read

Aya 44 – 47: Hununua Upotevu Na Kuwataka Mpotee

Israil Na Nguvu Ya Shari

Je huwaoni ambao wamepewa fungu katika Kitabu hununua upotevu na kuwataka mpotee njia.

Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa makusudio ya waliopewa fungu kati- ka Kitabu ni Mayahudi ambapo amewasifu Mwenyezi Mungu kwanza kwa upotevu; pale aliposema hununua upotevu, na pili kwa upotezaji pale aliposema: na kuwataka mpotee. Kisha akawasifu kwa ugeuzaji maneno, pale aliposema: hugeuza maneno kutoka mahali pake.

Historia haikujua watu walio wapinzani zaidi wa haki na maadui wa kheri kuliko Mayahudi. Wamekuwa wapotevu, wapotezaji na wageuzaji maneno, pale walipokuwa madhalili waliotawaliwa. Ama leo baada ya dola dhalimu kuwatengenezea wao koloni, hawakuacha upotevu, upotezaji na kugeuza maneno.

Bali wamekuwa ni nembo ya shari ya kimataifa na silaha na maangamizi aliyonayo kila mkoloni mkandamizaji, na ni kipimo cha kupambanua nguvu ya shari na uhaini na ile ya heri na ukombozi.

Hakuna dola yoyote ya kikoloni, wakati huu inayotaka kutawala watu, lazima itakimbilia Israel ndipo itaweza kutekeleza lengo lake. Taifa lolote dhalimu Mashariki na Magharibi lazima liombe msaada wa kuhami masilahi yake kwenye watu hawa dhalimu wenye dhambi.

Al-hamdulillah, dalili zimejionyesha waziwazi katika Vietnam za kumwandalia binadamu mpya atakayejua njia ya kummaliza adui wa haki na wa ubinadamu.

Binadamu wa leo1 katika Vietnam na binadamu wa kesho mahali popote, atatofautiana na binadamu wa jana.

Yeye anaweza kumtofautisha mwenye haki na uhaini bila ya utatanishi, hata kama atakinaishwa mara elfu na ataweza kumweka kila mmoja mahali pake. Hapo binadamu ataweza kuishi bila ya matatizo na mabomu.

Matukio yamethibitisha - hasa lile balaa la tarehe 5 June 1967- kwamba mata- tizo ya waarabu na waislam chimbuko lake ni kuweko watu wasiostahiki kuwa viongozi. Hili litakwisha kadiri siku ziendavyo.

Na Mwenyezi Mungu anawajua sana maadui zenu; na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mlinzi na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa msaidizi.

Mungu anajua na sisi tunajua vile vile kuwa Mayahudi na wanaowategemea ni maadui wa haki na ubinadamu, wala sio jambo lililojificha kwa yeyote kuwa dola ya Israel ni nembo ya uovu ya kimataifa, lakini wengi wetu hawawajui vibaraka wanafiki.

Kwa sababu wao wanajificha kwenye nguo ya watu wema na kuwakanganya watu duni. Na iko siku watafichuka na Mwenyezi Mungu atawafedhehesha na kuing'oa mizizi yao kwa mikono ya waumini na wakom- bozi.

Miongoni mwa Mayahudi wako ambao hugeuza maneno kutoka mahali mwake.

Aya zilizo katika mwelekeo huo ni kama hizi zifuatazo: "Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa ajili ya uongo wanasikiliza kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia; hugeuza maneno kutoka mahali mwake." (5:41) "… Wanasikia meneno ya Mwenyezi Mungu kisha wanayageuza baada ya kuwa wameyafahamu …" (2:75)

Ni sawasawa na walivyolifanyia azimio la Umoja wa Mataifa la ulazima wa Israel kuondoka sehemu za Waarabu wanazozikalia kwa mabavu walizozivamia tarehe 5 June 1967 na wakaliita wajibu wa ushirikiano pamoja na Waarabu2

Maneno yoyote yasiyoafikiana na makusudio maovu wanayabadilisha na mahali mwake hata kama wakijua na kufahamu kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mwanzo waliibadilisha Taurati; mahali pa Aya ya uadilifu na rehema wakabadilisha na kuwa unyang'anyi na dhuluma na kuwaua wanawake na watoto.

