read

Aya 222-223: Hedhi

Maana

Baada ya kumuuliza Mtume mtukufu (s.a.w.w.) kuhusu miezi mitakatifu, ulevi, kamari watakachotoa na mayatima; kisha walimuuliza kuhusu hedhi. Amesema Razi: "Imepokewa habari kuwa Mayahudi na Majusi walikuwa wakikaa mbali sana na wanawake wakati wa hedhi; Wakristo walikuwa wakiwaingilia bila ya kujali hedhi; na watu wa zama za Jahiliya (kabla ya Uislamu) walikuwa hawali, hawanywi, hawakai kitanda kimoja wala hawakai nyumba moja na mwanamke mwenye hedhi; kama walivyokuwa wakifanya Majusi na Mayahudi.

Wanakuuliza kuhusu hedhi; waambie ni udhia. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.

Swali linahusu kuchanganyika na wanawake wakati wa hedhi, ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake mtukufu kuwajibu waulizaji kwamba wajitenge na wanawake siku za hedhi; yaani wasiwaingilie. Imekuja Hadith inayosema; "Fanyeni kila kitu isipokuwa kuingilia tu."

Makusudio ya neno 'Adha' (udhia) ni madhara kwa kuwa ni uchafu na najisi.

Wala msiwakurubie mpaka watoharike.

Wamehitalifiana juu ya makusudio ya kutoharika kuwa je, ni kukatika damu tu bila ya kuoga au ni pamoja na kuoga? Yaani inajuzu kuingiliwa kabla ya kuoga au la?
Wamesema Shia inajuzu kumwingilia hata kabla ya kuoga kwa vile ndio ufahamu wa tamko Tuhr watoharike. Ama kujitoharisha hiyo ni kazi ya wanawake ambayo inakuwa baada ya tohara (kwisha damu).

Amesema Malik na Shafii: Haijuzu ila baada ya kuoga. Na wanasema Hanafi: Ikiendelea damu kwa muda wa siku kumi, inajuzu kumkurubia kabla ya kuoga, lakini ikakatika damu kabla ya siku kumi haijuzu mpaka aoge. Mwenye tafsiri ya Al Manar ameelezea juu ya ufafanuzi huu kwa kusema: "Huu ni ufafanuzi wa kushangaza."

Wakishatoharika, basi waendeeni pale alipowaamrisha. Mwenyezi Mungu.

Neno pale ni uhakika wa mahali, kwa maana ya tupu ya mbele, kama inavyofahamika. Masuala ya hedhi na hukumu zake tumeyazungumzia kwa ufafanuzi zaidi katika kitabu Fiqhul Imam Jaffar Sadiq na kitabu Al Fiqhu ala Madhahibil Khamsa.

Wake zenu ni mashamba yenu. Basi yaendeeni mashamba yenu mpendavyo.

Neno “Anna Kulingana na sarufi (nahw ya Kiarabu) lina maana ya vyovyote, wakati wowote au popote. Zimekuja kauli nyingi kuhusu maana ya neno hilo Anna katika Aya hii: Kuna mwenye kusema: Ni kwa maana ya wakati wowote; yaani muwaendee (muwaingilie) wakati wowote usiku au mchana. Wengine wakasema ni kwa maana ya popote yaani mna hiyari ya kuwaingilia popote tupu ya mbele au nyuma. Vile vile kuna mwenye kusema ni kwa maana ya vyovyote; yaani hali yoyote kukaa, kulala, n.k.

Limesema kundi la wafasiri, miongoni mwao akiwa ni mwenye Tafsiri ya Al Manar ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni na mwenye Tafsiri ya Bayanu Ssada ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wa Kishia, kwamba Neno shamba linafungamana na mazao na ni tupu ya mbele tu, ndiyo ambayo inaweza kuoteshwa mazao (Mtoto ). Kuongezea kuwa kuendea tupu ya nyuma ni udhia.

Sisi tunaiunga mkono rai hii kwa sababu mbili: Kwanza, mazao hayapatikani isipokuwa kwa kupitia tupu ya mbele tu, kama walivyotaja wafasiri hao. Pili, kauli yake Mwenyezi Mungu "Waendeni pale alipowaamrisha Mwenyezi Mungu” inaonyesha makusudio yake ni mbele baada ya kufasiri hayth kwa maana ya mahali.

Kuna baadhi ya Mafaqihi wa Kishia wanaojuzisha kumwendea mke nyuma lakini kwa makuruhu makubwa sana.

Wengine wamedai ati kuwa hayo yanahusika na Shia tu! Na kwamba hawaafikiani na yeyote katika hilo; na inajulikana kuwa Razi (mwanachuoni wa kisunni) amenakili katika kuifasiri Aya hii kwamba, Ibn Umar na Malik walikuwa wakisema: "Makusudio ya Aya ni kujuzisha kuwaendea wanawake nyuma." Na Al- Hafidh Abu Bakr Al-Andalusi wa madhehebu ya Kimalik (Sunni) - aliyekufa mwaka 542 Hijriya - katika juzuu ya kwanza ya kitabu Ahkamul Qur'an ukurasa 73 chapa ya mwaka 1331 A.H.; alisema hivi ninamnukuu: “Wamehitalifiana wanavyuoni katika kujuzu kumwendea mke nyuma, wengi wamejuzisha."

Ameyaeleza hayo Ibn Shaban katika Jimau nnis-wan wa Akhkamul Qur'an.

Sunni Na akategemeza, riwaya nyingi kujuzu kwake, kwenye kundi tukufu la masahaba, na Tabiina na kwa Malik. Bukhari ametaja kutoka kwa Ibn Aun, kutoka kwa Nafi kwamba Ibn Umar alikuwa akisoma Sura ya Baqara mpaka alipoishia 'Anna shiitum' alisema: "Je unajua imeteremka kwenye nini?" Nikasema: "La." Akasema: "Imeshuka katika kadha na kadha"; yaani tupu za nyuma za wanawake.

وَلَا تَجْعَلُوا اللَّهَ عُرْضَةً لِأَيْمَانِكُمْ أَنْ تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ {224}


Wala msimfanye Mwenyezi Mungu ni pondokeo la viapo vyenu, (ili) mfanye mema na mumche (Mwenyezi Mungu) na muwe wema kati ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ {225}


MwenyeziMungu hata


washik


a


kw


a


sabab


u


ya kuap


a


kwen


u


kw


a


upuzi upuzi


,


lakin


i


atawashika


katik


a


yaliyokusudiw


a


na


nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufiraMpole.

لِلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِنْ فَاءُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {226}


Kwawaleambaowanaapa kujitengana wake zaoni kungojea miezi minne. Na


kam


a


waki


r


eje


a


basi Mwenyez


i


Mung


u


ni Mweny


e


maghufira


Mwenyeku


r


ehemu.

وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ {227}


Na wakiazimiatalaka,basi


Mwenyez


i


Mung


u


ni Mweny


e


kusikia


,


Mwenye


kujua.