read

Aya 216-218: Mmeandikiwa Kupigana Vita

Maana

Mmeandikiwa kupigana vita.

Mmeandikiwa hapa ni kwa maana ya mmewajibishiwa zilivyo Aya kadhaa zenye neno hilo. Mwenyezi Mungu amewajibisha vita kwa Waislamu si kwa kuwa vita vinapendeza au vinatakiwa mara kwa mara. Pia si kwa ajili ya kupanua nchi na kutawala au kunyonya mataifa mengine, isipokuwa au Mwenyezi Mungu amewajibishia kwa ajili ya kuinusuru na kuitetea haki.

Kwa sababu haki pekee, ni fikra na nadharia tu. Ama kuifuatilia na kulazimiana nayo kunahitaji kazi ngumu, ambayo kwanza ni kuilingania kwa hekima na kwa njia iliyozoeleka. Kama haikuwezekana, basi ni wajibu kuitekeleza haki kwa nguvu. Nadharia yoyote isiyotegemea nguvu za kiutekelezaji, basi kuwepo kwake na kutokuwepo ni sawa.

Ni kwa ajili hii ndipo Mwenyezi Mungu akawajibisha, katika Aya hii na nyinginezo, kupigana jihadi na kila adui wa haki, ikiwa hakuna faida kwake kumwamrisha mema na mawaidha mazuri. Lau si nguvu za kiutekelezaji, basi nguvu za kisheria zingekuwa ni maneno yanayosemwa mdomoni na kuandikwa tu.
Nalo ni (jambo) la kuchukiza kwenu. Na huenda mkachukia kitu nacho ni heri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamujui.

Wafasiri wanasema kwamba masahaba wa Mtume walichukia vita, kwa sababu ni tabia ya mwanaadamu kuona uzito kujiingiza katika jambo litakalomwangamiza. Lakini wakati huo huo wanaitikia amri ya Mwenyezi Mungu kwa kutaka radhi Yake; sawa na mgonjwa anayekunywa dawa kwa kutaka kupona. Na Mwenyezi Mungu akawazindua kwa kauli yake: "Huenda mkachukia kitu nacho ni heri kwenu" kwamba matunda ya vita na jihadi yanawarudia wenyewe na sio Mwenyezi Mungu.

Huu ndio ufupi wa waliyoyasema wafasiri. Na dhahiri ya Matamshi inakubaliana nayo, lakini tukiwaangalia masahaba wenye ikhlasi na ushujaa katika jihadi, kujitolea kwao kwa ajili ya dini na jinsi dini ilivyotawala hisia zao.

Vile vile jinsi walivyopuuza uhai kwa kutaka kufa mashahidi mpaka ikawa anayeokoka vitani na kurudi salama anajiona ni mwovu tukiangalia yote haya na kuyatia akilini mwetu, wakati wa kufasiri Aya hii, tutaona kuwa, haielekei kwa masahaba kuchukia vita, na kwamba hapana budi kufasiri Aya kwa maana nyingine itakayochukuana na matamko.

Kwa ufupi maana ni kuwa masahaba walikuwa wakiogopa kuwa Uislamu utamalizwa na washirikina kutokana na idadi yao kuwa kubwa na ya Waislamu kuwa ndogo; kwamba wao wataangamia kusibakie atakayeunusuru Uislamu, na mwito wa Kiislamu uende bure.

Kwa hiyo walikuwa wakihofia Uislamu, sio nafsi. Ndipo Mwenyezi Mungu akawabainishia kuwa vita mnavyoitiwa na kuvichukia ni bora kwenu na kwa ajili ya Uislamu, na kwamba kukaa tu, kutapelekea kumalizwa nyinyi na Uislamu; na nyinyi hamjui hakika hii, lakini

Mwenyezi Mungu anajua, kwa sababu kwake halijifichi lolote. Aya iko katika mwelekeo wa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Ewe Mtume! Wahimize walioamini waende vitani. wakipatikana kwenu watu ishirini wanaosubiri watawashinda mia mbili. Na kama wakiwa watu mia moja kwenu watawashinda elfu moja ya wale waliokufuru, maana wao ni watu wasiofahamu." (8:65)

Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana (vita) katika (miezi) hiyo ni dhambi kubwa.

Yamekwishapita maelezo katika kufasiri Aya ya 192 na inayofuatia hiyo.

