa.

Kwa ujumla aina hizi sita alizozitaja Mwenyezi Mungu ni kwa njia ya mfano, sio kwamba hizo ndio zote. Yako mambo mengi ambayo ni vizuri kuyatolea mali; kama kujenga shule, vituo vya mayatima, mahospitali, kuilinda dini na nchi na mengineyo yanayohusu Umma kwa ujumla.

Ikiwa heshima ya mtu itavunjika isipokuwa kwa kutoa mali, basi ni wajibu kuitoa kwa mwenye kuweza; na lolote ambalo wajibu fulani hauwezi kutekelezeka isipokuwa kwa kufanya jambo hilo, basi ni wajibu kulifanya.

Mwenyezi Mungu ameashiria nguzo ya kutenda wema ya kiibada kwa kauli yake:

Na akasimamisha Swala na akatoa Zaka.

Swala ni ya kutakasa nafsi, Saumu ni ya kutakasa mwili na zaka ni ya kutakasa mali.

Ameashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye nguzo ya maadili kwa kusema:

Na watekelezao ahadi zao wanapoahidi.

Ahadi inayopaswa kutekelezwa iko namna mbili. Ya kwanza, ni ile inayokuwa kati ya mja na Mola wake; mfano Yamini Nadhiri na ahadi kwa sharti zilizotajwa katika vitabu vya Fiqh. Hayo tumeyafafanua katika Juzuu ya tano ya Kitabu Fiqhul-Imam Jaffar Sadiq (A.S).

Ya pili, ni aina ya ahadi ya muamala unaopita kati ya watu. Ni wajibu kuitekeleza; kama vile bei, ajira, deni n.k.

Mumini mwema anatekeleza mambo yote yanayomlazimu; hata kama hakuna uthibitisho wa kulazimisha kutekeleza. Ama kutekeleza kiaga sio wajibu kisheria, bali ni Sunna Kifiqh

Miongoni mwa tabia nzuri zenye kusifiwa ni subira (uvumilivu) ambayo ni katika nguzo za wema, yenye kuonyeshwa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na kuwa na subira katika shida na dhara na wakati wa vita.

Shida ni ufukara, na dhara ni maradhi, n.k. Makusudio ya kuvumilia ufukara na maradhi sio kuyaridhia, kwani Uislamu umewajibisha kuhangaika na kufanya juhudi kwa kadri iwezekanavyo, ili kujitoa katika ukata, maradhi, ujinga, na kila linalorudisha nyuma maendeleo.

Makusudio yake hasa ni kutosalimu amri kabisa katika shida na kuwa na mshikamano na kufanya kazi kwa uthabiti na bidii ili kujikwamua na yaliyowapata. Baadhi ya wafasiri wanasema: “Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja uvumilivu katika mambo matatu: (ufukara, maradhi na vita), pamoja na kuwa uvumilivu unatakiwa katika hali zote, kwa sababu hali hizo tatu ni miongoni mwa balaa na mitihani mikubwa. Mwenye kuvumilia hayo, basi anaweza kuvumilia mengine.

Hao ndio waliosadikisha na ndio wamchao Mungu.
“Hao” ni ishara ya wale ambao wamekusanya mambo yote haya yaliyota- jwa - misingi ya itikadi, kutoa mali, kutekeleza ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na tabia nzuri. Hakika hao ni wakweli katika imani yao, wenye kuogopa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake. Ama wale wanaosema kwa vinywa vyao tu, kuwa tumeamini na wala wasitoe wanayoyapenda wala kutekeleza yanayowalazimu na kuvumilia katika shida. Wote hao wako mbali na wema.

Wema Katika Ufahamu Wa Kiqur’an

Aya hii imeonyesha mambo matano: Itikadi, taklifa za kimali, ibada, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida. Haya mambo mawili ya mwisho ni katika mambo ya kimaadili.

Kwa dhahiri ni kwamba ibada, kama swala na saumu ni athari ya imani na ni alama yake isiyoepukika nayo. Kwa sababu asiyeamini kuwapo Mungu, hawezi kumwabudu.

Ama kutoa mali, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida, hayo yanapatikana kwa anayemwamini Mwenyezi Mungu au kwa anayemkanusha. Kwani wengi wanaomwamini Mungu wanasema wasiyoyatenda, ni wabahili; hata kwenye nafsi zao na wanasalimu amri mbele ya shida.

Lakini mara nyingine mkanushaji Mungu huweza kujitolea mhanga katika kupigania uadilifu na utu, anakuwa imara katika shida na kutekeleza anayoyasema.

Kwa hivyo, kidhahiri, inaonyesha kuwa imani hailazimiani na tabia njema wala kufuru hailazimiani na tabia mbaya lakini ilivyo hasa hakuna imani bila takuwa (kumcha Mungu).

Lakini Aya hii (sio wema). Imezingatia imani kuwa pamoja na tabia njema bila ya kutengana, kwa maana yakuwa sio kumwamini Mungu pekee ndiko kutakakomfanya mtu kuwa mwema; wala tabia nzuri bila ya imani haiwezi kumfanya mtu awe mwema, bali hapana budi kumwamini Mwenyezi Mungu, kuwa na tabia njema na kumwabudu.

Kwa hivyo basi ‘mwema’ anavyoelezwa katika Qur’an ni Mumin mwenye kufanya ibada, mtekelezaji ahadi, mkarimu na mvumilivu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنْثَىٰ بِالْأُنْثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ {178}


Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kisasi katika waliouawa; muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke. Naanayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwa wema na kulipa kwa ihsani. Hiyo ni tahfifu itokayo kwa Molawenunar


ehema. Na atakeyerukamipakabaadaya hayo, basi ana yeye adhabu iumizayo.

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ {179}


Mnauhaikatikakisasi,enyi wenyeakili,ilimsalimike.

  • 1. Hanafi wanasema : Ni wajibu mtu kuwalisha jamaa zake wa karibu asioweza kuwaoa. Hanbal wamesema: Ni sharti mlishaji awe ni mrithi wa anayelishwa. Malik wanasema: Si wajibu kulisha isipokuwa baba, mama na watoto wa kuwazaa tu, sio ndugu wengine. Shia Imamiya na Shafii wanasema: Ni wajibu kuwalisha wazazi, mababu na kuendelea juu na watoto, wajukuu na kuendelea chini.