read

Aya 186: Naitikia Maombi Ya Mwombaji

Maana

Inasemekana kuwa Bedui mmoja alimwendea Mtume na kumuuliza: “Mola wetu yuko karibu ili nimnog’oneze? au yuko mbali nimpigie kelele?” Ndipo ikateremshwa Aya hii kuwa ni jawabu la Bedui. Kama ni sawa kauli hii, au sio sawa lakini inanasibiana na maudhui.

Dua ni katika ibada bora na imehimizwa sana katika Qur’an na hadith. Kwa sababu ni dhihirisho la utumwa wa mtu kwa Mwenyezi Mungu na kumhitajia kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Hayo tumeyazungumzia kwa urefu katika kitabu Bainallah wal-insan.

Unaweza kuuliza: kauli yake Mwenyezi Mungu: “anaponiomba” baada ya kauli yake: “naitikia maombi ya mwombaji” ni jaribio la kupata ambacho tayari kipo, kwa sababu inafanana na kauli ya mwenye kusema: “Mwangalie mkaaji akiwa amekaa na msikilize msemaji akiwa anasema?”

Jibu: Makusudio ya “anaponiomba”, ni dua inayotoka katika moyo wa mwenye ikhlasi na mkweli katika maombi yake, sio dua ya ulimi tu. Hiyo inafanana zaidi na kauli ya mwenye kusema “Mtukuze mwanachuoni akiwa ni mwanachuoni”, akimaanisha mwanachuoni wa kikweli kweli sio mwenye jina tu la wanachuoni.

Swali la pili ambalo ni maarufu na mashuri ni: Dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu “naitikia maombi ya mwombaji”, na kauli yake; “niombeni nitawaitikia” ni kwamba Mwenyezi Mungu anamwitikia kila anayemwomba; wakati ambapo mtu anaweza kuomba sana na kunyenyekea, lakini haitikiwi maombi yake?

Wafasiri wamelijibu swali hilo kwa majibu mbali mbali, baadhi yao wakafikia majibu sita. Wote wameafikiana kwamba Mumin, mtiifu kwa Mwenyezi Mungu, huitikiwa maombi yake, kinyume cha mwingine. Lakini kauli hii inabatilika kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliitika maombi ya Iblis.

قَالَ أَنْظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ {14}

قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ {15}


“Akasema:Nipemudampakasikuwatapofufuliwa(viumbe),Akasema (MwenyeziMungu):Utakuwamiongonimwawaliopewamuda.” (7:14 -15)

Vyote iwavyo jibu la swali hilo linahitaji ufafanuzi kwa njia zifuatazo:

1. Mja kumwomba Mola wake mambo yanayopingana na desturi, kama vile kutaka riziki bila ya mihangaiko yoyote, elimu bila ya kujifundisha na mengineyo ambayo ni ya kutaka masababisho bila ya sababu, na kuingia nyumba kwa ukutani wala sio mlangoni. Hiyo siyo dua, au ni dua ya asiyemjua Mwenyezi Mungu na hekima zake na desturi yake. Kwani Mwenyezi Mungu ana desturi kwa viumbe vyake.

وَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّهِ تَبْدِيلًا {23}


“...


W


alahutapatamabadilikokatikadesturiwa MwenyeziMungu.” (48:23).

2. Kutaka tawfiq na uongofu katika hukumu za dini kwa kufanya amali za heri, kutekeleza wajibu na kuacha maasi na mambo ya haram.

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ {6}T


uongozenjiailiyonyooka”(1:6)

Vile vile dua ya kuomba kujiepusha na shari na maafa:

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ {1}

مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ {2}
SemanajilindakwaMolawaasubuhi.Nashariyaalichokiumba”(


1


13:1-2)

Pia kuna dua ya kumwomba Mwenyezi Mungu sababu za kufaulu katika riziki, elimu na afya:

“Ewe Mola wangu! nikunjue kifua changu. Na unifanyie nyepesi kazi yangu.”

Hayo yote ni kwa sharti ya kuwa mwombaji awe na ikhlasi na kumtege- mea Mwenyezi Mungu peke Yake. Hayo ndiyo maombi ya Mitume na watu wema na ndio makusudio ya dua zao.

3. Kabla ya yote inatakikana kwanza tujue na wala tusiipuuze hakika hii ambayo tunaona na kushuhudia kwa macho, nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humpa anayemwomba na asiyemwomba kwa rehema na ukarimu kutoka kwake. Na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu humpa ufalme anayemtaka na humzuilia ufalme anayemtaka, Humdhalilisha anayemtaka na humwinua anayemtaka na humpa nguvu anayemtaka bila ya dua.

