read

Aya 180-182: Wasia Kwa Wazazi

Lugha

Neno “Khayri” lina maana ya kinyume cha shari, na makusudio ya neno Khayr hapa ni mali. Inasemekana kuwa kila linapokuja neno Khayr kati- ka Qur’an linakuwa makusudio yake ni mali; kama ilivyo katika Sura (11:84 ) (24:33), (100:8), , n.k.1

Maana

Mmeandikiwa, mmoja wenu anapofikiwa na mauti kama akiacha mali, kuwausia wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri inayokubalika.

Aya hii ni miongoni mwa Aya za hukumu, na inaingia katika mlango wa wasia. Kauli za mafaqihi na wafasiri zimekuwa nyingi na kugongana kuhusu Aya hii. Miongoni mwa kauli hizo ni kama zifuatazo:-

• Ikiwa mtu ana mali na akaona dalili za mauti, basi ni wajibu kwake kuusia kitu katika mali yake kwa wazazi wawili na ndugu wa karibu, hata kama wao ndio watakaoirithi; atawakusanyia urithi na wasia.

• Wasia ni wajibu kwa jamaa zake wakiwa sio warithi.

• Wasia kwa akraba ni sunna tu, na wala si wajibu.

• Kuwausia warithi haki yao na viwango vyao vya kurithi. Kwa hivyo Aya itakuwa inapita mapito ya Aya inayosema:

يُوصِيكُمُ اللَّهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنْثَيَيْنِ ۚ فَإِنْ كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ {11}


“MwenyeziMunguanawausiajuuyawatotowenu;fungulamwanamume nikamafungulawanawakewawili.”(4:


1


1).

• Wasia utakuwa ni wajibu kwa jamaa ikiwa mali ni nyingi.

• Aya ni Mansukh (haitumiki hukumu yake) kwa Aya ya urithi. Na mengineyo zaidi ambayo hayategemewi kabisa.

Kuwausia Warithi

Sunni na Shia wametofautiana katika kuswihi wasia kwa warithi. Wakaafikiana madhebu mane kuwa hauswihi, wakitegemea hadith isemayo: “Hakuna wasiya kwa warithi”.

Shia Imamia wameafikiana juu ya kuswihi wasia kwa warithi na wengineo, kwa kutothibiti Hadith hiyo kwao, na kwamba dalili ya kuswihi wasia inachanganywa kwa ujumla na wasia kwa warithi; kuongezea riwaya mahsusi kutoka kwa Ahlul Bait (a.s.). Dalili yenye nguvu ya kuswihi wasia kwa warithi ni Aya hii tuliyo nayo.

Allama Hilli katika kitabu At Tadhkira anasema: “Wasia kwa warithi unafaa kwa kauli za wanavyuoni wetu wote, ni sawa warithi wamekubali au la. Hilo ni kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye Aya hizi tulizo nazo.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amewajibisha kuwausia wazazi wawili, kwa sababu wao ndio akraba (jamaa wa karibu) zaidi wa maiti, kisha akasema kutilia mkazo wajibu huo: “Ni haki haya kwa wenye takua” yaani anamwambia yule ambaye hayaitakidi haya, kuwa si katika wamchao Mungu.

Tena akatilia mkazo kwa mara ya pili kwa kauli yake: “Na atakayeubadilisha baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha.”

Mwisho akaitilia mkazo jumla hii kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mjuzi”.

Unaweza kuuliza: Shia wamesema, inajuzu kuusia, na wala hawakusema ni lazima, pamoja na kuwa Aya mmeandikiwa kwa maana ya imesema mmewajibishiwa, kwa hivyo basi Shia wameihalifu Aya kama walivyoihalifu Sunni kwa kusema kuwa hauswihi wasia kwa warithi?

Jibu: Wameafikiana Waislamu wote kwamba kutoa hukumu ya sharia katika Qur’an, hakufai ila baada ya kuangalia Hadith za Mtume, na baada ya kufanya utafiti wa Ijmai vile vile. Kama hakuna Hadith wala Ijmai katika maudhui ya Aya, basi inajuzu kutegemea dhahiri ya Aya.

