read

Aya 208-210: Ingieni Katika Usalama Nyote

Maana

Enyi Mlioamini! Ingieni katika usalama nyote.

Imesemekana kuwa makusudio ya neno Silmi hapa ni Uislamu, na kwamba msemo unawaelekea wanafiki ambao wameificha kufuru na kudhihirisha Uislamu. Na imesemekana kuwa msemo unawaelekea wenye kumwamini Mwenyezi Mungu katika Ahlul Kitab ambao hawakusilimu. Na ikasemekana kuwa unawaelekea Waislamu wote kwa hivyo maana yake yanakuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea katika hukumu Zake zote sio baadhi. Na pia imesemekana maana yake ni suluhu kwa maana kuwa ingieni katika suluhu nyote.

Tuonavyo sisi ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemwamrisha mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu, kwa imani sahihi kuingia katika lile ambalo lina salama yake ya dunia na akhera. Na njia ya usalama inajulikana na wote, nayo ni kusaidiana, kuungana, na kuacha vita na uhasama. Vile vile kuyashinda matamanio na kuwa na ikhlasi katika kauli na vitendo.

Makusudio ya maana hayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:‘Wala msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni aduiwa wazi, Aliyoileta mara tu, baada ya kusema. ‘Ingieni katika usalama nyote’.

Hapo Mwenyezi Mungu amezingatia kuwa nyayo za shetani kinyume chake ni usalama; na amemweka mtu mbele ya mambo mawili tu, hakuna la tatu; Ama kuingia katika usalama au kufuata nyayo za shetani ambazo ndio dhati ya uovu, ugomvi, shari na ufisadi.

Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuingia katika usalama na kukataza kufuatwa nyayo za shetani, amemhadharisha yule atakayehalifu amri yake na makatazo yake na akatishia kwa kusema: "Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima."
Mwenye nguvu, hashindwi katika amri Yake wala hakimzuwii chochote kwa alilokusudia kulifanya. Mwenye hekima, humlipa mema mtiifu na humwadhibu mwasi.

Razi anasema: "Huo ndio ukomo wa kiaga kwa sababu ni kuhofisha bila ya kutaja adhabu. Huenda mzazi akamwambia mtoto wake: "Ukiniasi basi wewe wanijua na wajua uwezo wangu kwako", basi maneno hayo yanakuwa ni makemeo ya ufasaha zaidi kuliko kutaja kipigo na mengineyo.

Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivuli vya mawingu na Malaika.

Maana kwa ujumla ni kwamba wale wenye kukadhibisha na wakaasi watajiwa na adhabu kwa ghafla wala hawataokoka. Aya iko katika mwelekeo wa Aya inayosema:

فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً ۖ {18}


"NahawangojiilasaayaKiyamakiwajiekwaghafla...?"(47:1


8


).

Na lishe jambo; na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu.

Mauti ambayo hapana budi nayo, yakija na Kiyama kikija, kila kitu kitakuwa kimekwisha na hapatabakia mbele ya wenye makosa isipokuwa hisabu na mateso.

Siri Na Matukio Ya Ghafla

Hakuna yeyote ajuaye yatakayomtokea mbele na siri ya wakati, heri au shari. Hawezi kuyajua hayo vyovyote atakavyokuwa na elimu au imani: "Na nafsi yoyote haijui itachuma nini kesho." (31:34)

Mara nyingi mtu hujiwa na heri kwa ghafla wakati yeye anatazamia kupata shari; na hujiwa ghafla na shari wakati anapotazamia heri. Hakuna kitu kinachotia uchungu kama hicho cha kupata shari wakati wa kutazamia heri; kama vile ambavyo hakuna kitu kitamu kama kupata heri wakati wa kutazamia shari.

Mwenye akili hawezi kughurika na alivyo navyo, bali hufikiria mzunguko wa zama; kama vile ambavyo hakati tamaa na lolote linalompata; kwani dunia inageuka milele; ndio maana ikasemwa; "Kudumu hali ni muhali na faraja inakuja kutokana na dhiki." Imam Ali (a.s.) anasema: "Baada ya dhiki ni faraja.

Anaendelea kusema Imam: "Hakika Musa bin Imran alitoka kuwatafutia watu wake moto akasemeshwa na Mwenyezi Mungu na akarudi akiwa Mtume." Mwenyezi Mungu anasema:

إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ {87}


"...Hawakati tamaa ya rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri."(12:87).

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ {99}

Na amesema tena:


Hawajiaminishina mipango ya MwenyeziMungu ilawatuwenyehasara."(7:99).

Imeelezwa katika vitabu vya Historia na Sera kwamba Ibn Ziyat alikuwa waziri na mtu wa kutegemewa na Mu'utasim, naye alikuwa ni katika mataghuti wa hali ya juu na dhalimu mkubwa. Alitengeneza tanuri la chuma alilolijaza misumari yenye ncha pambizoni mwake.

Anapomkasirikia mtu humtupa ndani, kila anavyojitingisha ndivyo misumari inavyomwingia mwilini mwake. Mutawakkil alipotawala alimshika Ibn Ziyat na akamfunga kwa chuma mikononi mwake na miguuni mwake kisha akamtupa katika tanuri hilo, na baadaye akafa. Kabla ya kufa alisikika akiimba shairi hili: Sifazake tulia, hebu nenda pole pole, Kigeugeu dunia, huenda nyuma na mbele.

سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُمْ مِنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَنْ يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ {211}


Waulize wana wa Israil, isharangapizilizowazitulizowapa? Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu


baad


a


y


a


kumfikia


,


basi


hakikaMwenyeziMungu ni Mkaliwakuadhibu.

زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ {212}


W


amepambiwa makafiri maisha ya duniani, na wanawafanyia maskhara


wal


e


walioamini


.


N


a


wale


weny


e


taku


a


watakuw


a


juu


ya


o


Sik


u


y


a


Kiyama


.


Na


Mwenyezi Mungu hum


ruzuk


u


amtakay


e


bil


a


hisabu.