read

Aya 196-203: Timizeni Hijja Na Umra

Maana

Aya hizi zimeonyesha baadhi ya hukumu za Hijja, Mafaqihi wameweka vitabu maalumu vinavyohusu Hijja, nami nimetunga kitabu kwa jina Al- Hajj ala Madhahabil-Khamsa; kisha nikakiunganisha katika kitabu Al- Fiqh ala Madhahabil Khamsa wakati kiliporudiwa kuchapishwa kwa mara ya tatu. Vile vile nimeizungumza kwa urefu katika Juzuu ya pili ya kitabu Fiqh ul-Imam Jaffar Sadiq (a.s.)

Hijja imekuwa maarufu tangu zama za Nabii Ibrahim na Ismail (a.s.) na iliendelea katika zama za ujahiliya; na Uislamu ukaithibitisha baada ya kuisafisha na mambo machafu, na kuongeza baadhi ya ibada.

Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Maana ya Hijja kilugha, ni kukusudia, na kisharia ni ibada maalum katika mahali na wakati maalum. Umra kilugha ni ziara yoyote; na kisheria ni ziara katika Al-Ka’aba kwa namna maalum,

Hijja ni wajibu katika Qur’an, Hadith na Ijami. Bali wajibu wake umethubu- tu kwa dhahiri ya dini. Na mwenye kuikanusha sio Mwislamu, sawa sawa na aliyekanusha wajibu wa Saumu na Swala. Shia Imamiyya na Shafii wamesema Umra ni wajibu, Hanafi na Malik wamesema ni Sunna.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu “Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” Yaani Hijini na fanyeni Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake na sio kwa makusudio ya kidunia. Kwani Waarabu walikuwa wakikusudia kuhiji kwa ajili ya kukutana, kujifaharisha, kutafuta mahitaji na kuhudhuria soko. Ndipo Mwenyezi Mungu akaamrisha Hijja iwe ni kwa makusudio yake Yeye kwa ibada safi yenye kutakasika na makusudio yoyote mengine.

Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana.

Yaani ikiwa mmeherimia Hijja, kisha mkazuilika kukamilisha ibada kwa njia yake ya kisheria kutokana na maradhi au adui na mengineyo, basi ni juu yenu kuchinja mnyama atakayepatikana kwa urahisi; kwa uchache awe ni mbuzi, wastani ni ng’ombe na wa juu zaidi ni ngamia.

Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao.

Msemo unaelekezwa kwa wale waliozuilika ambao hawakuweza kutimiza Hijja au Umra. Wao hawatakuwa wametoka katika ihram yao (miko ya Hijja) mpaka wajue kwamba mnyama amefika mahali pake pa kuchinjwa. Na mahali pa kuchinja ni Mina ikiwa ni Hijja; na kama ni Umra basi ni Makka. Hayo ni itakapokuwa kizuizi ni maradhi. Ama ikiwa kizuizi ni adui, basi mahali pa kuchinja ni pale mahali palipotokea kizuizi. Kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) alichinja mnyama katika Hudaybiya, alipozuiliwa na washirikina kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu (Al Ka’aba).

Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana adha kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnyama.

Yaani ikiwa mwenye kuhirimia atanyoa kichwa chake kwa dharura, basi ni juu yake kutoa kafara, atakuwa na hiyari baina ya kufunga siku tatu, kuwalisha masikini sitini au kuchinja mnyama; kwa uchache awe ni mbuzi.
Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha akahiji, achinje mnyama aliyemwepesi kupatikana.

Yaani mtu asiyekuwa na kizuizi, akafanya Umra kisha akahiji baadae katika mwaka huo huo, basi ni juu yake kuchinja mnyama. Hii ndiyo aina ya Hijja inayojulikana kwa jina la Haj Tamattui (Hijja ya starehe) ambayo ni wajibu kwa wasiokuwa watu wa Makka.

Imeitwa Hijja ya starehe, kwa sababu mwenye kuhiji baada ya kumaliza amali za Umra anatoka kwenye miko ya Umra mpaka aje ahirimie Hijja.

Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika Hijja na siku saba mtakaporudi:

hizo ni siku kumi kamili. Imam Jaffar Sadiq (a.s.) amesema; Mwenye kufanya Hajj Tamattu, asipopata mnyama atafunga siku tatu katika Hijja; siku ya saba, ya nane na ya tisa katika Dhul-Hijja (mfungu tatu) wala hakuna sharti la Iqama na siku saba atafunga atakaporudi kwa watu wake. Hizo ni siku kumi kamili za kutosheleza mnyama.

Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na msikiti mtakatifu.

Mwenye Majmaul Bayan amesema kuwa hayo yaliyotangulia kutajwa katika Tamattui ya Umra kisha Hijja, sio kwa watu wa Makka na walio karibu yake. Isipokuwa ni kwa ambaye hayuko Makka, yule ambaye yuko mbali na Makka kwa zaidi ya maili kumi na mbili (12) kwa kila upande.

Mafaqihi wa Kishia Imamiya wamesema Hajj Tamattui ni wajibu kwa walio mbali na Makka, wala haijuzu kwa aliyembali na Makka kuhiji Hijja Qiran na Ifrad, kwani hizo ni wajibu kwa watu wa Makka na wa kando kando yake; na wao haijuzu kwao kuhiji Hajj Tamattui. Kwa ufafanuzi zaidi angalia vitabu vya Fiqh.

Hijja ni miezi maalumu.

Nayo ni kuanzia Shawwal, Dhul-qaad na kumi la mwanzo la Dhul-Hijja. (mfunguo mosi, mfunguo pili na mfunguo tatu) Mwenye kuhirimia kabla yake Hijja yake haitaswihi na mwenye kuhirim- ia ndani ya miezi hiyo itaswihi na ataleta amali zilizobakia.