Imethibiti katika Hadith na Ijmai kwamba wasia kwa akraba sio wajibu, kwa hivyo hapana budi kuichukulia Aya kuwa ni Sunna katika wasia na wala sio wajibu, na yanakuwa maana ya “Ni haki kwa wamchao Mungu”, kwamba Sunna hii ni yenye kuthibiti kwa haki, kwa sababu maana ya haki ni kuthibiti. Makusudio ya “Namna nzuri inayokubalika”
Ni kuwa kitu chenye kuusiwa kinanasibiana na hali ya mwenye kuusia na mwenye kuusiwa; kisiwe kichache cha kudharaulika, wala kisiwe zaidi kuwadhuru warithi; yaaani kisizidi theluthi ya mali itakayoachwa na marehemu.
Kuna Hadith inayosema: “Hakika Mwenyezi Mungu amewapa the- luthi ya mali yenu wakati wa kufa kwenu.”

Na atakayeubadilisha baada ya kuusikia.

Yaani atakayebadilisha wasia na kuugeuza na hali anajua.

Basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha:

Yaani dhambi ya kubadilisha, itamwangukia yule mwenye kubadilisha, awe ni mrithi, walii, hakimu, wasii au shahidi. Hii ni dalili kwamba mwenye kufanya dhambi ni juu yake mwenyewe peke yake. Ikiwa marehemu alimuusia mtu ambaye anamwamini kuwa atamtekelezea haki ya Mwenyezi Mungu au ya watu aliyonayo, halafu aliyeusiwa akafanya uzembe au hiyana, basi maiti hana dhambi yoyote isipokuwa dhambi iko juu ya yule aliyeusiwa.

Razi anasema: “Wanavyuoni wameitolea dalili Aya hii, kwamba mtoto mdogo hawezi kuadhibiwa kwa ukafiri wa baba yake. Na haya ni katika mambo yaliyo wazi kiakili ambayo Qur’an imeyathibitisha kwa mifumo mbali mbali; kama Aya inayosema: Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mtu mwingine.” (35:18).

Mwenye kuhofia muusiaji kwenda kombo au dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi.

Kupata dhambi hapa kuna maana ya kukusudia dhulma. Aya hii inavua hukumu ya Aya iliyotangulia; yaani mwenye kubadilisha wasia atakuwa na dhambi, isipokuwa kama mwusiaji amekosea katika wasia wake. Hapo itajuzu kwa wasii au walii au hakimu kubadilisha batili kuiweka kwenye haki, sio kubadilisha haki. kwenye batili

Hayo ndiyo waliyoyataja wafasiri kuhusu maana ya Aya; nayo ni sahihi hayo yenyewe, lakini yale tunayoyafahamu kutokana mfumo mzima wa Aya, na kuyathibitisha mwenye Majmaul-Bayan, ni kwamba mtu akitokewa na dalili za mauti na akausia mambo ambayo ndani yake mna dhuluma; kama kuwapa wengine na kuwanyima wengine, na katika wasia huo wakahudhuria watu wenye akili na waumini, basi itakuwa hakuna dhambi kwa yule aliyehudhuria kumwonyesha haki mwusiaji na kusuluhisha kati yake na warithi wake, ili wote wawe wameafikiana na kuridhia, wala usizuke baina yao ugomvi na migongano baada ya kufa mwusiaji.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ {183}


Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu, ili


mpat


ekuw


an


atakua.

أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ ۚ وَأَنْ تَصُومُوا خَيْرٌ لَكُمْ ۖ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ {184}Sikumaalumzakuhisabika. Na atakayekuwa mgonjwa katikanyinyi,auyukosafarini, basi atimize idadi katika siku nyingine.Na wale wanaoweza kwa shida, watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya heri kwa kujitolea, basi ni bora kwake.Na kufunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {185}


Ni mwezi wa Ramadhan


amba


o


imete


r


emshw


a


katika


mwezi huo Qu


r


’an, kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge; na


mweny


e


kuw


a


mgonjw


a


au


safarini


,


bas


iatimiz


ehisabu


katika siku nyingine.


Mwenyez


i


Mung


u


anawatakia yaliy


o


mepes


i


wal


a


hawatakii yaliy


o


mazito


,


n


a


mkamilishe


hisab


u


hiyo


,


n


a


mumtukuze


Mwenyez


i


Mung


u


kw


a


kuwa


amewaongoza, na ili mpate


kushukuru.

  • 1. Kauli hii nimeikuta katika baadhi ya vitabu vya tafsiri nilivyonavyo, lakini inapingwa na Aya inayosema:“Aya yoyote tunayoifuta au kuisahauliza tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake ...”(2 : 106) Ambapo hapa kuna neno Khayr lililotumiwa kwa maana ya Aya iliyo bora sio mali.