read

Aya 74 -76: Wanaouza Uhai Wa Dunia Kwa Akhera

Na wapigane katika njia ya Mwenyezi Mungu ambao huuza maisha ya duniani kwa akhera.

Uzuri wa yaliyosemwa katika kufasiri Aya hii ni haya yafuatayo: "Hakika Uislamu haupigani kwa ajili ya kupata ardhi au kuwatawala wakazi; haupigani kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda na masoko; au kwa ajili ya rasilmali zitakazozalishwa katika makoloni.”

Uislam haupigani kwa ajili ya fahari ya mtu, nyumba, tabaka, dola, umma au watu fulani. Isipokuwa unapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwenye ardhi na kumakinika njia yake katika maisha na ili mtu afaidike na njia hii na uadilifu baina ya watu huku ukimwacha mtu awe huru na mwenye hiyari kati- ka itikadi ambayo atakuwa nayo.'

Natamani wakati ninasoma jumla hii (Uislamu haupigani kwa jili ya malighafi ya viwanda) niunganishe na jumla hii: 'na wala si kwa ajili viwanda vipakwe damu ya wasiokuwa na hatia, wanawake na watoto.

Na mwenye kupigana katika njia ya Mungu. Akauawa au akashinda, tutampa ujira mkubwa.

Kila mwenye kuinusuru haki kwa njia ya haki na kufuata amri ya Mwenyezi Mungu peke yake, basi yeye ni mwenye kushukuriwa na mwenye kulipwa; ni sawa iwe ameshinda na akapata ngawira, au ameshindwa.

Wanahistoria, pamoja na kutofautiana misimamo yao, wameafikiana kuwa siri ya kuenea uislam ni itikadi ya Mtume (s.a.w.) na sahaba, kwamba wao ni wenye kupata faida katika hali yoyote, ya kuuliwa au kuua. Ikiwa ni kuuawa, basi mwelekeo ni peponi; au ikiwa ni kuua itakuwa tamko la haki limeinuka, na hili ndilo walilolitaka; kuongezea imani kwamba ajali yao ikifika haichelewi hata saa wala haizidi. Imani ya mtu ikifikia hatua hii hawezi kusimamishwa na kizuizi chochote.

Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa katika wanaume na wanawake na watoto.

Mtume (s.a.w.) alihama kutoka Makka kwenda Madina, na walihama pamoja naye wale walioweza na wakabakia wenye kushindwa, wakiwemo wanaume wanawake na watoto. Nao walikuwa wakipata adha kubwa kutoka kwa washirikina kwa ajili ya dini yao; na wala hawakuweza kujikinga wala kupata usaidizi. Kwa ajili hii ndio Mwenyezi Mungu akawaita 'wanaoonewa'. Walipokuwa hawana la kufanya, walimwelekea Mwenyezi Mungu na kusema:

Ewe Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie mlinzi kutoka kwako.

Mwenyezi Mungu ameifanya misukosuko ya wanyonge ni njia ya kuwahimiza jihadi waislam kuwaokoa ndugu zao wa dini, jamaa wanyonge walibakia Makka mpaka mwaka wa ushindi Mtume alipoingia Masjidul-haram wakiwa washindi, vigogo vya ushirikina vikasalimu amri na masanamu yakavunjwa. Uislamu ukatukuka na akawaneemesha wale walio wanyonge katika Makka na kuwafanya watukufu.

Wale walioamini wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na walioku- furu wanapigana katika njia ya shetani.

Katika Aya 71 Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kutoka kwenda vitani vikosi au wote; katika Aya 74, ameamrisha kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; katika Aya 75, amewahimiza kuwakomboa wanaoonewa. Katika Aya hii amegawanya wapiganaji kwenye mafungu mawili; waumini wanaopigana kwa ajili ya haki na uadilifu, na makafiri wanaopigana kwa ajili ya kutawala, kunyang'anya, na kudhulumu.

Hawa ndio wasaidizi wa shetani; na Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini wapigane na kuwatangazia vita na kuacha kufanya mapatano nao kwa namna yoyote ile. Kwa sababu kuwamaliza ndio heri na utengeneo wa ubinadamu, na kupatana nao ni shari na ufisadi.

Kwa ufupi ni kwamba Aya zote tulizozielezea na nyinginezo zinazohusu vita zina lengo moja tu, uimara na uthabiti katika kuwapiga vita wabatilifu na wenye kutaka kujichukulia faida. Aya za Jihadi zinatofautiana katika mfumo na ibara tu, lakini lengo ni moja.

Basi piganeni na marafiki wa shetani; hakika hila za shetani ni dhaifu.

Dhahiri ya Aya hii, ni kwamba wenye haki daima watawashinda wabatilifu, lakini aghlab hali inakuwa kinyume; je kuna siri gani?

Umetangulia mfano wa swali hili na jibu lake kwa ufafanuzi katika kufasiri Aya ya (3:137) kifungu cha Balaa la June. Lakini hapa tutajibu kwa mfumo mwingine, tuliojua kutokana na hotuba ya Imam Ali (a.s.) katika Nahjul-bal- agha.

Ufupi wa jibu ni kuwa vijasumu vibaya haviishi na kukua isipokuwa kwenye takataka na uchafu. Hivyo hivyo shetani hapati mahali pa kutekeleza hila zake isipokuwa penye jamii mbaya. Hapa maandalizi yake hupata nguvu na kujaza nguvu zake. Katika kauli yake Imam, inadhihiri kuwa umuhimu wa Iblis unafaulu pale wanapokuwa katika jamii mafukara wenye shida na matajiri wajeuri. Imam anasema hivi:

"Yafahamu vizuri haya! Ikiwa silaha ya shetani itakuwa na nguvu, vitimbi vyake vikaenea na uwindaji wake ukawa mwepesi tupa jicho lako popote unapotaka katika watu.

Je, utaona zaidi ya fakiri mwenye mashaka au tajiri aliyebadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kuwa ukafiri au bakhili aliyefanyia haki ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio ubakhili! au jeuri ila ni kama kiziwi Wako wapi wabora wenu na wema wenu? Wako wapi waungwana wenu na watoaji wenu?

Wako wapi wanaochunga haki katika chumo lao? “- mpaka kufikia pale aliposema - “kwa hali hii ndio mnataka kuwa karibu na Mwenyezi Mungu katika nyumba ya utukufu wake, na muwe ni watukufu wa vipenzi vyake mbele zake? Awalaani Mwenyezi Mungu wanaoamrisha mema na kuyaacha, na wenye kukataza mabaya na huyafanya."

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا {77}

Je, huwaoni wale ambao wameambiwa: Zuieni mikono yenu, na msimamishe Swala na mtoe Zaka. Walipolazimishwa kupigana, mara kundi moja katika wao wakawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu au kwa hofu zaidi; na wakasema: Ewe Mola wetu! Kwa nini ukatufaradhia vita usituahirishie muda mchache! Waambie: Starehe ya duniani ni chache, na akhera ni bora kwa wenye kumcha Mungu wala hamtadhulumiwa hata kidogo.