read

Aya 204-207: Kauli Zao Zinakupendeza

Maana

Baadhi ya wafasiri wapya wamejaza kurasa kwa maneno matamu katika kufasiri Aya hizi, lakini hawakuzidisha chochote zaidi ya kuwagawanya watu kwenye wema na uovu. Kwa dhahiri haya yanajulikana na wote, hayahitaji ubainifu wowote, sikwambii tafsiri ndefu tena.

Unaweza kuuliza; Ikiwa kugawanyika watu kunajulikana na wote, basi kubainisha kunakuwa ni maelezo ambayo tayari yameshaelezwa na kufafanua lililofafanuliwa na yapasa kuyachukulia maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) vizuri?

Jibu: Inawezekana kuwa makusudio ni kuongoza na kuelekeza kwamba mwenye akili anatakikana kutohadaliwa kwa mambo ya nje wala asimwamini mwenye kutegeneza maneno matamu. Kwa sababu wafisadi ni mabingwa wa kazi hiyo na kazi ya ria. Kwa hivyo ni juu yetu kutomtegemea yeyote isipokuwa baada ya kufanya majaribio na kupatikana dalili ya ukweli wake na usafi wake.

Hiyo ndiyo asili ya ujumla inayoenea katika hukumu nyingi za dini na za kidunia; kama kuchagua Hakimu, Kadhi, Naibu, Kadhi, Mufti na kila anayesimamia masilahi ya Umma.

Ajabu ya maajabu ni kutakiwa shahada ya kielimu tu kwa mwenye kujitokeza kwa kazi muhimu ya mji au nchi na inayogusa maisha ya watu. Lakini haulizwi uaminifu wake na tabia yake, pamoja na kuwa hayo ndio msingi. Wengi wenye shahada wanazitumia kuwa ni zana za kuibia.

Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza hapa duniani, naye humshuhudia Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali ni hasimu mkubwa kabisa. Yaani wanadhihihirisha mapenzi na heri na hali wao ndio maadui zaidi wa heri na watu wa heri.

Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi.

Wamehitaliafiana wafasiri kuhusu neno Tawalla. Je makusudio ni kuon- doka na maana yake kuwa ni, anapoondoka kwa yule aliyemdanganya, ‘huhangaika katika ardhi kwa ufisadi’. Au kwamba makusudio ni kutawala na usultani, na maana yawe, ‘na atakapokuwa mtawala atafanya wanayoyafanya watawala waovu ya kuangamiza mimea na viumbe?’

Mwenye Tafsir Al manar amenakili kutoka kwa Ustadha wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba ameyapa nguvu maana ya utawala kwa kuunganisha na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi." Kwa maana ya kuwa mtawala mkaidi anakuwa na kiburi kuongozwa kwenye maslahi au kupewa tahadhari ya mambo ya ufisadi, yeye hujiona yuko juu ya haki; kama vile alivyo juu ya watu wake anaowatawala, basi itawezekanaje kwa mtu kumwambia amwogope Mwenyezi Mungu.
Na huangamiza mimea na viumbe.

Mimea ni kilimo na viumbe ni wanyama. Makusudio ni maslahi yote ya kiuchumi katika kilimo, viwanda na ufugaji, mali ghafi, na mengineyo yanayohusika na uhai wa watu na maisha yao. Mwenyezi Mungu amehu- sisha kutaja kilimo na ufugaji kwa vile viwanda wakati huo havikuwa na umuhimu wowote kama ilivyo sasa.

Uharamu wa mambo hayo kwa mtazamo wa Uislamu ni sawa na uharamu wa kumwaga damu; na mwenye kukusudia ubaya katika vitu hivyo, ndio amekusudia ubaya wa utu hasa; hata kama vitu hivyo ni milki ya adui anayepiga vita Waislamu.

Mtume (s.a.w.w.) amekataza kukata miti, kuharibu mimea na majengo na kutia sumu miji ya washirikina siku za vita, n.k.