Na kuzuilia watu na njia ya Mwenyezi Mungu na kumkufuru na (kuwazuilia) msikiti mtakatifu na kuwatoa humo wenyewe ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Waarabu walikuwa wakijizuilia kupigana katika miezi mitukufu ambayo ni Dhul-Qaada, Dhul-Hijja, Muharram na Rajab (mfunguo pili, mfunguo tatu, mfunguo nne na mfunguo kumi). Mtume naye akaithibitisha ada hii, kwa sababu inapunguza shari na umwagikaji damu. Kwa ujumla Uislamu umethibitisha kila ada nzuri au isiyokuwa mbaya iliyokuwa wakati wa Jahilia.

Hata hivyo Waarabu waliokuwa wakiitukuza na kuitakasa miezi hii, walivunja miiko yake na wakatangaza kupigana vita na Mtume katika mwaka wa sita Hijriya; wakamzuwia pamoja na masahaba zake kuzuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kumfitini mwenye kusilimu; wakawa wanamwadhibu kwa aina aina ya adhabu kwa muda wa miaka kumi na tatu; kama walivyofanya kwa Bilal, Suhaib, Khabbab na Ammar bin Yasir pamoja na baba yake na mama yake.

Lakini Waislamu wanapotaka kujikinga au kulipiza kisasi kwa washirikina, basi washirikina huanza kupiga mayowe kwa propaganda za upotevu, kwamba Waislamu wamevunja miko. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawabainishia kuwa makosa waliyoyafanya wao kwa Waislamu ni makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kupigana katika miezi mitukufu. Na kwa ajili hii Waislamu wamehalalishiwa kupigana na washirikina mahali popote na wakati wowote watakapowapata kwa kuchukua kisasi.
Na fitina ni kubwa zaidi kuliko kuua.

Yaani kuwafitini Waislamu na dini yao, mara nyingine kwa kuwaadhibu na mara nyingine kujaribu kuwatia shaka katika nyoyo zao, ni mbaya zaidi kuliko kupigana katika miezi mitukufu.

Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika dini yenu, kama wakiweza.

Lengo la washirikina ni kutobakia athari yoyote ya Uislamu duniani. Na ni kwa ajili hii tu, ndio wanapigana na Waislamu, na wanaendelea kupi- gana nao.
Basi kama Waislamu wakichukia kupigana na washirikina, lengo la maadui litatimia.

Roho hii ya kikafiri ya kiadui, inaendelea mpaka leo popote pale penye harufu ya Uislamu; inaendelea katika nafsi za wengi katika mashariki na magharibi. Sababu ya kwanza ya uadui kwa Uislamu ni utu wake, uadilifu wake na kuzuia kwake dhulma na ufisadi. Kwa sababu hiyo ndio wanawakusudia na kila shari na kuwapiga vita kwa nyenzo mbalimbali. Vile vile kuwafitini kulingana na hali ilivyo. Kwa hiyo ni juu yetu kuzinduka na maadui hawa na kuwapiga vita kwa silaha ile ile wanayotupiga nayo.

Na yeyote katika atakayertadi, kisha akafa hali yakuwa kafiri, Basi hao zimepomoka amali zao katika dunia na Akhera . Na hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele.

Hii ni hadhari kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa mwenye kuwaitikia maadui na kutoka dini yake, basi mtu huyo amepata hasara ya duniani na akhera na mwisho wake ni Jahannam ambayo ni marejeo mabaya.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Kisha akafa hali yakuwa kafiri," inafahamisha waziwazi kwamba mwenye kurtadi (kutoka) katika dini, akitubia kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu huikubali toba yake na huondokewa na adhabu; na akili inakubaliana na hilo. Lakini mafaqihi wa kishia wamesema: Ikiwa ni mwanamume na kutoka kwake kukawa kunatokana na kuzaliwa; kisha akatubia, basi ataondokewa na adhabu ya akhera tu, ama ya duniani ambayo ni kuuliwa itakuwapo. Kama kukiwa kutoka kwake
kunatokana na mila basi hatauawa.1 Katika ufafanuzi huu wametegemea riwaya za Ahlul Bait (a.s).

Maana ya kupomoka amali zao katika dunia ni kuwa wao watafanyiwa muamala wa kikafiri kuongezea kustahiki kuuawa. Ama kupomoka amali zao huko akhera, ni adhabu na mateso.

Hakika wale walioamini na wale waliohama na wakafanya jihadi kati- ka njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kutarajia rehema ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutaja hali ya washirikina na waliotoka katika Uislamu na kutaja adhabu yao, amefuatishia kutaja waumini na malipo yao.

waliohama (Muhajirina) ni wale kutoka Makka kwenda Madina pamo- ja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na waliofanya jihadi ni wale waliotoa juhudi zao katika kuunusuru Uislamu na kupigana na maadui zake.

