read

Aya 194-195: Miezi Mitakatifu

Maana

Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu.

Miezi mitakatifu ni minne; mitatu inafuatana, nayo ni Dhul-Qaada, Dhul Hijja na Muharram (mfunguo pili, mfunguo tatu na mfunguo nne). Na mwezi mmoja uko pekee na ni (Rajab). Miezi hii imeitwa mitakatifu kwa sababu ya kuharamishwa kuuana ndani ya miezi hiyo. Katika wakati wa ujahiliya na wa Uislamu, ilikuwa mtu anaweza kukutana na mtu aliye- muua baba yake katika miezi hiyo na asimfanye chochote.

Yameshatangulia maelezo kwamba Mtume na sahaba zake walitaka kufanya umra katika mwezi wa dhul-Qaada (mfunguo pili) mwaka wa sita (6 Hijriya), wakazuiwa na washirikina na wakatupiwa mishale na mawe; kisha waka-fanyiana suluhu kuwa Waislamu warudi mwaka utakao- futia. Lakini Waislamu wakaogopa washirikina wasije wakaanza kupigana katika mwezi mtakatifu; ndipo Mwenyezi Mungu akawapa idhini ya kupigana na washirikina na akabainisha kuwa lenye kukatazwa ni kuanza uadui wa kupigana na sio kujikinga.

Kwa hivyo maana ya mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu ni kwamba mwenye kuihalalisha damu yenu enyi Waislamu katika mwezi huu, basi nanyi ihalalisheni damu yake katika mwezi huo huo.

Na vitu vitakatifu vina kisasi.

Yaani mwenye kuvunja heshima ya Mwenyezi Mungu atalipizwa kisasi na atafanywa kama alivyofanya. Hiyo ndiyo asili kwa ujumla inayoondoa kila udhuru wa mwenye kuvunja heshima. Mwenye kuhalalilisha damu za watu, mali zao na heshima zao, naye atahalalishwa kwa kiasi kile ali- chowafanyia.
Heshima kwa mtu mwingine inatokana na heshima ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kama akivunja heshima ya mwingine. Hapo itakuja haki ambayo daima inakuwa juu na wala haikaliwi. Hapa ndipo tunapata tafsiri ya:

Anayechokoza pia nanyi mchokozeni kwa kadiri alivyo wachokoza.

Sharti la kulipiza ni kuwa sawa na kosa la aliyeanza bila ya kuzidisha au kupunguza. Hicho ndio kisasi hasa kilivyo.

Unaweza kuuliza: Mwenye kuchokoza , yeye ni mchokozi bila ya wasiwasi wowote, lakini mwenye kulipiza kisasi bila shaka siye mchokozi. Kwa hiyo kuna wajihi gani kwa Mwenyezi Mungu kusema: Mchokozeni

Jibu: Makusudio ya kuwafanyia uchokozi, sio uchokozi hasa kwa maana yake, isipokuwa makusudio ni malipo ya uchokozi uliofanywa kwa kipimo chake bila ya kudhulumu. Hayo ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu(s.w.t.): "Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo..." (42:40)

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Kutoa katika njia yake Mwenyezi Mungu kunakuwa ni kwa masilahi ya umma; kama vile shule, hospitali na nyumba za kulea mayatima. Vile vile jihadi, sadaka kwa mafukara na masikini na kuwalisha watu wa nyumbani. Bora zaidi ya kutoa ni kule kunakohusika na kutia nguvu na kuieneza dini, kuthibitisha haki na kuibatilisha batili.

Wala msijitie, kwa mikono yenu, katika maangamivu

Mwenyezi Mungu ametumia neno mikono kwa maana ya mtu kujiingiza mwenyewe. Kama tukiangalia jumla hii peke yake tu bila ya kuangalia mfumo mzima wa maneno, ingelikuwa maana yake ni kuwa haijuzu kwa mtu kufanya lolote ambalo lina madhara na bila ya kuwako manufaa kwa ujumla.

Lakini tukichunga mfumo wa maneno na kuja kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamivu" baada ya kusema: "Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu", basi maana yanakuwa, toeni katika mali zenu sio kwa ubahili wala ubadhirifu, kwa sababu yote hayo mawili yanaleta uangamivu.

