read

Aya 190-193: Na Piganeni Katika Njia Ya Mwenyezi Mungu

Lugha

Neno Fitna lina maana ya balaa na misukosuko, na makusudio yake hapa ni ukafiri, yaani kuwaharibu watu na dini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kutokana na kulinganganisha na neno "Na dini iwe ya Mwenyezi Mungu peke yake."

Maana

Katika Majmaul Bayan imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipotoka yeye na sahaba zake katika mwaka ambao walitaka kufanya Umra wakiwa watu elfu moja na mia nne (1400), walipofika Hudaybia, Washirikina waliwazuia wasiingie Al Ka'aba. wakachinjawanyama hapo Hudaybia;1 kisha wakafanya suluh na washirikina kurudi, na waje mwaka ujao.

Mwaka ulipofika Waislamu walijiandaa kutekeleza Umra, lakini wakaogopa kupigwa vita na Washirikina. Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zake wakachukia kupigana na washirikina katika mwezi mtukufu tena ndani ya Haram (sehemu takatifu ya Makka).

Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii, na kuidhinishwa kupigana. Baadhi ya jamaa wamesema hiyo ndiyo Aya ya kwanza kushuka kuhusu vita.

Uislamu Unapiga Vita Dhulma Na Ufisadi

Baadhi ya ambao wana ghera juu ya Uislamu na kujaribu kuugombea Uislamu kwa kila njia, hata kama itapigana na misingi ya Qur'an, wamesema kuwa Uislamu hauruhusu kupigana na yeyote isipokuwa mchokozi; na vita vya Kiislamu, katika zama za Mtume, vilikuwa ni vya kujikinga sio hujuma na walitoa dalili kwa aya kadhaa miongoni mwazo ni Aya hii tuliyonayo sasa na Aya nyingine inayosema: "Na piganeni na makafiri nyote kama wao wote wanavyopigana nanyi nyote" (9:36)

Lililowafanya kuugombea hivyo Uislamu, ni madai ya maadui wa Uislamu kwamba Uislamu ni dini ya vita, sio dini ya amani, kwa kisingizio cha vita vya Mtume (s.a.w.w.).

Ilivyo hasa ni kuwa Uislamu umeruhusu kupigana kwa sababu zifuatazo: Kujikinga

Kupigana na madhalimu; Mwenyezi Mungu anasema: “Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni, likiwa moja la hayo linadhulumu jengine, basi lipigeni lile linalodhulumu mpaka lirudie kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." (49:9)

Kumaliza ukafiri wa wanao mkufuru Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَنْ يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ {29}


"PiganeninawalewasiomwaminiMwenyeziMunguwalasikuyamwisho, walahawaharimishialivyoviharimishaMwenyeziMungunaMtumewake wala hawafuati dini ya haki miongoni mwa waliopewa kitabu,(piganeni nao)mpakawatoekodikwahiariyao,haliwametii."(9:29)

Mtume amesema: "Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka waseme hapana Mungu isipokuwa Allah. Kama wakisema, basi imehifadhika nami damu yao na mali zao."

Lakini kupigana kwa aina hii hakuruhusiwi isipokuwa kwa idhini ya Masum au naibu wake kuepuka vuruga.

Kujuzu kupigana kwa kujikinga, hakuna maana kuwa hakuna idhini ya kupigana kwa malengo mengine, kama vile kumaliza dhulma na ukafiri. Uislamu umeruhusu kupigana kwa ajili ya kupatikana dini ya haki na uadilifu, kwa sababu ukafiri wenyewe ni uadui katika Uislamu. Lakini Uislamu umeharamisha kupigana kwa ajili ya kutawala watu na kuwapokonya uwezo wao na kutawala uchumi wao.

Uislamu umejuzisha kutumia nguvu kumaliza maovu na madhambi na kupigania haki za binadamu, uhuru wake na heshima yake. Wakoloni walianzisha vita wakaleta machafuko na kumwaga damu, wakatafuta elimu kwa ajili ya kuua na kunyonya, na kuiweka juu dhulma na uadui 2

Hilo ndilo jawabu la wale wanaojaribu kuutweza Uislamu na Nabii wake, kwamba Uislamu ni dini ya vita na upanga. Na kweli Uislamu ni dini iliyokamilika. Inampiga vita kila asiyefuata haki na uadilifu na anayeleta uharibifu na ufisadi katika ardhi. Na kumkufuru Mwenyezi Mungu ni dhulma na ufisadi katika dini ya Kiislamu na sharia yake.

