read

Aya 53-55: Hawawapi Watu Hata Chembe

Maana

Bado maneno yako kwa mayahudi. Mwenyezi Mungu katika Aya ya 44 amewataja kwa upotevu na upotezaji; katika Aya 45 uadui wao kwa waislamu katika Aya ya 46 kwa kugeuza maneno; katika Aya 49 kwa kujitukuza; katika Aya 50 kwa uzushi na katika Aya ya 51 kwa inadi, ukaidi na kuboresha ibada ya sanamu kwa unafiki.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawataja kwa ubakhili:

Au wao wana fungu katika Ufalme? Basi hapo wasingewapa watu hata kitobwe cha kokwa ya tende.

Maana ni kuwa mayahudi hawana dola wala ufalme. Lau wangelikuwa na sehemu ya ufalme, wangeliwazuilia watu wote heri na wasingelimwachia yeyote kitu; hata kiasi cha kitobwe cha kokwa ya tende kilicho kidogo sana kisichotumika.

Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. Walikuwa na wanaendelea kuwa hawawezi kuona neema ya Mwenyezi Mungu kwa mja yeyote miongoni mwa waja wake ila hujaribu kuiondoa kwa njama au kwa riba au kwa kudanganya kwa binti zao na wake zao. Na wakipata nguvu kidogo hunyang'anya na kumwaga damu.

Kuanzia siku walipovamia ardhi ya Palestina mwaka 1948, waliwatoa wazalendo nchini mwao baada ya kuwachinja wanawake na watoto kila mahali.

Na mnamo mwaka 1967 waisrail, kwa kusaidiwa na wakoloni, walivamia sehemu nyingine ya ardhi ya waarabu. Kikakaririka kitendo chao cha kwanza, cha kuua na kufukuza. Hili sio geni katika historia yao na tabia zao.

Waarabu wametawala na ukaendelea utawala wao miaka kadhaa; ukaenea mashariki na magharibi; na mayahudi walikuwa ni miongoni mwa raia zao; wakafanya uadilifu kwa wote na kuwafanyia wema mayahudi na watu wa dini nyinginezo; mpaka wakasema watunzi wa kimagharibi; kama vile Gustav Lebon: "Haikujua historia utawala wenye huruma zaidi ya Waarabu." Wameshuhudia kama hivyo wengineo "chombo humimina kilicho nacho" anasema Ibin Swafiy.

Itakuwa ni vizuri kunakili aliyoyataja mwenye Al-amanar wakati wa kufasiri Aya hii, katika mwaka wa 60 wakati Palestina ilipokuwa katika utawala wa dola ya Uthmaniya, Ninamnukuu: "Maana yanayopatikana katika Aya hii, ni kwamba

hawa mayahudi ni watu wachoyo na wabakhili sana, wanaona tabu kunufaika mwengine yeyote kutokana nao. Wakiwa na utawala wanawazuilia watu was- inufaike hata kidogo, japokuwa ni kitu kipuuzi tu. Basi kwa nini isiwe uzito kwao kutokea Mtume wa kiarabu (Muhammad) ambaye ana milki wakiwemo mayahudi?

“Sifa hii bado wanayo hadi leo. Ikiwa juhudi zao za kuunda serikali katika Palestina zitafanikiwa, basi watawafukuza waislamu na wakristo na hawatawapa hata kitobwe cha kokwa ya tende. Dalili ziko kwamba wanajaribu kumiliki ardhi takatifu na kuwazuia wengine na sababu zote za kupata riziki. Wameweka akiba ya mali nyingi sana kwa ajili ya hilo. Kwa hiyo ni wajibu kwa serikali ya Uthmaniya kutowapa nafasi mayahudi katika Palestina wala wasiwaache wakamiliki ardhi na kuhamia kwa wingi. Kwani hilo lina hatari kubwa.”

Mwenye Tafsir Al-manar anasema Aya haithibitishi wala kukanusha kutawala mayahudi Palestina, isipokuwa inabainisha tabia watakayokuwa nayo lau watatawala Palestina.

Haya ndiyo aliyoyasema ulama katika maulama wa Kiislam kuhusu tafsiri ya Aya hii. Ameisema miaka arobaini kabla ya kupatikana serikali ya Israel kati- ka Palestina. Hii haifahamishi kitu zaidi ya kufahamisha ukweli wa Nabii Muhammad (s.a.w.) katika Utume wake na ujumbe wake, pale alipotoa habari kwa Wahyi wa Mwenyezi Mungu kabla ya zaidi ya miaka 1300, kwamba mayahudi lau watamiliki na kutawala wangelikuwa na yale yaliyotokea mwaka 1948 na 1967.

Je, ambaye Mwenyezi Mungu ameufungua moyo wake kwa uislam akawa yuko katika nuru itokayo kwa Mola wake (ni sawa na mwenye moyo mgumu)? Basi adhabu kali itawathubutukia wale wenye moyo mgumu wasimkumbuke Mwenyezi Mungu. Hao wamo katika upotevu ulio wazi (39:22)

Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake?

Hii nayo ni sifa nyingine katika sifa za mayahudi, hasadi. Makusudio ya watu hapa ni Mtume Muhammad (s.a.w.) na waumini walio pamoja naye. Na hasadi yao mayahudi ni kutokana na dini ya haki aliyopewa Muhammad na waumini na kumakinishwa katika ardhi.

Mayahudi waliposhindwa kuizuwia neema hii kwa waislamu, waliungana na washirikina dhidi ya waislam, wakaenezea propaganda dhidi ya uislamu na Mtume wake. Hatimaye uovu ukawazungukia wao na wakafukuzwa Hijaz kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

Basi tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa Ufalme mkubwa.

Makusudio ya Kitabu ni Zabur ya Daud, Taurat ya Musa na Injil ya Isa. Hekima ni Utume na elimu: maana yake kwa nini mnamhusudu Muhammad (s.a.w.) na waarabu kwa sababu ya Utume na kumakinika katika nchi? Mwenyezi Mungu amekwishawapa nyinyi mfano wa hayo katika waliopita; kama vile Yusuf, Daud na Suleiman.

Katika wao kuna waliomwamini na katika wao kuna waliojiepusha naye.
Wafasiri wametofautina katika dhamiri ya 'waliomwamini;' kuwa je ni kumwamini Muhammad (s.a.w.w.), au Ibrahim au Kitabu? Lenye nguvu zaidi ambalo linaafikiana na maana na kusaidiwa na kuzingatia ni kuwa dhamiri inamrudia kila Mtume aliyepewa Kitabu na hekima.

Neno 'kila Mtume' hata kama halikutajwa katika Aya waziwazi, lakini linafahamika kutokana na mfumo wa maneno.

Kwa vyovyote iwavyo, hakuna tofauti kuwa maana ya Aya ni kwamba si jambo geni kwa hao na mfano wao kutomwamini Muhammad (s.a.w.). Kwani Mitume waliotangulia waliaminiwa na kikundi na wakakanushwa na kundi jingine. Na kundi la ukanushaji lilikuwa kubwa; kama asemavyo (s.w.t.): "…Wengine katika wao walikuwa waongofu na wengi katika wao walikuwa mafasiki." (57:26)

Jahannam yatosha kuwaunguza wale wapingao haki.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُمْ بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا {56}

Hakika ambao wamezikufurisha Aya zetu tutawatia motoni; kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waonje adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na Mwenye hekima.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا {57}

Na ambao wameamini na wakatenda amali njema, tutawaingiza katika pepo zenye kupita mito chini yake, ni wenye kudumu milele humo; wana humo wake waliotakaswa na tutawatia katika vivuli vya daima.