read

Aya 188: Kula Mali Kwa Batili

Maana

Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili.

Msemo unaelekezwa kwa wote wenye kulazimiwa na sharia. Maana ya msile mali zenu, ni sawa na kauli yake. Mwenyezi Mungu; "Msijiue" yaani msiuane.

Hiyo inafahamisha umoja wa utu, na kwamba utu ni kama kiwiliwili kimoja na watu ni viungo vyake, lilopata kiungo kimoja linafikia kiungo kingine.

Makusudio ya kula, ni kutumia mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali. Neno "kati yenu" katika Aya linahusisha mali iliyotokana kwa mabadilishano ya haramu, kama riba; au mali iliyosimama kwa haramu, kama pombe, nguruwe ambayo hayathibitishwi na sharia.

Mfano wa hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu: "... Msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana...."(4:29)

Ama uharamu wa mali iliyochukuliwa kwa unyang'anyi, wizi kiapo cha uongo, n.k. hayo yanafahamika kwa dalili nyingine. Kwa ajili hii, ndipo mafaqihi wakatoa dalili kwa Aya mbili hizo juu ya kubatilika kila muamala (mapatano) alioharamisha Mwenyezi Mungu. Aya hii inafahamisha wazi wazi kwamba Uislamu unakubali mtu kumiliki chake. (mali ya mtu binafsi.)

Na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi.

Haya yanaungana na kula. Makusudio ya dhambi hapa ni rushwa, kwa kuangalia mfumo wa maneno ulivyo. Maana yaliyokusudiwa ni kukataza kutoa rushwa kwa mahakimu kwa ajili ya kula mali za watu.

Na hali mnajua.

Yaani msifanye dhambi hii na hali mnajua ubaya wake. Hakuna mwenye kutia shaka kwamba kufanya jambo ovu na huku mtu anajua, ni uovu zaidi kuliko kufanya na shaka shaka.

Kuna hadith isemayo: "Kujizuia na shaka shaka ni bora kuliko kujitia katika maangamizo." Basi itakuwa ni bora zaidi kujizuia ikiwa mtu anajua uharamu.

Rushwa ni katika mambo makubwa yaliyoharamishwa, hata katika hukumu ya haki. Mwenyezi Mungu ameilaani rushwa na mwenye kuitoa, mwenye kuipokea na mwenye kuwaunganisha wawili hao.

Imepokewa Hadith inayofahamisha kuwa rushwa ni kumkufuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na riwaya nyingine inasema ni shirk.

Hukumu Ya Kadhi Fasiki

Hanafi anasema kuwa hukumu ya Kadhi fasiki inafaa, hayo yameelezwa katika kitabu kiitwacho Ibn Abidin chapa ya mwaka 1325 hijriya., mlango wa Hukumu. Ninamnuukuu; "Fasiki ni mtu wa kutoa ushahidi, kwa hiyo anaweza kuwa Kadhi."

Na katika kitabu Fat-hul Qadir J5 uk. 454 mlango wa hukumu amese- ma; "Ilivyo ni kuwa hukumu ya kila mtawala inafaa, hata kama ni mjinga tena fasiki, na hayo ndiyo yaliyo wazi katika madhehebu yetu."

Shia Imamiya wamesema kwa kauli moja kwamba fasiki hawezi kuhuku- mu, na hukumu yake haifai kutekelezwa, hata awe na elimu kiasi gani.

Wamelitilia mkazo hilo kundi la mafaqihi wa Kiimamiya waliposema kuwa mwenye haki haijuzu kupeleka madai yake kwa kadhi asiye mwadilifu, hata kama ikibidi kuwa haki yake hawezi kuipata isipokuwa kwake, kwa namna ambayo lau si kadhi huyo, basi haki yake itapotea.

Akihalifu mwenye haki yake, basi haijuzu kuchukua chochote kilichohukumiwa hata kama ni haki; kwa kuchukulia kauli ya Imam Jaffar As Sadiq (a.s.): "Anachokichukua ni haramu, ijapokuwa ni haki yake iliy- omthibitikia."

Mafaqihi wengi wa kiimamiya wamesema kwamba mwenye haki anaweza kumtaka msaada asiyekuwa mwadilifu katika kupata haki yake ikibidi, ikiwa hawezi kupata njia nyingine, bila ya kutofautisha kuwa haki yenyewe ni deni au mali.

Kwa sababu kuzuia madhara ya nafsi kunajuzu, bali mara nyingine huwa ni wajibu, ikiwa hakutimii isipokuwa kumrudia asiyekuwa mwadilifu. Ama dhambi na haramu iko juu ya mwenye kuizuia haki sio mwenye kuchukua haki yake.

Hukumu Ya Kadhi Haibadilishi Uhakika Wa Mambo

Hakimu mwadilifu akiwahukumu watu wawili na akampa haki asiyekuwa na haki kwa kushindwa kutoa ushahidi mwenye haki, basi haijuzu kuchukua alichohukumiwa. Kwa sababu hakimu hageuzi uhakika.

Mtume (s.a.w.w.) anasema: "Mimi ni mtu kama nyinyi isipokuwa napewa wahyi tu, na nyinyi mnapokuja kutaka hukumu kwangu, huenda mwingine akawa fasaha zaidi kwa hoja kuliko mwenzake. Nikihukumu kutokana na niliyosikia, basi ninayemhukumia kitu katika haki ya nduguye, (ajue) nimehukumia kipande cha moto."

Lakini Abu Hanifa amesema kinyume cha hivyo. Akinukuliwa na mwenye Tafsir Al-Manar katika kuelezea Aya hii, Abu Hanifa amesema: "Kadhi akihukumu kuvunjika ndoa kati ya mume na mke kwa ushahidi wa uongo, itakuwa haramu kwao kuishi maisha ya ndoa.

Na kama shahidi akitoa ushahidi wa uongo kwamba fulani amemuoa fulani na hakimu akahukumu kuwa ni sawa, basi ni halali kwa mwanamume kumwingilia bila ya ndoa, kwakutosheka na hukumu ya Kadhi ambayo anajua kuwa sio haki."

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَنْ تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ ظُهُورِهَا وَلَٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {189}


Wanakuuliza kuhusu ya miezi.Sema:'Hiyonivipimo vya nyakati kwa ajili yawatu naHijja.


W


alasiwemakuingiamajumba kwa nyuma yake, bali mwema nialiye na takua. Na ingieni majumba kupitia milangoni mwake, na mcheni Mwenyezi Munguilimpatekufaulu.