read

Aya 219-220: Ulevi Na Kamari

Lugha

Limetumiwa neno Khamri, lenye maana ya kufunika, kwa maana ya ulevi, kwa sababu ulevi unafunika akili. Na limetumiwa neno Maysir, lenye maana ya wepesi, kwa maana ya kamari, kwa sababu chumo la kamari linakuwa jepesi bila ya jasho.

Maana

Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari.

Waliuliza baadhi ya Waislamu kuhusu hukumu ya ulevi na kamari katika Madina; yaani zaidi ya miaka 13 tangu ulipoanza mwito wa Kiislamu.

Hiyo inafahamisha kuwa hukumu ya pombe ilikuwa imenyamaziwa muda mrefu, kama zilivyonyamaziwa baadhi ya hukumu za haramu mpaka wakati wake maalum, kulingana na masilahi. Mara nyingine kubainisha hukumu kunataka hekima ya kuchukulia mambo pole pole.

Inasemekana kuwa ubainifu wa hukumu ya pombe ulikuwa hivi, kwa sababu Waislamu walikuwa wameizoweya wakati wa Ujahiliya (kabla ya kuja Uislamu); lau wangelizuiliwa mara moja tu, ingelikuwa uzito kwao.

Bali Mwenyezi Mungu aliwakumbusha Waislamu walipokuwa Makka kwamba katika jumla ya neema zake ni kwamba wao wanafanya ulevi na kupata riziki kutokana na tende na zabibu. Anasema Mwenyezi Mungu:

وَمِنْ ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ {67}


"Nakutokananamatundayamitendenamizabibumnatengenezaulevina rizikinzuri..."(16:67)

Waliuliza baadhi ya Waislamu kuhusu hukumu ya pombe na kamari, Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwajibu: Katika hivyo madhara makubwa na manufaa kwa watu na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Jawabu hili peke yake halitoshi kuwa ni dalili ya uharamu wa ulevi. Kwa sababu hakusema kuwa ni haramu; linafahamisha kawaida ya kujikinga na madhara ni bora kuliko maslahi, na muhimu inatanguliwa na muhimu zaidi.

Lakini tukiangalia Aya isemayo:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ {33}


"Sema: Mola wangu ameharimisha mambo maovu yaliyodhihirika na yaliyofichikanamadharanauasipasipohaki..."(7:33)

Tukiiunganisha Aya hiyo na hii tunayoizungumzia tutapata dalili ya kuharimishwa ulevi waziwazi na kwa mkato.

Kwa sababu natija inayopatikana ni kuwa ulevi ni madhara na madhara ni haramu, kwa hivyo ulevi ni haramu. Hiyo ni pamoja na kuongezea Aya inayosema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {90}

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ {91}


"Enyimlioamini!Hakikaulevinakamarinamasanamunamishaleyakutizamia(ramli)niuchafu katikakazi ya Shetani. Basijiepusheni navyo, ili


mpat


ekufaulu


.Hakik


aShetan


ianatakkuwatili


auadu


in


abughudh


abaina yen


u


kw


a


ulev


i


n


a


kamar


i


kuazuili


a


n


a


kumkumbuk


a


Mwenyez


i


Mungu n


aKuswali


.Bas


ije


,mtaacha?


"(5:9


0-91)

Kwa hiyo kusema jiepusheni navyo ni amri ya kujiepusha, na amri inafahamisha wajibu. Na kusema basi je mtaacha! Ni kukataza, na kukataza kunafahamisha uharamu. Ndipo Waislamu waliposikia Aya hii wakasema: "Tumeacha."
Ama ile Aya inayosema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ{43}


"Enyimlioaminimsiikurubieswalahalimmelewa..."(4:43)

Ilishuka kabla ya Aya (5:90-91), ambazo zina uzito mkubwa. Tumeeleza kwamba huenda ilikuwa ni hekima ya kuchukulia mambo pole pole katika kubainisha uharamu, kwa vile kutoikurubia swala hali mme-lewa haina dalili yoyote ya kuonyesha uhalali wa pombe katika isiyokuwa swala. Tutafafanua Inshaallah tutakapofikia Aya hizo.

