read

Aya 178-179: Kisasi Cha Waliouawa

Maana

Wanavyuoni wa sharia ya Kiislamu wamepanga namna tatu za adhabu:

1. Haddi; kama kukata mkono wa mwizi, kupigwa mawe hadi kufa kwa mzinifu aliye na mke, kupigwa viboko kwa mnywaji pombe, n.k. Utakuja ufafanuzi mahali pake Inshallah.

2. Diya (Fidia): Hiyo ni adhabu ya kimali.

3. Kisasi - kufanyiwa yule aliyefanya jinai kwa makusudi sawa na vile alivyomfanyia yule aliyemuua, au aliyemkata kiungo au aliyemjeruhi. Ama kupiga hakuna kisasi. Mafaqihi wameweka maelezo maalum kwa kila namna ya adhabu hizo tatu, na Aya hii inaingia katika kisasi.

Enyi mlioamini! mmeandikiwa kisasi katika waliouawa.

Wakati wa ujahiliya (kabla ya Uislamu) watu walikuwa hawana sheria yenye mpango; wanauana kidhulma na kiuadui, na kulipiza kisasi kwa watu wasiokuwa na hatia na wala sio kwa yule aliyekosa.

Mtu wa kawaida akiuawa, basi watu wake wataua idadi kubwa ya watu wa muuaji. Na, kama mwanamke akimuua mwanamke mwenzake, basi mahali pake patachukuliwa na watu wa ukoo wake au kabila yake; wanaweza kuua hata watu kumi kwa mmoja tu.

Dhuluma hii ilisababisha vita vya kikabila; watoto na wajukuu wakarithi uadui na chuki. Ndipo Mwenyezi Mungu akaweka sharia hii ya kisasi ambayo inafahamisha usawa na kisasi kiwe kwa yule aliyeua kwa hali yoyote awayo na wala sio watu wasiokuwa na makosa, na pia kusiweko na ziada au upungufu; kinyume na ilivyokuwa zama za ujahiliya.

Na kwa sharti ya kuwa kuua kuwe ni kwa kukusudia sio kwa kukosea au bilakukusudia.1

Katika maana Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ{45}


“...Nafsikwanafsi...” (5:45).

فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا {33}


“...Lakinihiyoasipitekiasikatikakuua...” (17:33).

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِثْلُهَا ۖ {40}


“Namalipoyaubayaniubayauliosawanahuo...” (42:40).

فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ {194}


“...Basianayewachokozamchokozenikwakadirialivyowachokoza...” (2:194).

Muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa mwanamke.

Maana yake yako wazi hayahitaji ufafanuzi. Hiyo ni ibara ya usawa kati- ka kisasi kati ya muuaji na aliyeuliwa katika uhuru, utumwa na jinsia.

Unaweza kuuliza kuwa: Ufahamisho wa mfumo wa tamko unaonyesha kuwa muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa. Na kama mwanamume akimuua mwanamke hauawi, Je wameafikiana Mafaqihi?

Jibu: Hakika Aya imeonyesha aina tatu tu ambazo ni muungwana kumuua muungwana, mtumwa kumuua mtuwa na mwanamke kumuua mwanamke, na haikueleza aina ya nne ambayo ni muungwana kumuua mtumwa au mtumwa kumuua muungwana na mwanamume kumuua mwanamke au mwanamke kumuua mwanamume.

Aya imefahamisha kwa matamko yake kwamba kisasi kimewekwa katika aina tatu za kwanza; na hayo wameafikiana Mafakihi, kwa sababu katika dhahiri ya Qur’an hakuna kuhitalifiana.
Vile vile Aya haikukanusha au kuthibitisha kisasi katika aina nyingine, si kwa kimatamko wala kiufa- hamu. Kwa hiyo hapana budi kurejea kwenye dalili nyingine ya Hadith au ijmai.

Mafaqihi wamehitalifiana katika hilo: Malik, Shafii na Hambal wanasema: Muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa.

Abu Hanifa anasema: Bali atauawa muungwana kwa kumuua mtumwa wa mtu mwingine, lakini hauawi kwa kumuua mtumwa wake. Wameafikiana wote wanne kwamba mwanamume atauawa kwa kumuua mwanamke na kinyume chake.

Shia Imamia wamesema: “Muungwana akimuua mtumwa hauawi, bali atapigwa kipigo kikubwa na kutoa fidia ya mtumwa. Na mwanamke akiua mwanamume, watu wa aliyeuawa wanayo hiyari ya kuchukua fidia, kama huyo muuaji akikubali au kumuua. Kama wakichagua kuua, hapo watu wake hawatatoa chochote.

Kama mwanamume ndiye aliyemuua mwanamke, basi watu wake wanayo hiyari ya kuchukua fidia kama muuaji akikubali au kumuua kwa masharti ya kuwapa warithi wa yule aliyeua nusu ya fidia ya mwanamume ambayo ni Dinar mia tano (500).

Na anayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwa wema; na kulipa kwa ihsani.

