read

Aya 211-212: Waulize Wana Wa Israil

Maana

Waulize wana wa Israil, ishara ngapi zilizo wazi tulizowapa?

Makusudio ya waulize hapa sio swali hasa la kihakika, kwa sababu Mtume (s.a.w.) anajua hali zao, wala makusudio sio kuelezea hali waliyokuwa nayo; kama ilivyo katika Aya ya 49 na inayofuatia. Isipokuwa makusudio hasa ni kuwa Waislamu wazingatie na wapate funzo na hali ya Waisrail.

Njia ya kupata funzo ni kuwa Waisrail walijiwa na Mtume Musa (as)kwa miujiza na hoja ambayo ni mkono kuwa mweupe, fimbo kugeuka nyoka na kupasuka bahari.

Vile vile kufunikwa na wingu, kuteremshiwa Manna na Salwa na jabali kutoka maji. Pamoja na hayo yote waliasi na kukhalifu, ndipo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa madhila na utwevu katika dunia na adhabu iumizayo katika Akhera.

Na Waislamu nao wamejiwa na Muhammad (s.a.w.w.) kwa miujiza na hoja zinazofahamisha ukweli wa Utume wake na kuswihi sharia yake; naye akawafikilizia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa waaingie katika Uislamu wote, kwani humo watapata heri na utengeneo wao; kama wakiasi kama walivyofanya Waisrail, basi yatawapata yaliyowapata Waisrail.

Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Makusudio ya neema hapa ni dalili za haki, kwani hizo ni katika neema kubwa. Kwa sababu ndani yake mna uongofu na kuokoka na kuhiliki na upotevu. Makusudio ya kuzibadilisha ni kuziasi na kuziharibu. Kwa hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia” ni sawa na kauli yake: "Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu..." (2:209).

Vile vile kusema kwake: "Basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" ni sawa na kusema:

أَنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {209}


“Kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenyehekima." (2:209)

Maana ni moja na lengo ni moja.

Hapana Imani Bila Takua (Ucha Mungu)

Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani.

Hapana tofauti kati ya mwenye kukanusha kuwapo Mwenyezi Mungu na yule mwenye kuamini kinadharia tu, lakini matendo yakawa ni tofauti. Hapana tofauti kati ya wawili hao.

Kwa sababu kila mmoja ameathiriwa na dunia na vipambo vyake, ameathirika na kitu cha sasa hivi kuliko cha muda ujao; heri na manufaa ameyapima kwa kiwango cha manufaa yake, wala hakupima na mambo aliyoharamisha Mwenyezi Mungu wala na msimamo wa kibinadamu.

Mimi kila ninavyozidi kuzama katika tafsiri ya Qur'an na kuangalia kwa undani Aya zake, basi huwa na yakini zaidi kwamba imani bila ya ucha Mungu haina maana yoyote; na kwamba kila anayeiangalia dunia kuwa ndio makusudio yake yote, basi atakuwa ameiweka mbali sharia ya haki na dini, atake asitake.

Imekuja Hadith Mutawatir kutoka kwa Mtume Mtukufu akisema: "Dunia na akhera zina madhara" yaani zinadhuriana kuhujumu moja yao nikuiacha nyingine. 1

Imam Ali (a.s.) anasema: "Hakika dunia na Akhera ni maadui wawili wanaotofautiana, na ni njia mbili tofauti. Mwenye kuipenda dunia ataichukia akhera na kuwa adui yake; zote mbili ni kama Mashariki na Magharibi, mwenye kutembea kati yao huwa mbali na nyingine kila anapokaribia moja wapo."

Na wanawafanyia maskhara wale walioamini.

Ni kawaida wale wanaozichezea Hoja za Mwenyezi Mungu na hukumu zake wakihalalisha damu na mali ya haramu kuwadharau na kuwachezea wale wanaojilinda na maharamisho na kuvumilia tabu na mashaka kwa ajili ya kumridhisha Mungu.

Na wale wenye takua watakuwa juu yao siku ya Kiyama.

Amesema wenye takua wala hakusema wale walioamini, kwa sababu imani bila takua si lolote; kama tulivyobainisha. Maana yako wazi ni kuwa makafiri wakiwadharau waumini hivi sasa, basi mambo yatabadilika kesho. Mwenyezi Mungu anasema:

قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ {27}


"...Hakikahizayanaubayaleoitawafikamakafiri."(16:27).

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ {34}


"Basileowaleambaowameaminiwanawacheka makafiri."(83:34)

Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hisabu.

Riziki ni mbili ya dunia na riziki ya Akhera. Riziki ya dunia inajulikana na riziki ya Akhera, ni neema isiyokatika na isiyokuwa na chembe ya huzuni au hofu. hataipata yeyote isipokuwa kwa imani na amali njema: Anasema Mwenyezi Mungu:

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {82}


"Nawale walioamini na kutenda mema, hao ndio watuwa Peponi, humo watakaamilele."(2:82).

Kila mtu anaweza kupata riziki duniani, awe ni kafiri au Mumin, mwema au mwovu, na anayehangaika au asiyehan-gaika; kama vile urithi, zawadi, wasiya, n.k. Vile vile inaweza kupatikana kwa njia ya halali, au haramu, kama vile kunyang'anya, kughushi na utapeli.
Mwenye Tafsir Al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba, amesema wakati wa kutafsiri Aya hii, kwamba riziki bila ya kuhangaika inaweza ikapatikana kwa baadhi ya watu. Ama kwa Umma ni muhali kujitosheleza isipoku-wa kwa kuhangaika na kufanya kazi. Huo ni ukweli ulio wazi kabisa.

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ وَأَنْزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّهُ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ {213}


W


atuwotewalikuwawamila moja. Basi Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii watoao bishara na waonyao. Na pamoja nao akawateremshia kitabu kinachoshikamana na haki ili kihukumu baina ya watu katika yalewaliohitilafiana. Na hawakuhitilafiana katika hayo ila wale waliopewa Kitabu, baada ya kuwafikia ubainifu,kwasababuyauhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongozakwenyehakiwalioaminikatikayalewaliyohitilafiana kwa idhini yake. Na MwenyeziMungu humwongoza amtakayekwenyenjia iliyonyooka.

  • 1. Kuna Hadith nyingine inayosema: “Si mbora wenu yule mwenye kuacha dunia kwa akhera, wala akhera kwa dunia lakini mbora wenu ni yule atakayechukua hii na hii . Mumin mwenye nguvu ni bora kuliko dhaifu.”.