Zaidi ya hayo Waislamu wote tangu mwanzo hadi hivi leo wamekongamana kwa kauli moja tu! Kuwa ulevi ni katika madhambi makubwa, na kwamba mwenye kuuhalalisha siye Mwislamu. Na mwenye kuinywa kwa kupuuza ni fasiki na atapigwa (Had) viboko themanini.

Imekuja Hadith Mutawatir kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba amelaaniwa mwenye kupanda mti wa (hiyo pombe), mwenye kuigema, mwuzaji, mnunuzi, mwenye kuhudumia wanywaji na mnywaji. Na imeelezwa katika baadhi ya hadith kwamba hakuna sharia yoyote ya mbinguni ila imekataza ulevi. Tumeyaeleza kwa ufafanuzi zaidi maudhui haya katika juzuu ya nne ya kitabu “Fiqhul Imam Jaffar Sadiq” katika mlango wa vyakula na vinywaji.

Na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Makusudio ya ithm hapa ni madhara. Madhara ya pombe yanadhihirika katika mwili, akili na mali na vile vile kuacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kugombana na kufanya mambo yaliyoharamishwa.Wanahistoria wanasema kwamba baadhi ya walevi walizini na mabinti zao.

Abbas bin Mirdas, alikuwa kiongozi wa watu wake, katika zama za Jahiliya (kabla ya Uislamu) alijiharimishia pombe yeye mwenye tu kwa maumbile yake. Alipoulizwa sababu, akasema: "Siwezi kuchukua ujinga kwa mkono wangu nijiingize mwenyewe, wala siko radhi asubuhi niwe bwana mkubwa wa watu na jioni niwe mpuzi wao."

Daktari mmoja mashuhuri wa Kijerumani alisema: "Fungeni nusu ya mabaa na mimi ninawadhaminia kuwa hamtahitajia nusu ya zahanati na mahospitali na majela."

Ama kamari inaleta uadui na chuki na inazuia kutajwa Mwenyezi Mungu; kama ilivyoonyesha Aya tukufu, inaharibu tabia kwa kuzoeya uvivu na kutafuta riziki kwa ndoto tu! Pia inavunja majumba na inamtia mtu kwenye umasikini ndani ya saa moja tu. Inatosha kuwa haramu kamari, kule kuchukua mali bure bure tu.

Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Vilivyowazidia.

Yaani: Toeni vilivyozidi haja zenu na za familia yenu. Amri ya kutoa hapa ni ya suna sio ya wajibu, isipokuwa inakuwa wajibu kutoa kama zikithibiti sharti za khumsi na zaka. Tutaelezea kwa ufafanuzi, Inshaallah.

Aya hii ni kama Aya isemayo: "Wala usifanye mkono wako ni wenye kufungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo utakuwa ni mwenye kulaumiwa mwenye kufilisika." (17:29)

Imeelezwa katika Hadith kwamba mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na kibonge cha dhahabu kama yai, akamwambia Mtume: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu chukua hii ni sadaka Wallah sina chochote zaidi ya hiyo."

Mtume akaachana naye; kisha akamfuata tena na kurudia kumwambia, kisha Mtume akakichukua na kumrudishia mwenyewe akisema: "Mtu ananijia na mali yake naye hana kitu kingine chochote; kisha aombe watu! Hakika sadaka inatokana na kujitosha; chukua mwenyewe hatuna haja nayo."

Iko Hadith pia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiiwekea familia yake matumizi ya mwaka mzima.

Namna hii anawabainishia Mwenyezi Mungu Aya mpate kufikiri katika dunia na akhera

Yaani Mwenyezi Mungu anawabainishia hukumu yake katika pombe na kamari, na hukumu yake katika vile ambavyo tunatakikana kuvitoa sadaka katika mali zetu kwa misingi ya maslahi yetu. Yeye haamrishi isipokuwa lile ambalo lina maslahi ya kidunia na askhera, na wala hakatazi isipokuwa lile lenye uharibifu.