Mwenye Tafsiri Al-manar, katika kufasiri Aya hii, amesema: "Wamethibitisha wanavyuoni kugeuzwa kwa vitabu vya agano la kale na jipya kwa ushahidi mwingi." Katika kitab Idh'harul-haq cha Sheikh Rahmatullah (wa India) kuna ushahidi mia moja wa kugeuzwa kimaandishi na kimaana.

Kisha akataja mwenye Al-manar baadhi ya ushahidi huo katika Juz,5 Uk. 141 chapa 1328 A.H. Sheikh Jawad Al-balaghi naye akatunga kitabu madhubuti kilichokusanya maudhui haya, alichokiita Rihlatul-madrasiyya; na kimechapishwa mara kadhaa. Mtume (s.a.w.) aliwapa Mayahudi wa Hijaz (Madina) mwito wa kuifuata haki na kuacha kuyabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, lakini wakaendelea kuwa na inadi; na husema tumesikia; na tumeasi; na sikiza bila kusikilizwa; Yaani hutasikilizwa wala kuitikiwa mwito wako unaotulingania. Hilo si ajabu kwa watu wenye asili ya shari na chimbuko la ufisadi.

Na (husema) Raina kwa kupondoa ndimi zao na kuitukana dini.

Wafasiri wamesema kuwa Mayahudi walisema Raina wakiwa hawakusudii maana ya dhahiri ya tamko hili ya kuwachunga. Isipokuwa walikusudia ru'una yaani upumbavu. Na jambo hili ni kupotosha na kuitusi dini. Yamekiwshatangulia maelezo zaidi ya tamko Raina katika kufasiri Aya 104 ya Sura ya Al-Baqara.

Lau kama wao wangesema: Tumesikia na tumetii, na usikie na utuangalie, ingelikuwa ni heri kwao na sawa zaidi.

Kwa kuwa kauli hiyo ni ya sawa zaidi na bora na salama zaidi ndipo wakaiacha na wala wasiiseme.

Katika kufasiri Aya hii, Arrazi anasema: Maana ya kwamba wao ni sawa lau wangelisema: Tumesikia na tumetii, badala ya kusema: Tumesikia na tumeasi. Kwa sababu wao wanajua ukweli wako. Na badala ya kusema: Na sikiza bila kuzikizwa, wangesema na sikia tu. Vile vile badala ya kusema kwao Raina waseme Undhurna; yaani tupe muda kidogo ili tukufahamu; lau wangeliyasema yote haya ingelikuwa bora na sawa.

Lakini Mwenyezi Mungu amewalani kwa kufuru zao.

Na kuifanyia inadi haki na kung'angania batili, na laana ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake na machukivu yake.

Basi hawaamini ila wachache tu.

Tangu enzi na enzi watu kutoka mataifa mbali mbali na dini mbalimbali wameingia katika Uislamu kwa makundi, isipokuwa mayahudi tu. Walisilimu wachache sana; kama vile Abdillah bin salam na baadhi ya wafuasi wake. Bali wao mayahudi waliupiga vita uislam na waislam na bado wanaendelea kuufanyia vitimbi kwa nyenzo zote. Hii ni dalili kubwa kuwa uislamu ni haki na kweli. Jambo la kushangaza ni kwamba viongozi wa uislam na wanaoutolea mwito, hawakuutolea dalili utukufu wa Uislam na utu wake kwa uadui wa Mayahudi waliosema; "Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba." (5:64) Uadui wao ni kwa uilsam na kila mwenye kusema: "Lailahailla Ilah."
Enyi mliopewa Kitab! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha mliyonayo nyinyi.

