read

Aya 221: Msiwaoe Wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu

Maana

Aya hizi ni miongoni mwa Aya za hukumu, na zinaingia katika mlango wa ndoa. Kabla ya kuingilia madhumuni ya Aya, kwanza tutajaribu kufasiri neno. Nikah, Mushrikina, Amah,

Neno (Nikaha) lina maana mbili: Kufunga ndoa na kumwingilia mwanamke. Neno Mushrikina (washirikina) imesemekana kuwa ni kila asiyeamini utume wa Muhammad (s.a.w.w.). Kwa kauli hii watakuwa wanaingia watu wa Kitabu ambao ni Mayahudi, na Wakristo. Na inasemekana kuwa Qur'an haikusudii watu wa Kitabu, japo wanasema kuwa Issa ni Mwana wa Mungu na utatu wa Mungu. waliosema haya wametoa dalili kwa Aya hizi:

مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ{105}


"Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu wala washirikina..."(2:105)

لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ{1}


"Hawakuwa, wale ambao wamekufuru katika watu wa Kitabu na washiririkina..."(98:1)

Katika Aya hizo kuna viunganishi kati ya watu wa kitabu na washirikina, na kiunganishi kinafahamisha tofauti. Kwa sababu kitu hakiwezi kuungan- ishwa na kitu hicho hicho.

Neno Amah (mjakazi) na Abd linatumiwa kwa mtumwa na hata aliyehuru. Unaweza kumwambia aliyehuru: "Ewe mjakazi wa Mwenyezi Mungu," vile vile mtumwa kwa sababu binadamu wote ni watumwa wa Mwenyezi Mungu.

Maana ya Aya ni kuwa enyi Waislamu msioane na washirikina, bali oaneni na wanaotokana nanyi hata kama sio bora kama washirikina kwa umbo na tabia au kwa jaha na mali.

Hao wanaiita kwenye moto.
Yaani hao washiikina. hikima ya kukataza kuoana ni hiyo ya mwito wa motoni, na kwamba muungano wa kuiondoa unapelekea uharibifu wa itikadi na dini. Kwa ufupi unapelekea ufasiki na kupuuzwa hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Tunashuhudia hivi leo vijana wetu wengi wako katika hali mbaya kuliko makafiri na washirikina, kutokana na kudharau kwao, kuipuuza dini na kujivua kabisa katika athari za dini. Wanawalea watoto wao malezi yasiyokuwa ya dini wala ya tabia njema. Lau sikuwa walishuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake, basi tungeliwafanyia muamala wa walahidi na washirikina.

Lakini kwa sababu ya tamko hili tu (la shahada), ndilo limehifadhi damu, mali na kusihi kuoana na kurithiana nao hata kama haya yanatokana na njia za taqlid na kurithi.1

Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye pepo na maghufira.

Hapa kuna miito miwili:

• Mwito wa kwanza: Ni wa wanaoshirikisha - kufanya yale yanayoingiza motoni na kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

• Mwito wa pili: Ni wa Mwenyezi Mungu - kufanya yanayoleta maghufira na kuingia peponi. Miongoni mwa hayo ni kuoa mwenye kuamini na wala sio mwenye kushirikisha. Hapana mwenye shaka kwamba wanaoamini ndio wanaoitika mwito wa Mwenyezi Mungu na wanapata maghufira yake na hatimae kuingia pepo Yake kwa idhini Yake; yaani kwa uongofu na tawfiki yake.

Kuoa Mwenye Kitabu (Ahlul-Kitab)

Wameafikiana Waislamu kwamba haijuzu kwa Mwislamu kuoa au kuolewa na asiyekuwa na kitabu; kama vile kuoa wale wanaoabudu masanamu, jua na moto, n.k. kwa ufasaha zaidi yule asiyeamini.

Vile vile haijuzu kumuoa au kuolewa na Majusi, hata kama imesemwa Majusi ni shabihi ya wenye kitabu.

Wameafikiana madhehebu manne ya Ahli Sunna juu ya kusihi kumuoa mwenye kitabu, na wamehitalifiana Mafaqihi wa Kishia. Wengi wao wamesema kuwa haijuzu kwa Mwislamu kumuoa Yahudi au Mkristo. Na wengine wamesema inajuzu. Miongoni mwa Ulamaa wakubwa waliosema hivyo ni Sheikh Muhammad Hassan katika Jawahir, shahidi wa Pili katika Masalik na Sayyid Abul Hassan katika Wasilah, wamesema inajuzu. Na sisi tuko pamoja na rai hii kwa dalili hizi:

1. Dalili zinazohalalisha ndoa zimemtoa Mwislamu mwanamume kumwoa Mshirikina, na Mwislamu mwanamke kuolewa na mshirikina na mwenye kitabu. Kwa hivyo inafahamisha kuwa wasiokuwa hao inajuzukuoa.

2. Kauli yake Mwenyezi Mungu:

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ {5}


"Leo mmehalalishiwa kula vilivyo vizuri na chakulacha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu nihalali kwao na wanawake wasafi waumininawanawake wasafi katika wale waliopewa kitabu kabla yenu..."(5:5)

Kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu: Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa (zenu),” makusudio ya makafiri hapo ni washirikina sio wenye Kitabu. Kwa sababu Aya iliwashukia wanawake waliosilimu na kuhama na Mtume wakiwaacha waume zao washirikina; na mfumo mzima wa Aya unafahamisha hivyo. Aya yenyewe ni hii:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُمْ مَا أَنْفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنْكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا{10}


"Enyimlioamini!W


atakapowajiawanawake walioamini wanaohama,basi wafanyienimtihani; Mwenyezi Mungundiyeajuayezaidiimaniyao. Mkiwajuaniwaumin


ibas


imsiwarudish


ekw


amakafiri


.Haw


as


ihalal


ikwa ha


o


(wanaum


e


makafiri


)wal


awa


o(wanaum


emakafiri


)


s


i


halal


i


kwao


.


Na warudishien


i(waum


ezao


)(mahari


)waliyotoa


.W


al


akwen


us


ivibay


akuwaoa ikiw


amtawap


amahar


iya


o(ha


owanawake


)kwenu


.W


al


amsiwawek


ekatika kifung


o


ch


a


makafiri..."(60:10)

Pia ziko Hadith sahihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) katika kusihi kumuoa mwanamke katika wenye kitabu, na haya tumeyafafanua zaidi katika juzuu ya tano ya kitabu. Fiqhul Imam Jafar Sadiq. Mlango yaliyoharamu, kifungu cha kutofautiana dini

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ {222}


W


anakuuliza kuhusu hedhi; waambie ni udhia. Basijitengeni na wanawake wakati wa hedhi wala msiwakaribie mpaka watoharike.W


akisha toharika basi waendeni pale


alipowaamrish


a


Mwenyezi Mungu


.


Hakik


a


Mwenyezi


Mungu huwapenda wanaotubia na huwapenda wanaojitoharisha.

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنْفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ مُلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ {223}


W


ake zenunimashamba yenu. Basi yaendeeni


mashamb


a


yen


u


mpendavyo, n


atangulizien


inafs


izenu


;na mchen


i


Mwenyez


i


Mung


u


na


jueni kwamba mtakutana


Naye


,


n


a


wap


e


habar


i


njema weny


ekuamini.

  • 1. Ndoa na mirathi zinakuwa kwa dhahiri ya Uislamu, sio kwa Uislamu halisi. Hayo tumeyafanyia utafiti katika kitabu Usulul-ithbat sehemu ya madai na kuhalifu sharia.