read

Aya 189: Wanakuuliza Kuhusu Miezi

Maana

Wanakuuliza kuhusu miezi.

Swali hili linawezekana kuwa pande mbili, ikiwa hatukuangalia jibu lake linalofuatia: Kwanza, nikuwa ni swali la kutaka kujua sababu za kisayansi; kutokana na tofauti inayoonekana - kuanzia mwezi mwandamo, kisha mwezi mkamilifu, tena unarudi kama ulivyokuwa. Pili, kuwa ni kuuliza hekima yake, sio sababu za kisayansi.

Tukiliangalia swali pamoja na jibu lake: “Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu”, litakuwa ni swali la hekima tu, na wala sio la sababu za kisayansi. Hili ndilo lenye nguvu zaidi.

Ama kauli ya anayesema kuwa wao waliuliza kuhusu sababu za kisayansi na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.). akamwamrisha Mtume wake kuwajibu kwa kubainisha hekima kuonyesha kuwa swali lao haliko mahali pake, kwa sababu wao wameshindwa kufikia kwenye sababu za kisayansi ambazo zinahitaji darasa ndefu na zenye undani na utangulizi mwingi wa kielimu; na ilivyotakiwa wao waulize hekima na faida ya kutofautiana miezi, jambo ambalo wao wanaweza kulifahamu. Kauli hiyo haitegemei dalili yoyote isipokuwa kuonelea kuwa ni vizuri hivyo tu.

Unaweza kusema kuwa dalili iko; nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Wala si wema kuingia majumba kwa nyuma”.

Kwamba kuuliza kwenu sababu za kisayansi, ni sawa na kutaka kuingia nyumba kwa nyuma; lakini kuuliza kwenu hekima yake, ni kama anayetaka kuingia nyumba kwa mlango wake.

Jibu, kwanza hiyo ni Ijtihadi ya kuleta taawili ya tamko na wala sio kutafsiri dhahiri ya tamko. Pili, imethibiti kuwa jumla hii imeshuka kutokana na waliyokuwa wakiyafanya wakati wa kijahilia, ya kuingia nyumba kwa nyuma. Ufafanuzi ni kama ifuatavyo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake kuwajibu kuwa heki- ma ya kutofautiana miezi ni kuyawekea wakati maslahi yao na mambo yao ya kidunia, kama vile madeni na kukodisha; na mambo yao ya kidini, kama vile Hijja na saumu.

Kwa maneno mengine ni jibu linapitia katika kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t) “: ...Ili mjue idadi ya miaka na hisabu..." (10:5) Wala si wema kuingia majumba kwa nyuma yake.

Bali mwema ni yule anayemcha Mwenyezi Mungu.

“Na ingieni majumba kupitia milangoni mwake”. Wafasiri wengi wasema wakati wa kijahiliya mtu kuwa anapohirimia Hijja, hutoboa tundu ya kuingilia au hutengeneza ngazi ya kupanda sakafuni; na akiwa ni katika Mabedui hutoka nyuma ya kibanda.

Baadhi ya waislamu nao walikuwa wakifanya hivyo hapo mwanzo mwanzo, ndipo ikashuka Aya kuwabainishia kwamba wema ni kumwogopa Mwenyezi Mungu, kufanya amali za heri na kujiepusha na maasi na machafu, sio kuingia majumba kwa nyuma na mengineyo ambayo hayaingii akilini wala kuwa na lengo la dini na imani.

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ {190}


Napiganenikatika njiaya Mwenyezi Mungu nawale wanaowapiga, wala msichokoze.Hakika Mwenyezi Munguhawapendiwachokozi.

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِنْدَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِنْ قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ {191}


Nawauwenipopotemuwapatapo na muwatoe popote walipowatoa; na fitina ni mbayazaidikulikokuua.W


ala msipigane nao karibu na MsikitiMtukufumpakawapigane na nyinyi huko.


W


akipiganananyinyi basi nanyi piawapigeni.Namna hivindivyo yalivyo malipo ya makafiri.

فَإِنِ انْتَهَوْا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {192}


Lakini kamawakikoma, basi hakika Mwenyezi Munguni Mwenye maghufira,Mwenyeku


r


ehemu.

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّهِ ۖ فَإِنِ انْتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ {193}


Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina, na diniiwe ya Mwenyezi Mungu. Na kama wakikoma, basiusiwekouaduiilakwamadhalmu.