Kwa dhahiri msemo unawakusanya mayahudi na manaswara, kwa vile wote ni watu wa Kitab. Imesemekana kuwa msemo unawahusu mayahudi kwa kuangalia mfumo wa maneno. Makusudio ya tuliyoyateremsha ni Qur'an tukufu, kwa sababu ndiyo inayosadikisha Taurat, kama ilivyoteremshiwa Musa (a.s.) na Injil, kama ilivyoteremshiwa Isa (a.s.)

Mtume (s.a.w.) aliwapa mwito, mayahudi, wa kuingia kwenye uislam kwa kuuzingatia kuwa ni haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Akawapa dalili na hoja kila mara. Lakini wapi! Haki na hoja zake si chochote kwa mayahudi. Dini yao ni faida na mali tu; na hawatapata faida ya haraka haraka katika uislam wala katika Taurat, isipokuwa faida na utajiri wa haraka haraka wataupata katika ulanguzi, riba, kunyang'anya, kughushi, utapeli, umalaya, kamari, kuleta fitina, vita na mengineyo.
Kwa ajili hiyo ndio wao wamekua msitari wa mbele katika uwanja huu; na Mtume anajua fika hali hii, lakini aliwalingania ili kutimiza hoja tu: "… Na sisi si wenye kuwaadhibisha mpaka tuwapelekee Mtume …" (17:15)

Kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni.

Katika tafsir ya Aya hii, tumeona tafsir nne zenye kupingana. Yenye nguvu tuonavyo ni ile ya Sheikh Muhammad Abduh ambayo kwa ufupi ni kwamba kugeuza ni kinaya cha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawapofusha njia wasijue pa kuelekea kwenye makusudio yao; sawa na wale wanaorudi nyuma kila wanapotaka kwenda mbele.

Au tukawalaani kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi).

Watu wa Sabato ni watu miongoni mwa Mayahudi waliobadilisha dini na wakapetuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo akawafedhehesha na kuwaadhibu duniani kabla ya akhera. Tumeyafafanua hayo katika sura Baqara. (2:65)

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anawakemea kuwa kama hawatajiepusha na upotevu, kupoteza na kubadilisha basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafedhehesha kama alivyowafedhehesha mababu zao.

Kwenye tafsiri nyingi ikiwemo Tafsiri ya Arrazi, Majmaul-bayan na Bahlul-muhit nimesoma jumla ninayoinukuu hapa: "Hapana budi wafutwe Mayahudi kabla ya Kiyama," Amin!

Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima iwe ni yenye kufanywa.

Hakuna wa kupinga hukumu yake wala kuvunja amri yake ambaye hukiambia kitu 'kuwa' kikawa. Ewe Mwenyezi Mungu! Liharakishe jambo litakaloifanya dini yako iwe juu na watu wako wawe na nguvu.

إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ ۚ وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا {48}

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kufanyiwa mshirika, lakini husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hakika amezusha dhambi kubwa.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنْفُسَهُمْ ۚ بَلِ اللَّهُ يُزَكِّي مَنْ يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا {49}

Je, huwaoni wale ambao hujitakasa nafsi zao? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, nao hawatadhulumi wa hata kilicho kwenye uwazi wa kokwa ya tende.

انْظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِ إِثْمًا مُبِينًا {50}

Tizama jinsi wamzuiliavyo Mwenyezi Mungu uongo. Na latosha hilo kuwa ni dhambi iliyo wazi.
  • 1. Hapo ilikuwa ni mwaka 1968
  • 2. Maulama wa Kiislamu wametunga vitabu vingi kuhusu muujiza wa Qur’an na wakataja aina nyingi za miujiza, lakini hawakutaja jinsi Qur’an ilivyoeleza hakika ya Mayahudi, ambapo huo nao ni Muujiza