Neno “chochote” linafahamisha kwamba walii wa aliyeuawa, akisamehe chochote kinachofungamana na muuaji, kama kusamehe kumuua na kuridhia kuchukuwa fidia, basi inatakikana muuaji aukubali msamaha huu kwa wema. Imesemekana pia kuwa neno chochote linafahamisha kuwa, kama warithi wakiwa wengi na mmoja wao akamsamehe muuaji, basi hakuna kisasi, hata kama waliobakia watang’ang’ania kutaka kisasi.

Vyovyote iwavyo, hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kwa walii wa damu iliyomwagwa haki ya kisasi kutoka kwa aliyeua kwa makusudi. Haifai kumlazimisha muuaji atoe fidia ikiwa mwenyewe anataka kuuliwa, wala muuaji hawezi kumlazimisha walii wa aliyeuawa kuchukua fidia ikiwa mwenyewe anataka kulipiza kisasi cha kuua.

Inaruhusiwa kwa wote wawili kuafikiana kwa kufanyiana suluhu ya kiasi cha mali ya fidia, kiwe kichache au kingi, ili kiwe ni badala ya kisasi. Maafikiano hayo yakitimia basi itakuwa ni lazima kutekelezwa na wala haiwezekani kubadilisha.

Ni juu ya walii wa aliyeuawa kumtaka muuaji badala ya kisasi kwa wema, bila ya kumtilia mkazo wala kumdhikisha au kuomba zaidi ya haki yake. Na ni juu ya muuaji kutoa mali kwa wema, bila ya kuchelewesha, kupunguza au kufanya hadaa yoyote.

Hiyo ni tahfifu itakayo kwa Mola wenu.

Yaani hekima ya kuwekwa fidia badala ya kisasi ni tahfifu na rehema kwenu.

Na atakayeruka mipaka baada ya hayo, basi yeye ana adhabu iumizayo.

Walikuwa baadhi ya watu wakati wa ujahiliya, wanaposamehe na kuchukua fidia, kisha wanapompata muuaji baadaye humuua. Hapo Mwenyezi Mungu akakataza kupetuka mipaka huku na akamwahidi adhabu iumizayo mwenye kuyafanya hayo.
Baadhi ya wafasiri wanasema: Hakimu atamhukumu kuuliwa aliyemuua muuaji baada ya kupita msamaha; hata kama atatoa fidia na kuridhia walii wa aliyeuliwa. Lakini kauli hii ni ya kuonelea uzuri hivyo tu, na wala Aya haifahamishi hilo si kwa karibu wala mbali.

Mna uhai katika kisasi enyi wenye akili.

Hii ni sababu ya kuwekwa sharia ya kisasi na kubainisha hekima, na kwamba katika hukumu hiyo kuna kulinda kufanyiana uadui. Kwani mwenye kujua kwamba yeye atauliwa baada ya kuua, ataogopa.

Ama kutoa mali sio kuzuia kuua, kwani watu wengi wangeliweza kutoa mali kwa sababu ya kuwakomoa maadui zao.

Wafasiri wamerefusha maneno katika kubainisha ufasaha wa Aya hii na kuilinganisha na msemo unaosema; “Kuua ni kinga ya kuua.” Baadhi yao wametaja njia sita, Alusi ameongeza mpaka kufikia kumi na tatu na waliokuja baada ya Alusi nao wakaongeza zao. Njia zote hizo zinarudia kwenye utafiti wa matamshi tu.

كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِنْ تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ {180}


Mmeandikiwa


,


mmoj


awenu


anapofikwa na mauti kama


akiach


a


mali


,


kuwausi


a


kitu wazaz


i


wawil


i


n


a


akrab


a


kwa


namna nzuri inayokubalika. Ni haki haya kwa wenye


takua.

فَمَنْ بَدَّلَهُ بَعْدَمَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ {181}


Naatakayeubadilisha(wasia) baadayakuusikia,basidhambi yake ni juu ya wale watakaobadilisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia,Mjuzi.

فَمَنْ خَافَ مِنْ مُوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {182}


Mwenye kuhofiamwusiaji


kwend


a


komb


o


a


u


dhambi,


akasuluhish


a


bain


a


yao


,


basi hatakuw


a


n


a


dhambi


.Hakika Mwenyez


i


Mung


u


n


i


Mwenye


maghufir


a


Mweny


e


ku


r


ehe


mu.

  • 1. Kuua kwa makusudi ni kukusudia kitendo na kuua; kama mtu kumchoma kisu mwengine kwa kukusudia kumchoma na kumuua au kakusudia kitendo cha kuua tu, kama kukusudia kumchoma katika moyo wake lakini bila ya kukusida kuua. Hayo ni mauaji ya kukusudia. Ama kuua kwa makosa, ni kukosea katika kusudio lake na kitendo chake; kama mwenye kukusudia kumfuma mnyama akampata mtu, hapo mtu siye aliyekusudiwa kufumwa wala kuuliwa. Kuua bila ya kukusudia ni kukusudia kitendo, lakini sio kuua; kama anayempiga mtoto kumtia adabu, akafa; hapo tendo la kupiga limekusudiwa, lakini mauti hayakukusudiwa. Katika hali hizi mbili (Kuua kwa makosa na kuwa bila ya kukusu- dia) hakuna kisasi isipokuwa fidia tu.