Ibada Ya Mwenye Kutubia Baada Ya Kurtadi (Kutoka Katika Uislamu)

Mwenye kutoka katika Uislam (murtadi) akitubia na akarudi katika Uislamu kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu humkubalia toba yake kwa hukumu ya kiakili na kwa dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Kisha akafa hali yakuwa kafiri" alipounganisha kupomoka amali na kufa katika hali ya kafiri.

Hapo basi yanakuja maswali mawili: Swali la Kwanza: Je, ibada zake kama vile swala, Hijja, Saumu na Zaka, zitasihi baada ya kurudi kwenye Uislamu?
Mafaqihi wa Kisunni wameafikiana kuwa zinasihi na kukubaliwa. Mafaqihi wa Kishia wameafikiana kwamba zinazokubaliwa ni za yule wa mila, na wamehitalifiana katika wa kuzaliwa. Wengi wao wamesema hazisihi kwa hali yoyote na kwamba Uislamu wake baada ya kuutoka, haumfai na chochote katika dunia kabisa, bali atatendewa muamala anaofanyiwa kafiri;isipokuwa Uislamu wake utamfaa akhera tu, kwa kuondokewa na Adhabu. Lakini wahakiki wa mambo katika Shia wamesema, bali zinasihi ibada zake, na utamfaa Uislamu wake na atafanyiwa muamala wa Kiislamu. Nasi tuko pamoja nao.

Swali la Pili: Je, Murtadi akirudi katika Uislam atalazimika kulipa ibada zake alizozifanya wakati alipokuwa Mwislamu kabla ya kurtadi. Hanafi na Maliki wamesema, atalazimika kulipa. Na Shafii amesema hatalazimika.

Ama Mafaqihi wa Kishia wamesema kuwa zinasihi ibada za mwenye kutubia baada ya kurtadi, wao wanasema mtu halipi chochote alichokifanya wakati ni Mwislamu, isipokuwa atalipa yaliyompita wakati wa kutoka Uislamu (kurtadi).

Kupomoka

Mu'utazila wamesema kuwa thawabu za Mumin mtiifu zinaanguka zote kwa maasi yatakayofuatia; mfano hata mwenye kuabudu umri wake wote, kisha akanywa tama moja tu la pombe, basi ni kama ambaye hakumwabudu Mwenyezi Mungu kabisa. Vile vile twaa inayofuatia inaondoa madhambi yaliyotangulia; na hayo ndiyo maana ya kupomoka amali.

Shia Imamiya na Asha’ri wameafikiana kuwa hakuna kuharibika; wakasema kila amali ina hisabu yake inayoihusu; wala twaa haifungamani na maasi, nayo hayafungamani na twaa, bali atakayefanya wema (hata) uzani wa sisimizi atauona. Mwenye kufanya uovu na wema akiwa muumini Mwenyezi Mungu ataupima wema wake na uovu wake. Ikiwa wema utazidi, atakuwa kama ambaye hakufanya uovu, kwa sababu wingi unafuta uchache. Ikiwa yote ni sawa, basi atakuwa kama ambaye hakutokewa na lolote.

Kupomoka kuko mbali sana na maana haya; maana yake hasa ni mwenye kufa akiwa kafiri baada ya kuwa Mwislamu, ukafiri wake huu utakuwa unafichua amali zake alizokuwa akizifanya wakati wa kusilimu, kuwa hazikuwa katika njia inayotakikana tangu mwanzo; sio kwamba alistahiki thawabu kisha zikafutwa, bali hili ni katika upande wa kuzuwia sio kuondoa; yaani thawabu hazikuwepo.

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِنْ نَفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنْفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ {219}


Wanakuuliza kuhusu ulevi


n


a


kamari


.


Sema


:


Katika


hivyo mna madhara makubwana manufaa kwawatu, na madhara yake ni makub


w


a


zaid


i


kulik


o


manufaa


yake.Nawanakuulizawatoe nini?Sema:


V


ilivyowazidia. Namna hii Mwenyezi Mungu


anawabainishi


a


A


y


ampate


kufikiri.

فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِنْ تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {220}


Katika dunia naakhera.Na wanakuulizakuhusu maya


tima


.


Sema:


Kuwatengenezea ndiyo heri. Na kamamkichanganyika nao, basini ndugu zenu. Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadina mtengenezaji.Na kama angelitaka Mwenyezi


Mung


u


angeliwati


a


katika dhiki


.


Hakik


a


Mwenyezi Mung


u


n


i


Mwenye


nguvu,Mwenyehekima.

  • 1. Kuzaliwa ni kuwa mwislamu na wazazi wake au mmoja wao ni Mwislamu na mila ni kuwa wazazi wake ni makafiri, kisha yeye akasilimu baadaye akatoka kwenye Uislamu.