read

Aya 215: Watoe Nini?

Maana

Wanakuuliza watoe nini?

Msemo unaelekezwa kwa Mtume (s.a.w.w.).

Sema: Kheri yoyote mtakayotoa ni kwa ajili ya wazazi na akraba na mayatima na masikini na mwananjia. Makusudio ya neno kheri hapa ni mali.

Wazazi wawili ni baba, mama, babu na bibi, kwa sababu wao wanaingia katika jina la wazazi wawili. Ndugu ni akraba wa karibu wa mtoaji, yatima ni asiyekuwa na baba na mwana njia ni yule aliyeishiwa njiani na kushindwa kufika kwa watu wake na wala hana chakula.

Unaweza kuuliza kuwa dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa watu waliuliza aina ya kitakachotolewa sio nani wa kumpa. Na jibu ni la matumizi sio la aina, sasa je, imekuwaje?

Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya jawabu ni kumzindua muulizaji kwamba yeye anatakikana kuuliza nani wa kumpa, sio nini atoe. Razi amemnakili Qafal kwa jibu jingine; nalo nikuwa hata kama swali liko kwa tamko la Ma (nini) lakini kilichoulizwa ni nani wa kumpa sio cha kutoa, kwa sababu cha kutoa kinajulikana.

Sheikh Muhammad Abduh ameyatilia mkazo hayo kwa kauli yake: "wasomi wa fani ya mantiki ndio waliosema, swali la Ma linahusika na aina na jinsi..."

Lakini waarabu wanatumia kwa aina. Qur'an haiko katika mfumo wa Aristotle na mantiki yake, isipokuwa iko katika mfumo wa lugha ya Kiarabu ulio waziwazi. Jibu hili lina nguvu kuliko la kwanza ingawaje natija ni moja.

Swali la pili: “Je kuwapa waliotajwa katika Aya hii, ni wajibu au sunna? Jibu: Ni wajibu kwa wazazi kuwalisha watoto, na watoto kuwalisha wazazi ikiwa upande mmoja una uwezo na mwengine hauna uwezo wa kujilisha wenyewe. Kutoa huku hakuhisabiwi kuwa ni zaka. Ama mayatima na wasafiri, inajuzu kuwapa kutokana na zaka ya wajibu; kama vile ambavyo inajuzu kuwapa wote sadaka ya sunna.

Na sadaka ya suna hupewa kila mwenye kuhitajia, awe Mwislamu au si Mwislamu, kwa sababu kuna malipo katika kumnywesha kila mwenye ini la joto (kiu); kama ilivyoelezwa katika Hadith.

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ {216}


Mmeandikiw


a


kupigana


(vita


)


nal


o


n


i


(jambo


)


la


kuchukiza kwenu. Na huenda mkachukiakitu nacho ni


kher


i


kwenu


,


n


a


huenda


mkapend


a


kit


u


nach


o


ni


sharikwenu. NaMwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِنْدَ اللَّهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَنْ يَرْتَدِدْ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {217}


Wanakuuliza juu yakupi


gan


a


(vita


)


katik


a


mwezi


mtakatifu. Sema: Kupigana vita katika (miezi) hiyo ni


(dhambi


)


kubwa


.


Na kuzuili


a


wat


u


n


a


nji


a


ya Mwenyez


i


Mung


u


na


kumkufuru na (kuwazuilia) MsikitiMtakatifunakuwa


to


a


hum


o


wenyew


e


ni kukubw


a


zaid


i


mbel


e


ya


MwenyeziMungu. Na fitina ni kubwa zaidi kuliko kuua. Wala hawataachakupigana nanyi mpaka wawatoe katika diniyenu,kama waki


weza


.


N


a


yeyot


e


katika nyiny


i


atakayertadi


,


kisha


akafa hali ya kuwa kafiri, basi hao zimepomoka amali zaodunianina akhera.Na haondio watuwa motoni, humowatakaamilele.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّهِ ۚ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ {218}Hakika walewalioaminina


wal


e


walioham


a


na


wakafanya jihadi katika njia


y


a


Mwenyez


i


Mungu


,


hao


ndio wenye kutaraji


r


ehema


y


a


Mwenyez


i


Mung


u


na Mwenyez


i


Mung


u


ni


Mwenyekughufiria,Mwenye ku


r


ehemu.