Kwa hivyo basi maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba,” sio kwamba Yeye hatoi isipokuwa kwa dua. Wala hakuna maana katika kauli yake:

إِنَّ رَحْمَتَ اللَّهِ قَرِيبٌ مِنَ الْمُحْسِنِينَ {56}


“HakikarehemayaMwenyeziMunguikokaribunawanaofanyawema.” (7:56)

Kuwa rehema ya Mwenyezi Mungu iko mbali na waovu. Hapana si hiyo! Hakika rehema Yake imeenea kila kitu.

وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا {20}


“...NakutoakwaMolawakohakuzuiliki.”(17:20)

Zimekuja baadhi ya riwaya za dua ya maumivu ya tumbo, nyingine za maumivu ya mgongo, ya jicho, ya meno, n.k. Hadith hizo, ama zitakuwa zimewekwa tu, kwa sababu haziendi na hali halisi wala hazifai chochote; au pengine makusudio ni kujibidiisha kufanya matibabu pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu.
Inasemekana kwamba Amirul Muminin (a.s.) alimpitia Bedui, aliyekuwa na ngamia mwenye ukurutu karibu yake.

Imam akamwuliza Bedui: “Kwa nini humfanyii dawa?” Akajibu: “Kwa nini ewe Amirul Muminin! Ninamfanyia,” Imam akauliza: “Dawa gani?”
Bedui akajibu: Dua
Imam akasema: “Pamoja na dua tumia dawa ya utomvu.”

Basi na waniitikie na waniamini.

Razi katika Tafsiri yake anasema: “Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamwambia mja wake: Mimi ninaitikia maombi yako pamoja na kwamba Mimi sikuhitajii kabisa, basi nawe vile vile uwe ni mwenye kuitikia maombi yangu pamoja na kwamba wewe ni mwenye kunihitajia kwa kila hali. Ni ukubwa ulioje wa ukarimu huu!”

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنْتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ {187}


Mmehalalishwa usiku wa saumu kuwaingilia wake


zenu


.


W


a


o


n


ivaz


ilen


una nyiny


i


n


ivaz


ilao


.Mwenyezi Mung


u


anaju


a


kuw


a


mlikuwa


mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba


yen


u


n


a


amewasamehe


.


Basi sas


a


changanyiken


i


(onaneni) na


o


n


a


taken


i


aliyowaandikia Mwenyez


i


Mungu


.


N


a


kuleni


na kunyweni mpaka


uwabainiki


e


weup


e


w


a


Alfajiri katik


a


weus


i


w


a


usik


u


wakati


wa alfajiri. Kisha timizeni


saum


u


mpak


a


usiku


.


N


a


wala


msichanganyik


e


na


o


n


a


hali


mk


o


katik


a


itikaf


u


msikitini. Hiy


o


n


i


mipak


a


y


a


Mwenyezi


Mungu, msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu


anabainish


a


ishar


a


Zak


e


kwa wat


u


il


i


wapat


e


kumcha


.


Hiyo


ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiikurubie.


Namn


a


hi


i


Mwenyez


i


Mungu anabainish


a


ishar


a


zak


e


kwa wat


uil


iwapat


ekuw


an


atakua.

Aya 187: Mmehalalishiwa Usiku Wa Saumu

Lugha

Usiku wa saumu ni ule anaoamkia mtu akiwa amefunga. Kwa asili neno Rafath lina mana ya uchafu makusudio yake hapa ni kumwingilia mke. Vazi ni nguo ya kuvaa, lakini makusudio katika Aya hii ni kuchanganyika.

Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuwaingilia wake zenu.

Yaani inafaa kwa mwenye kufunga kumwingila mkewe katika usiku wa kufunga. Usiku wa kufunga unakusanya siku zote za Ramadhan na wala hauhusiki na usiku fulani, au sehemu fulani tu ya usiku! Hilo limefahamika kutokana na kuachiwa neno bila ya kufungwa na kitu kingine.

Mwenyezi Mungu amefumba kuwaingilia kwa neno rafath (uchafu) kwa ajili ya kuitakasa ibara; kama vile ambavyo amefumba katika Aya nyingine kwa maneno kama: Kugusa, kuingiliana na kukurubiana. Ibn Abbas anasema: "Mwenyezi Mungu ni mwenye staha hufumbia anachotaka."

Wao ni vazi lenu, na nyinyi ni vazi lao.

Baadhi ya wafasiri wanasema; vazi hapa ni fumbo la kukumbatiana. Razi anasema: Rabia amesema ni kuwa wao ni tandiko kwenu na nyinyi ni shuka kwao.

Haya ni sawa na tafsiri ya Mustashriqina wanaosema: Wao ni suruali kwenu na nyinyi ni suruali kwao. Ilivyo hasa ni kuwa neno Libas ni matokeo ya neno Labis kwa maana ya kuchanganyika kuvaanas.
Makusudio kwa ujumla ni kubainisha hukumu ya kuruhusiwa kuingiliana na wanawake usiku wa saumu; kwani mke na mume wakiwa pamoja na kutangamana, basi inakuwa uzito sana kwa mume kuvumilia.

Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe.

Msemo unawaelekea baadhi na wala sio wote. Hilo tunalifahamu kutokana na neno hiyana, kutakabali toba na msamaha.

Wafasiri wengi wanasema kwamba Mwenyezi Mungu alimhalalishia mfungaji tangu mwanzo wa sharia, kula na kunywa na kujamiiana na mkewe usiku wa saumu kwa sharti la kutolala au kuswali swala ya Isha. Kwa maana ya kuwa akilala usiku au kuswali Isha, basi ni haramu juu yake kula, kunywa na kujamii mpaka uingie usiku unaofuatia. Na kwamba sahaba mmoja alivunja sharti hili; hivyo akamjamii mkewe baada ya kuamka; kisha akajuta sana na akakiri makosa yake kwa Mtume (s.a.w.w.); ndipo ikashuka Aya hii.

Vyoyote iwavyo ni kwamba nafsi ina mambo ambayo inakuwa vigumu kujizuwiya nayo. Kwa hiyo mtu huishibisha kwa kujificha au kwa kuasi dini ya Mwenyezi Mungu. Basi lililo bora ni kuhalalisha lile linalopen- delewa ikiwa kuna njia yoyote ya kuhalalisha, ili mtu asivutwe kwenye maasi mara kwa mara, hatimaye kuwa mwenye dharau na kutojali dini na hukumu za Mwenyezi Mungu.

Na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu.

Ambayo ni kustarehe na wanawake wakati wa usiku wa saumu, jambo ambalo hapo mwanzo lilikuwa haramu.

Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainike weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku.

Yaani mmehalalishiwa kujamiina kuanzia mwanzo wa usiku mpaka machimbuko ya Alfajiri.

Imepokewa Hadith ya Mtume (s.a.w.w.): "Alfajiri ni mbili: Ama ile ambayo iko kama mkia wa mbwa mwitu hiyo haihalalishiwi kitu (swala) wala kuharimishiwa (kula). Ama iliyo katika umbo mstatili ambayo inae- nea pambizoni, hiyo ni halali kuswali ndani yake na ni haramu chakula”.

Kisha timizeni saumu mpaka usiku.

Mwanzo wa saumu ni kuanzia Alfajiri na mwisho wake ni unapoanza usiku. Usiku unaingia kwa kutua jua, lakini kutua kwake hakuwezi kujulikana kwa kufichika machoni tu, bali hujulikana kwa kutoweka wekundu upande wa mashariki kwa sababu mashariki ndiyo inayochomoza magharibi. Kwa hivyo wekundu wa mashariki unakuwa ni akisi ya mwanga wa jua, na kila linavyozidi kujificha zaidi jua ndipo akisi hii inavyopotea

Ama yale wanayotuhumiwa Shia kwamba wao wanachelewesha swala ya Magharibi na futari ya Ramadhan mpaka zitokeze nyota, huo ni uongo na uzushi. Imam Sadiq (a.s.) aliambiwa kuwa watu wa Iraq wanachelewesha swala ya Magharibi mpaka zitokeze nyota. Akasema. "Hiyo ni kazi ya adui wa Mwenyezi Mungu Abul Khatwab."

Na wala msichanganyike nao, na hali mko katika itikafu msikitini.

Katika vitabu vya Fiqh kuna mlango mahsus unoitwa mlango wa itikafu. Aghlabu mafaqihi huutaja baada ya mlango wa saumu. Maana ya itikafu katika sharia ni kukaa mtu katika msikiti wa jamaa sio chini ya siku tatu, kwa masiku mawili, kwa mwenye kufunga; kwamba asitoke msikitini isipokuwa kwa haja muhimu na kurudi mara moja anapomaliza.

Ni haramu kwa mwenye kukaa itikafu kuingiliana na mwanamke usiku au mchana; hata kubusu na kugusa kwa matamanio.
Kukatazwa hapa, kunafungamana na kuvaana na mwanamke kwa hali yoyote; iwe ni ndani ya msikiti au nje. Mwenye kukaa itikafu akitoka msikitini na akajamiiana na mwanamke usiku, hata kama atakoga na kurudi msikitini, atakuwa amefanya haramu; na itamlazimu kutoa kafara ya mwenye kufungua makusudi katika mwezi wa Ramadhan - kumwachia huru mtumwa, au kufunga miezi miwili mfululizo au kulisha maskini sitini.

وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ {188}


W


alamsilemali zenubaina yenu kwabatili na kuzipelekakwa mahakimuili mpate kulasehemuyamali yawatukwadhambinahali mnajua.