read

Aya 214: Kuingia Peponi

Maana

Au mnadhani kuwa mtaingia peponi na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara.

Hakika Aya hii tukufu inamwelekea kila mwenye kuamini haki, akaitumia na akailingania. Inasema waziwazi kwamba desturi ya Mwenyezi Mungu kwa wanaoinusuru haki, ni kuitolea thamani yake wao wenyewe, watu wao na hata mali zao.

Vile vile kuvumilia adha na kuwa na subira juu ya masaibu na shida. Waliokuwa kabla yenu walipambana na aina za maudhi wakasubiri; Je, nanyi mtasubiri kama walivyosubiri? Au nyinyi mnataka kuingia peponi bila ya kuilipia thamani. Na mwenye pepo hiyo amekataa isipokuwa thamani yake iwe ni imani, ikhlas na kuvumilia hofu, njaa na upungufu wa mali na nafsi!

Yamekuja maelezo katika khutba mojawapo ya Nahjul Balagha: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)alikuwa akisema: ‘Hakika pepo imezungukwa na machukivu na moto umezungukwa na anasa; na jueni kuwa hakuna katika twaa ya Mwenyezi Mungu isipokuwa huwa machukivu na hakuna katika maasi ya Mwenyezi Mungu isipokuwa anasa.’"

Kwa faida zaidi ni vizuri msomaji arudie tuliyoyataja katika kufasiri Aya ya 155 kifungu 'Thamani ya pepo.'
Na wakasukwasukwa hata akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini?

Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini, ni swali kutoka kwa Mtume na waumini, linaloleta picha ya misukosuko na shida walizozipata kutoka kwa maadui wa haki na makundi ya batili

Maana kwa ujumla ni kwamba walionusuru haki, waliotangulia, walipatwa na shida na wakaingia katika misukosuko mpaka wakadhani kwamba nusura imechelewa, hivyo wakaitaka ije haraka kwa kusema: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini? Mwenyezi Mungu naye akawajibu kwa kusema:

Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu.

Aya hii iko katika mwelekeo wa Aya isemayo:

حَتَّىٰ إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ ۖ {110}


"HataMitume walipokata tamaa, wakadhani ya kwamba wamekadhibishwa,msaadawetuuliwajia..."(12:


1


10)

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنْفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ {215}


W


anakuuliza watoe nini?


Sema


:


Kher


i


yoyote


mtakayotoani kwaajiliya wazazi wawilina akraba na mayatima na masikini na mwananjia.Nakheriyoyote


mnaoufany


a


Mwenyezi


Munguanaujua.