Lau tunailinganisha sharia ya Kiislamu na mambo yanayofanywa leo na dola za kikoloni na vita vyao vya silaha za kemikali kwenye mimea, watu na wanyama, na kuitia sumu anga kwa mabomu ya Atomic na kuyatupa kwa wanawake na watoto, lau hayo yote tunayaunganisha na Uislamu, basi tutajua huruma, uadilifu na utu wa Uislamu na unyama wa dola za Magharibi na jinsi zilivyopetuka mipaka katika dhulma na unyang'anyi.

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hapendi ufisadi.

Hakuna uharibifu mkubwa zaidi kuliko kuzusha vita na kutumia silaha zenye kubomoa ili kuwatawala watu na kuwanyang'anya chakula na matunda ya jasho lao.

Na anapoambiwa mche Mwenyezi Mungu hupandwa na mori wa kufanya dhambi.

Mtu mwema wenye ikhlasi anakubali masahihisho na nasaha, bali huzitafuta na kuzikaribisha, kwa sababu yeye hana lengo jengine zaidi ya haki, wala hatafuti sifa; kwa sababu amali yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) sio umashuhuri.

Imam Amirul Muminin (a.s.) anasema katika maneno anayowasifu wanaomcha Mwenyezi Mungu: "Hawaridhii na amali zao chache wala hawakioni kingi kilicho kingi; wao wanajituhumu na wao ni wenye kunyenyekea katika amali zao."

Katika hotuba yake siku za ukhalifa wake alisema.

"Mtu hata kama ana cheo kikubwa katika haki na fadhila kubwa katika dini hawezi kuwa hahitajii kusaidiwa katika aliyobebeshwa na Mungu katika haki zake; wala si mwenye kutaka kujitukuza; wala mtu hata kama nafsi zinamfanya mdogo na kudharauliwa na macho sio kuwa hawezi kusaidia au kusaidiwa...Wala msinidhanie kuwa mimi ni mzito katika haki nitakayoambiwa, kwani mwenye kuifanya nzito haki atakayoambiwa au uadilifu atakaoonyeshwa, basi kwake kuitumia haki na uadilifu ni kuzito zaidi."

Hivyo ndivyo anavyotakikana mwanachuoni mwenye ikhlasi ya kweli. Ama mnafiki mwenye hiana, haki inakuwa nzito juu yake kwa sababu itamfedhehesha; na hununua sifa kwa thamani kubwa ili azibe upungufu wake na uovu wake.

Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu.

Yaani baadhi ya waumini wanaikabili Jihadi na wanapenda mauti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. sawa na wale wengine wanaopenda uhai. Hawana lengo jengine isipokuwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu Zake.

Razi katika kutafsiri Aya hii anasema kuhusu sababu za kushuka kwake kuwa kuna riwaya tatu; Mojawapo ni kwamba Aya hii imeshuka kwa sababu ya Ali bin Abi Twalib (a.s.) alipolala kwenye kitanda cha Mtume wakati wa Hijra, alisimama Jibril kichwani mwake, Mikail miguuni mwake na Jibril: Pongezi! Pongezi! ewe Ali akisema: Mwenyezi Mungu anajionea fahari kwako, mbele ya Malalika.1

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ {208}


Eny


i


mlioamini


!


Ingieni katik


a


usalam


a


nyote, wal


a


msifuat


e


nyay


o


za


Shetani. Kwa hakikayeye kwenuni aduiwawazi.

فَإِنْ زَلَلْتُمْ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {209}


Nakamamkitelezabaadaya kuwafikia ubainifu, basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenyenguvu,Mwenyehekima.

هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا أَنْ يَأْتِيَهُمُ اللَّهُ فِي ظُلَلٍ مِنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ {210}


Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya


mawing


u


n


a


Malaika


,


na


liish


e


jambo


;


n


a


mambo


yote hurudishwa kwa


Mwenyez


iMungu.

  • 1. Sheikh Mudhaffar katika kitabu Dalailu Swidq J2 anasema; “Wale ambao wamenakili kuwa Aya hii imeshuka kwa haki ya Ali, ni Razi, Thaalabi na mwenye Yanabiul-Mawadda, Abu Sadak katika Fadhail itrati twahira, Ghazali katika Ihyai, Hakim katika Mustadrak na Ahmad bin Hanbal katika Musnad. Zaidi ya hizo kuna riwa nyingine zilizopokewa kwa upande wa shia.