read

Aya 36: Kuwatendea Wema Wazazi Wawili

Maana

Na mwabuduni Mwenyezi Mungu.

Hakuna kitu cha kumwabudu Mwenyezi Mungu kilicho bora zaidi kuliko kupi- gania na kufa shahid kwa ajili ya haki; uhuru na ubinadamu. Ama kutafuta elimu na kufanya kazi kwa ajili ya maisha, kusaidia mambo ya kheri na kupatanisha watu waliokosana ni bora kuliko Swala zote na Saumu zote; kama iliivyoelezwa katika Hadith.

Wala msimshirikishe na chochote.

Kuukana uungu ni ukafiri; na kumshirikisha Mungu kuko aina mbili; Kumshirikisha katika Uungu; kama vile kuamini kuwa mwenye kuumba na kuruzuku ni zaidi ya mmoja. Miongoni mwa ushirikina huu ni kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ana mawaziri, wasaidizi na washauri.

Aina nyingine ya ushirkina ni katika utiifu; huko ni kuamini kuwa muumba, mwenye kuruzuku ni mmoja hana mshirika wala msaidizi, lakini ukawa unamwasi kwa kumtii kiumbe kwenye jambo ambalo halitamridhisha Mwenyezi Mungu, Vilevile miongoni mwa ushirikina ni kumridhia mtawala dhal- imu, waziri au naibu wake mwenye hiyana, na kadhi mjinga aliye mwovu, na yeyote anayesimamia mambo ya umma ambayo hana ujuzi nayo. Kuna Hadith isemayo 'Mwenye kuwaridhia watu kwa mambo wayafanyayo basi yu pamoja nao.'

Na watendeeni wema wazazi wawili.

Mara nyingi Mwenyezi Mungu hukutanisha wajibu wa kuabudiwa kwake na wa kutendewa wema wazazi wawili, katika Aya kadha; kama vile: "Na Mola wako amehukumu kuwa msimwabudu yeyote isipokuwa yeye tu, na kuwafanyia wema wazazi wawili; kama mmoja wao akifikiliwa na uzee naye, yuko kwako, au wote, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee na useme nao kwa msemo wa heshima." (17:23)

Aya nyingine ni ile isemayo: "… kwamba unishukuru mimi na wazazi wako wawili; ni kwangu mimi mare- jeo." (31:14)

Miongoni mwa dua za Imam Zainul-abidin kwa wazazi wake ni: "Ewe Mola wangu! Ni urefu ulioje wa kunishughulikia (wazazi) wangu kunilea! Ni tabu ilioje waliopata kunilinda! Na ni kujinyima kulikoje kwao kwa ajili ya kunitosheleza! Haiwezekani kwangu mimi kuwatekelezea haki zao, wala siwezi kutekeleza wajibu wangu kwao au kuwalipa huduma zao."

Na jamaa wa ukoo.

Hao ni kama ndugu wa kuzaliwa nao, ami n.k.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuwafanyia wema wazazi wawili, hapa ameamrisha kuwafanyia wema ndugu kisha ni mayatima na maskini. Hata kama si jirani kwa sababu yatima hana wa kumsaidia, yaani baba. Na kwamba maskini hawi sawa kijamii ila kwa kusaidiwa. Masikini anayehitajia kusaidi- wa, ni yule dhaifu asiyeweza kuchuma.

Ama kumsaidia mwenye kuweza kufanya kazi lakini akawa ni mvivu, ni kuchochea uduni uzembe. Kuna Hadith isemayo: "Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja anayefanya kazi na humchukia mvivu." Wanafunzi walimwuliza Nabii Isa: "Ni nani mbora zaidi katika sisi" Akasema: "Mbora wenu zaidi ni yule anayefanya kazi kwa mkono wake na kula kwa chumo lake."

Na jirani wa karibu na jirani wa mbali na rafiki wa ubavuni na msafiri na waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia.
Rafiki wa ubavuni ni yule mwenzako safarini, unayekaa naye mjini, unayeso- ma naye darasani au unayefanya kazi naye n.k. Msafiri hapa ni yule aliyeharibikiwa safarini.Waliomilikwa na mikono ni watu ambao hawako hivi sasa(watumwa).

Kufanya wema sio lazima kutoa mali tu, bali ni pamoja na kufanyiana upole, unyenyekevu, kujishughulisha kutimiza mahitaji yao kushauriana na kuficha siri. Pia ni pamoja na kuzifumbia jicho aibu za watu, kutotangaza ubaya wa watu, kuazimana vifaa na mengineyo mfano wa hayo.

Kwa vyovyote ni kuwa amri ya kuwafanyia wema wote hawa ni Sunna si wajibu.

Hakika Mwenyezi Mungu hapendi mwenye kiburi ajivunaye.

Hili ni kemeo kwa mwenye kujitenga na jamaa zake walio mafukara na jirani zake.

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُهِينًا {37}

Ambao hufanya ubakhili na huwaamuru watu kufanya ubakhili, na wakayaficha aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake. Na tumewaandalia Makafiri adhabu yenye kudhalilisha

وَالَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ وَمَنْ يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا {38}

Na wale ambao wanatoa mali zao kwa kuonyesha watu wala hawamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho. Na ambaye shetani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya.

وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ آمَنُوا بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقَهُمُ اللَّهُ ۚ وَكَانَ اللَّهُ بِهِمْ عَلِيمًا {39}

Na ingeliwadhuru nini lau wao wangelimwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakatoa katika aliyowaruzuku, na Mwenyezi Mungu anawajua.