Yatupasa kuuzingatia na kuuchunga uhakika huu tusimwasi Mwenyezi Mungu katika jambo lolote miongoni mwa amri na makatazo yake.

Kwa hivyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mpate kufikiri katika dunia na akhera" ni kwamba tufanye amali kwa ajili ya zote mbili (dunia na akhera) bila ya kuacha moja.

Na wanakuuliza kuhusu mayatima.

Wakati wa ujahilia (kabla ya Uislamu) watu walizowea sana kunufaika na mali za mayatima; pengine mtu aliweza kumwoa yatima au kumwoza mtoto wake kwa tamaa ya mali yake tu.

Ulipokuja Uislamu, Mwenyezi Mungu alimteremshia Mtume wake Aya hizi:

إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ {10}


"Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhulma, hakika wanakulamotomatumbonimwao..."(4:10)

وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ {152}


"


W


alamsikaribiemali ya yatima isipokuwa kwa njia ya wema kabisa..."(6:152)

Basi ziliposhuka Aya hizo waliacha kuchanganyika na kuwasimamia mayatima. Hapo maslahi yao yakaharibika na maisha yao yakawa mabaya. Ndipo baadhi ya Waislamu wakauliza kuhusu hali hiyo. Likaja jawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

Sema: Kuwatengenezea, ndio heri.

Maana yake msijizuilie na kuchanganyika na mayatima na kuzikurubia mali zao, kama mnataka kuwatengenezea uzuri katika malezi yao, adabu zao na kusimamia mali zao. Bali hilo lina malipo na thawabu. Lenye kuharamishwa ni kuzifuja na kuzila mali zao.

Na kama mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu.

Kundi la wafasiri limesema: "Hii ni idhini kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa anayesimamia yatima kumshirikisha pamoja na familia yake katika kula na kunywa ikiwa hilo ni sahali kwa msimamizi na achukue kutoka katika mali ya yatima kiasi kile cha malezi

Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadi na mtengezaji.

Fisadi ni yule anayesimamia yatima ili afuje mali zake: Na mtengezaji ni yule anayesimamia mali ya yatima kwa maslahi ya yatima kwa dhati. Kwa hivyo kauli yake hiyo Mwenyezi Mungu ni kemeo kwa mwenye kutaka kufuja na kufanya ufisadi.

Na kama Mwenyezi Mungu angelitaka angeliwatia katika dhiki.

Makusudio hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu amehalalisha kuchanganyika yatima na familia ya msimamizi na kuchukua katika mali ya yatima thamani ya kile alichompatia posho, ili yasipatikane mashaka na uzito. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anawatakia watu wepesi wala hawatakii uzito.

Hapa inaonyesha kuwa si lazima kuwe na usawa wa kutopungua hata kidogo kati ya kile alichokula yatima pamoja na familia ya msimamizi na kile atakachochukua badali kutoka katika mali ya yatima. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) husamehe tofauti ndogo isiyoepukika, bali msimamizi anaweza hata kula katika mali kwa wema akiwa fukara. Hayo ni kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَمَنْ كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَنْ كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ{6}


"...Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe, na atakayekuwamhitajibasi ale kwa kadriyaada.(4:6)

وَلَا تَنْكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنْكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُؤْمِنٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ {221}


W


ala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi muumini ni bora


kulik


o


mshirikin


a


hata akiwapendeza


.


W


al


amsi


waoze wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa


muumin


i


n


i


bor


a


kuliko


mshirikina hata akiwapendeza. Hao wanaita kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu


anait


a


kweny


e


Pep


o


na


maghufira,kwaidhini


Y


ake. Nayehubainisha


A


yaZake kwawatuili wapate kukumbuka.