Na anayejilazimisha Hija katika miezi hiyo, basi hakuna kuchafua wala ufuska wala mabishano katika Hijja.

Makusudio ya uchafuzi hapa ni kujamii. Mtu akimjamii mkewe na huku amehirimia Hijja, basi Hijja yake imeharibika, sawa sawa na aliyejamii au kula huku akiwa amefunga. Kwa hiyo atakamilisha Hijja yake, kisha aje alipe mwaka ujao; kama ilivyo kwa mwenye kuiharibu Saumu. Makusudio ya ufuska, ni uongo na kutukana.

Ama kuhusu kubishana riwaya za Ahlul Bait zinasema, hilo ni kusema mtu; “Hapana wallahi au “Kwa nini, wallahi n.k.”

Si vibaya kwenu kutafuta riziki ya Mola wenu

Kwa vile wakati wa ujahilia watu walikuwa wakifanya biashara na kuchuma siku za Hijja, kukadhaniwa kuwa ni haramu, ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.), akaondoa tuhuma hii na akabainisha kwamba kuchuma hakupin- gani na ikhlasi katika amali za Hijja.

Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katika
Mash’aril-Haram.

Arafa ni mahali maalum. Kumiminika kutoka Arafa ni kuondoka, Mash’aril-Haram ndipo pale panajulikana kama Muzdalifa na kutua hapo ni wajibu; kama ilivyo kwa Arafa.

Kisha miminikeni kutoka mahali wamiminikapo watu (wote)

Inasemekana kuwa Maquraish walikuwa hawatui Arafa pamoja na watu wengine kwa kiburi tu, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kutua hapo na kutoka pamoja na watu ili abatilishe waliyokuwa wakiyafanya Maquraish.

Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu zaidi.

Imepokuwa kutoka kwa Imam Baqir baba wa Imam Sadiq (a.s.) kwamba watu walikuwa wanapomaliza Hijja wanakusanyika huko na kuwataja wazazi wao kwa fahari, ndipo Mwenyezi Mungu akawaamrisha kuliacha hilo na badala yake wamtaje Mwenyezi Mungu na jinsi alivyowaneemesha. Kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuwaneemesha wao na mababa zao.

Na baadhi ya watu kuna asemaye: Mola wetu! Tupe duniani; nao katika akhera hawana lolote. Na miongoni mwao kuna asemaye: Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera, na utulinde na adhabu ya moto. Hao ndio wenye fungu katika waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhisabu.

Watu katika Hijja zao wako aina mbili. Aina ya kwanza ni yule asiyetaka lolote isipokuwa starehe ya dunia na hana makusudio yoyote isipokuwa dunia tu, na anapomwabudu Mwenyezi Mungu humwabudu kwa ajili ya dunia.

Hawa ndio wenye kunyimwa neema ya Akhera. Ama aina ya pili ni yule anayetaka heri ya dunia na akhera na anafanya amali kwa ajili ya dunia yake na akhera yake. Huyu ndiye mwenye radhi mbele ya Mwenyezi Mungu kesho kwa kulipwa amali yake njema.

Mwenye Tafsiri Rawhul Bayan amenukuu kutoka kwa Imam Ali bin Abi Twalib (a.s.) kwamba wema katika dunia ni mwanamke mwema na katika akhera ni Hurulain. Ama adhabu ya moto makusudio yake ni mwanamke muovu.

Iwe ni sahih Hadith hiyo au la, lakini mimi najua kuna watu wanaohisi kwamba lau wao wangekuwa katika Jahanam kisha wakahiyarishwa kutoka katika Jahanam na warudi kwa wake zao waliokuwa nao duniani au wabaki Jahannam, basi wangelichagua kubaki katika Jahannam kuliko kuishi tena na wake zao hao.

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabiwa.

Makusudio yake ni siku tatu za Tashriq nazo ni; Tarehe kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu katika mwezi wa Dhul-Hijja (mfungo tatu).

Si wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina usiku wa kumi na tatu, lakini kwa sharti ya kuwa atoke Mina siku ya kumi na mbili baada ya kupinduka jua na kabla ya Maghrib na awe hakuvunja mwiko wa kuwinda au kujamii. Kwa hali hiyo ndipo tunapopata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake kwa mwenye takua.

Yaani mwenye kuacha kuwinda na wanawake katika ihram yake.

Ikiwa amevunja mwiko wa kulala na mke au kuwinda au alichelewa na jua siku ya kumi na mbili akiwa yuko Mina, basi itakuwa wajibu kwake kulala usiku wa kumi na tatu na kutupia mawe vikuta vitatu (shetani).

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ {204}


N


a


katik


awat


u


kuna


ambay


e


kaul


i


yak


e


inakupendez


a


katik


a


maish


a


ya


duniani


,


naye humshuhudiz


a


Mwenyezi


Mungu kwa yaliyo moyoni


mwak


e


n


a


hal


i


n


i


hasimu


mkubwakabisa.

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ {205}


N


a


anapotawal


a


hufanya


bidii katika ardhi kufanya


ufisadi


,


n


a


huangamiza mime


a


n


a


viumbe


,


na


Mwenyez


i


Mung


u


hapendi


ufisadi.

وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ {206}


N


a


anapoambiwa


.


Mche


Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya


dhambi


.


Bas


i


Jahannam


inamtosha, napo ni makao mabayamno.

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ {207}


Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi


y


a


Mwenyez


i


Mungu


,


na


Mwenyezi Mungu ni mpole kwawaja.