Kulingana na suala hili hatuna budi kudokeza kuwa mafaqihi wa madhehebu zote za Kiislamu wameafikiana kwa kauli moja kwamba mwenye kuvunja miko ya Mwenyezi Mungu kwa kuihalalisha na kwa kumwaga damu na kunyakua mali, basi yeye ni mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu; hata kama akiswali na kufunga na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu; bali huyu ni mwovu zaidi kuliko yule mwenye kukufuru, lakini akazuia umwagikaji damu na kunyakua mali na akijizuia kuwaudhi watu.

Ndio, wote wawili ni makafiri, lakini kafiri mwingine ni mwovu kwa Mwenyezi Mungu na kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Bora ya watu ni yule mwenye kuwanufaisha zaidi watu, na mwovu zaidi wa watu ni yule ambaye watu wanahofia shari yake."

Tunasema tena kila mwenye kukanusha hukumu ya kisharia iliyothibitika kwa dhahiri ya dini na Waislamu wote, basi huyo ni kafiri hata kama amezaliwa na wazazi Waislamu na akatamka shahada mbili.

Wala msichokoze.

Yaani, msipigane kwa ajili ya manufaa ya kiutu, bali piganeni kwa lengo la heshima ya utu binafsi na kwa lengo la kuihami dini na haki msiwaue watoto, wazee na wagonjwa. Vile vile msiharibu majengo na kukata miti. Mafunzo yote haya na mengineyo yamekuja katika Sunna za Mtume.

Waueni popote muwapatapo.

Yaani waueni makafiri wakati wowote na mahali popote walipo isipokuwa kwenye Msikiti Mtukufu, kwa sababu kupigana hapo ni haramu isipokuwa wakianza humo
Unaweza kuuliza: Katika Aya ya mwanzo kumeamrishwa kupigana na anayepigana na Waislamu, lakini kwenye Aya hii kumeamrishwa kupigana tu, bila ya kufungamanishwa na kitu kingine. Je, Aya hii imefuta hukumu ya hukumu ile?

Jibu: Hapana kufutwa hukmu. Hivi punde tumeonyesha kwamba kujuzu kupigania nafsi hakufahamishi kuwa hakuna ruhusa ya kupigana kwa malengo mengine; kama vile kumaliza ukafiri na dhulma. Kama ukimwambia mtu 'wewe ni mtu mzuri' haina maana kuwa mwingine si mtu mzuri.

Basi hivyo hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu: 'Piganeni na wanaowapiga' haina maana msipigane na wasiowapiga. Ndio, kama angelisema msipigane isipokuwa na wanaowapiga, hiyo ingefahamisha kufunga huko ni kwa kukanusha.

Na muwatoe popote walipowatoa.

Washirikina wa Makka walimtoa Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zake hapo Makka, si kwa lolote isipokuwa tu masahaba hao wameamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake na Waislamu wakirudi Makka wakiwa washindi, wamtoe hapo kila asiyemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; sawa na vile walivyofanywa na washirikina 'malipo yenye kulingana.' Inasemekana Mtume aliwatoa washirikina ulipokuja msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi kwa kuchukulia Aya hii.

Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua.

Hii ni sababu ya kujuzu kuwaua washirikina. Makusudio ya fitina ni ushirikina. Maana ya kuwa mmeruhusiwa kuwaua washirikina, ni kuwa dhambi ya shirk ni mbaya zaidi kuliko dhambi ya kuua.

Baadhi ya tafsiri zinasema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekusudia katika kauli yake hiyo, kuwa Washirikina wa Makka hapo mwanzo wa mwito wa Uislamu walikuwa wakimfitini mwenye kusilimu kwa kumuudhi kumwadhibu na kumtoa mjini kwake. Na hiyo ni fitina mbaya zaidi kuliko kuua. Kwa ajili hii ndio kukaruhusiwa kuwaua na kuwatoa mijini mwao.