Kwa hivyo Aya kwa maana haya inakuwa kama ile Aya isemayo:

وَالَّذِينَ إِذَا أَنْفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا {67}


"Na wale ambao wanapotoahawafanyi ubadhirifu wala ubahili, bali wanakuwakatikatiyahayo."(25:67)

Inasemekana pia kwamba maana yake ni: Msijitie kwa mikono yenu kwenye maangamivu kwa kuacha kupigana jihadi na maadui wa dini na kutoa mali kwa ajili ya kuwaandaa wapigania jihadi, kwa sababu hilo litawaogopesha na atawaweza adui; muangamie na mdhalilike.

Haya ndiyo yaliyothibitishwa na majaribio waliyoyapitia Waislamu. Wamekosa uhuru wao na heshima yao tangu walipoacha jihadi na kutoa mali kwa ajili ya kuinusuru haki na uadilifu. Hivyo akapata tamaa kila mnyang'anyaji na mnyakuzi; hata Wazayuni, vibaraka wa ukoloni, nao waliivamia Palestina mnamo 1948. Baada ya Waarabu kunyamaza na wasifanye jihadi.

Baada ya miaka ishirini wakateka Sinai na ukanda wa Gaza Magharibi mwa mto Jordan; wakazikalia sehemu hizo kwa msaada wa Amerika, Uingereza na Ujerumani Magharibi. Wakawaua wanaume na kuwafukuza wanawake na watoto. Lau Waislamu wangefanya jihadi kabla yake, wangeliokoka na maangamizo haya na udhalili huu, na wala dola ya Israel isingekuwepo kabisa.

Na fanyieni wema Kwa jihadi na kujitolea mali katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kila njia inayomridhisha Mungu na yenye sifa nzuri.

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِنْ رَأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِنْ صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنْتُمْ فَمَنْ تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَنْ لَمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ {196}


Natimizen


iHijj


an


aUmra


kwaajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama waliowepesikupatikana.


W


ala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyamahaowafikemachinjionimwao. Na atakayekuwa mgonjwa katikanyinyi au ana adha kichwanimwake, basiatoefidiakwa kufunga au sadaka aukuchinja mnyama.Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujista


r


eheshakwakufanyaUmra,kisha akahiji,achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyepata, nikufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporudi; hizo ni siku kumikamili. Hayonikwa yuleambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungunimkaliwakuadhibu.

الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَعْلُومَاتٌ ۚ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ {197}


Hijja ni miezi maalumu. Na


anayejilazimish


a


kufanya


Hijja katika miezi hiyo, basi hakunakuchafuawalaufuska wala mabishano katika Hijja. Na heri yoyote mnayoifanya MwenyeziMungu anaijua. Na chukuenimasurufu,na hakika masurufu bora ni takua; na nicheni Mimi,enyiwenyeakili.

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلًا مِنْ رَبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُمْ مِنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّهَ عِنْدَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِنْ كُنْتُمْ مِنْ قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ {198}


Sivibayakwenukutafutariziki ya Mola wenu. Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril-Haram: Na mkumbukeni kama alivyowaongoza, ijapokuwazamani mlikuwa miongonimwawaliopotea.

ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {199}


Kisha miminikeni kutoka mahali wanapomiminika watu (wote), na mumwombe Mwenyezi Mungu maghufira; hakikaMwenyeziMungu ni Mwenye kughufiria Mwenye ku


r


ehemu.

فَإِذَا قَضَيْتُمْ مَنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ {200}


Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu; bali mtajeni zaidi. Na kuna baadhi ya watu wasemao:Molawetu!


T


upeduniani;naokatika Akhera, hawanalolote.

وَمِنْهُمْ مَنْ يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ {201}


Na miongoni mwao kuna asemaye;Molawetu!T


upemema duniani na (tupe) mema Akhera, na utulinde na adhabuyaMoto.

أُولَٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ {202}


Hao ndio wenye fungu kati


k


a


waliyoyachuma


,


na Mwenyez


i


Mung


uni


Mwepesiwakuhisabu.

وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَعْدُودَاتٍ ۚ فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ {203}


N


amtajen


i


Mwenyezi


Mungu katika siku zinazo


hisabiwa


.


N


a


mwenye


kufanya haraka katika siku


mbili


,


bas


i


s


i


dhamb


i


juu


yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenyetakua. Namcheni MwenyeziMungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusany- waKwake.