read

Aya 213: Watu Wote Walikuwa Mila Moja

Lugha

Mwenyezi Mungu amelitumia tamko Umma katika kitabu chake, kwa maana nyingi, kama vile Mila Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika mila yenu hii ni mila moja." (21:92)

Au kwa maana ya kundi - Mwenyezi Mungu anasema:

وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ {181}


"Nakatikawaletuliowaumbawakowatuwanaoongoza kwahakitu... (7:181).

Pia limekuja kwa maana ya muda; kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَعْدُودَةٍ{8}


"Nakamatukiwachelewesheaadhabumpakamuda uliokwishahisabiwa..."(


1


1:8).

Vile vile kwa maana ya Imam anayefuatwa - Mwenyezi Mungu anasema:

إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِلَّهِ {120}


"HakikaIbrahimalikuwamfano (wa kufuatwa) mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mung


."(16:120).

Ama makusudio ya neno Umma katika Aya hii tunayoifasiri, ni mila.

Maana

Kauli za wafasiri zimegongana katika kuelezea maana ya aya hii. Razi ameifafanua kwa kiasi cha kurasa saba. Ama mwenye Tafsir Al - Manar ameifaf-anua kwa kurasa ishirini na mbili na kumwacha msomaji wa kawaida patupu, bila ya kuambua chochote.

Na sisi, kama kawaida yetu, tumo katika njia yetu ya kumfanyia wepesi yule msomaji wa kawaida, kwa kiasi kile kitakachoafikiana naye.

Kwa hivyo ufafanuzi wake ni kwa uwazi na ufupi, ili aweze kuangalia vizuri Aya za Mwenyezi Mungu kwa wepesi na kuathirika nafsi yake. kama kunakuwa na maudhui muhimu, tunayaeleza katika kifungu cha peke yake.

Watu wote walikuwa mila moja.

Yaani walikuwa wa umbile ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia watu na ambalo Mtume (s.a.w.w.) ameliashiria kwa kusema: "Kila anayezaliwa huzaliwa kwenye fitra (umbile la usawa)." Mwenye Majmaul Bayan anasema: "Masahaba wetu wamepokea kutoka kwa Imam Abu Jaffar al
Baqir, kwamba kabla ya Nuh1 watu walikuwa mila moja ya umbile alilowaumba Mwenyezi Mungu - si wenye kuongoka wala kupotea; Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume. Kwa hivyo maana yake ni kwamba wao walikuwa ni wenye kuabudu kulingana na akili zao bila ya uongofu wa Mitume wala sharia."

Kisha wakajiliwa na mawazo na fikra ambazo ziliwapeleka katika tofauti ya itikadi na rai, hatimaye kwenye uadui. Kwa hivyo wakagawanyika vikundi vikundi baada ya kuwa ni wa mila moja. Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume na kitabu kinachosema kweli na kinachohukumu mizozo yao. Haya ndiyo maana yaliyo wazi ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Basi Mwenyezi Mungu akawaleta Manabii watoao bishara na waonyao.

Na pamoja nao akawateremshia kitabu kilichoshikamana na haki ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitalifiana.”

Hapa inatubainikia kwamba katika maneno kuna jumla iliyokadiriwa ambayo ni : "Watu walikuwa wa mila moja kisha wakahitalifiana”

Linalofahamisha hilo ni kauli inayosema: "Ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitalifiana." Na hilo linatiliwa nguvu na kauli hii:

وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ {19}


"Na watu hawakuwa isipokuwa wamila moja; kisha wakahitalifiana..."(10:19).

Na hawakuhitilafiana katika hayo ila waliopewa kitabu, baada ya kuwafikia ubainifu, kwa sababu ya uhasidi baina yao.

Yaani: Watu ambao walikuwa ni umma mmoja, kisha wakahitalifaina na Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume, watu hao pia walihitalifiana katika Mtume alieyepelekwa; wengine waliamini na kusadiki na wengine wakakufuru na kukadhibisha baada ya kusimama hoja na dalili wazi za mkato. Hakuna sababu yoyote ya kukadhibisha huku isipokuwa uhasidi na kuhofia manufaa yao ya kibinafsi na uadui.

Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongoza kwenye haki walioamini katika yale waliyohitalifana kwa idhini yake.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewafikisha wenye nia njema kwenye imani ya haki aliyokuja nayo Mtume; na imani hiyo ni kwa amri yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Kwa hiyo makusudio ya idhini ni amri.

Na Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.

Katika kufasiri Aya ya 26 ya Sura hii kifungu cha uongofu na upotevu, tumetaja maana ya uongofu ambayo miongoni mwake ni: Kukubali mtu nasaha na kuzitumia; na hayo ndiyo makusudio yake hapa. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawaafikisha watu wema kukubali nasaha na kufanya vitendo vya haki na heri.

Tofauti Kati Ya Watu

Kulipatikana kutofautiana kati ya watu tangu Qabil alipomuua nduguye Habil; kunaendelea hadi leo na kutabaki hadi siku ya mwisho. Kutofautiana hakuhusiki na watu wa dini tu; kama wanavyodai wasiojua hakika ya mambo. Kwani tunaona kutofautiana kusikokuwa kwa dini kumefikia kugeuka maneno na kuwa vita vya kumalizana. Ugomvi kati ya dola za kibepari kumepelekea vita vya Atomic. Bomu lilitupwa Hiroshima kwa wanawake na watoto na dola ya kibepari dhidi ya dola nyingine ya kiberi pia.

Na kugawanyika mwelekeo kwa dola za kijamaa kunaeleweka. Vile vile dola za Kiafrika na Kiesia zinatofautiana kulingana na upande wa wanyonyaji wanaozinyonya. Ama kutofautiana kwa dola za Kiarabu matokeo yake ni kupatikana Israil ndani ya nchi yao na hatimaye kusalimu amri mnamo tarehe 5 June, 1967.

Hali yoyote iwayo, kutofautiana kuna sababu nyingi, kama vile: Kutofautiana katika malezi na maendeleo, katika tabia na akili na kutofautiana kunakotokana na mgongano wa masilahi na manufaa ya kiutu.

Tofauti inayotokana na maendeleo, akili na tabia inaweza kurekebishwa kwa kufanya yale yanayoafiki misingi iliyothibitishwa na elimu na majaribio. Lakini tofauti zinazotokana na kugongana kwa manufaa ya kiutu hazina dawa isipokuwa kumzuwia adui kwa nguvu.

Maelezo yetu haya, ni kukamilisha tuliyoyasema katika kufasiri Aya ya 113 kifungu cha "Kila mmoja anavutia dini yake."

أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ ۖ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ {214}


A


umnadhan


ikuw


amtaingia Pepon


in


ahal


ihamjajiw


ana


mfano wa wale waliopita kabla yenu?


Y


aliwapata mashaka na madhara, na


wakasukwasukw


a


hat


a


akase


ma Mtume na walioamini pamoja naye: Nusura ya


Mwenyez


i


Mung


u


itafik


a


lini?


Jueni kuwa nusura ya


Mwenyez


iMung


uik


okaribu.

  • 1. Imeelezwa katika Tafsiri Rawhul-bayan kwamba baina ya Adam na kupewa Utume Nuh kuna kiasi cha miaka themanini (80)