Vyovyote iwavyo makusudio ya neno Fitna katika Qur'an sio ya kufanya umbeya na udaku kama wanavyofikiria wengi.

Wala msipigane nao karibu na Msikiti mtukufu mpaka wawapige huko.

Hili ni sharti la kujuzu kupigana katika Haram tukufu ambayo ameharamisha Mwenyezi Mungu kupigana ndani yake isipokuwa kama ikivunjiwa heshima kwa kupigana.

Wakipigana nanyi basi nanyi pia wapigeni. Kwa sababu wao wameanza na wakauvunjia heshima Msikiti mtakatifu na mwenye kuanza hakudhulumiwa, isipokuwa yeye ndiye dhalimu.

Lakini kama wakikoma, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, Mwenye kurehemu. Kulingana na mfumo wa maneno ulivyo, unahukumia kuwa maana yake ni, basi nanyi jizuieni nao na muwasamehe, kwa vile sababu iliyolazimisha kupigana nao ni kuanza kwao vita; wakijizuia basi sababu imeondoka.

Wafasiri wengi wamesema kuwa maana yake ni, wakitubia kutokana na ukafiri na wakamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa sababu kafiri hawezi kusamehewa na Mwenyezi Mungu kwa kuacha kupigana tu, bali husamehewa kwa kuacha kufuru. lakini huku ni kumuhukumia Mwenyezi Mungu(s.w.t.) kwa sababu Yeye anaweza kumsamehe anayemtaka, hata kama ni kafiri.

Ni kweli kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kumwadhibu mwema kabisa, sababu Yeye ni Mwadilifu, lakini anaweza kum- samehe mkosaji kwa namna yoyote ya uovu itakavyokuwa, kwa sababu Yeye ni Karimu, Mwenye huruma.

Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina na dini iwe ya Mwenyezi Mungu.

Yaani Jihadi ni kwa ajili ya imani ya Mwenyezi Mungu. Kumaliza ukanushaji (wa kumkanusha Mwenyezi Mungu) ni wajibu maadam duniani kuna athari ya shirki na ulahidi. Kama yakiondoka haya na watu wote wakaamini, basi wajibu wa Jihadi utakuwa umeondoka.

Kwa ujumla ni kwamba wajibu wa Jihadi kwa ajili ya kuueneza Uislamu una sharti ya kupatikana idhini ya Imam mwadilifu na wala haijuzu kwa hali yoyote bila ya amri yake. Ama Jihadi ya kuihami dini na nafsi, wajibu wake umeachwa bila ya kuwekwa sharti lolote.

Na kama wakikoma basi usiweko uadui ila kwa madhalimu.

Yaani kama wakiacha ukafiri na wakasilimu basi si halali kuwaua isipokuwa kwa sababu zinazowajibisha kuua, ambazo ni moja kati ya mambo matatu: Kukufuru baada ya kuamini, kuzini baada ya kuwa na mke na kuua mtu bila ya haki yoyote.

الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ {194}


Mwez


imtakatif


ukw


amwezi mtakatifu


;


n


a


vit


u


vitakatifu vin


a


kisasi


.Bas


iwanaowa


chokoza, pia nanyi


wachokozen


ikw


a


kadiri


walivyowachokoza. Na


mchen


i


Mwenyez


iMung


u


na


jueni kwambaMwenyezi Mungu yuko pamoja na


wanaomcha.

وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ {195}


Natoeni katika njia ya Mwenyezi Mungu wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu, na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu


huwapend


awafanya


owema.

  • 1. Hayo yalikuwa mwezi wa Dhul-qada (mfunguo pili) mwaka wa sita wa Hijriya. Na Hudaybia siku hizo ilikuwa na maji mengi na miti, lakini leo imegeuka na kuwa jangwa kama nilivyoiona mwaka 1964 A.D.
  • 2. Mnamo mwaka 1957 kilitolewa kitabu huko Amerika, kinachohusu Mustakabali wa nguvu za nuklia cha Torry Tony. Anaeleza mtungaji kwamba maendeleo ya elimu yame- teremsha bei ya kumuua Mtu. Mwanzo bomu la Atomic lilikuwa likigarimu pauni nyingi baadaye ikagarimu pauni moja na baada ya bomu la haidrojeni kumua mtu kukawa kunagharimu shilingi moja tu.