read

Aya 84: Haikalifishwi Ila Nafsi Yako

Maana

Basi pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu; haikalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize waumini.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja katika Aya 77 kuhusu wale walioogopa kupigana wakasema; "Ewe Mola wetu kwa nini ukatufaradhia vita…"

Na katika Aya ya 81 wakadhihirisha twaa na kuficha uasi wakasema 'Tunatii' na wakala njama dhidi ya yale waliyoyasema, Akataja katika Aya ya 83 wale waliotangaza habari za vita na siri zake. Baada ya kutaja yote hayo ndipo akamwamrisha Mtume wake kupigana jihadi, kuitetea haki na kuwahimiza waislamu kupigana jihadi pamoja naye na kuachana nao wale walioachana naye. Kwa sababu yeye hana jukumu wala kukalifishwa na matendo ya mwingine; isipokuwa matendo ya nafsi yake tu. Hii ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Haikalifishwi ila nafsi yako tu.

Siyo maana yake kuwa pigana peke yako tu, kama hakupigana pamoja na wewe yeyote; kama ilivyosemwa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amemkataza Mtume na waislam kupigana, wakati wa mwanzo mwanzo wa kutanganza dini;

na aliwaamrisha wasubiri na kuvumilia maudhi ya washirikina walipokuwa Makka. Kwa sababu kupigana wakati huo kulikuwa ni sawa na kujiua. Na hakuwamrisha jihadi ila baada ya kuhama kwenda Madina; wakawa sasa wanaweza kukabiliana na adui. Sasa ikiwa hali ni hiyo, itakuwaje Mtume aam- rishwe kupigana akiwa peke yake.

Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulizi ya waliokufuru.

‘Huenda’ hapa ni ya uhakika, kwa sababu ni katika maneno ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu havunji ahadi. Makusudio ya ‘waliokufuru’ ni wakuu wa Kiquraish ambao wamemtoa Mtume (s.a.w.) Makka na kuandaa jeshi la kumpiga vita mara nyingi. Na Mwenyezi Mungu alitekeleza ahadi yake, alimnusuru mja wake na akavishinda vikosi vya washirikina akiwa peke yake.

مَنْ يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُنْ لَهُ نَصِيبٌ مِنْهَا ۖ وَمَنْ يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُنْ لَهُ كِفْلٌ مِنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُقِيتًا {85}

Mwenye kuunga mkono jema, hupata fungu katika hayo, na mwenye kuunga mkono baya hupata hisa katika hayo; na Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.

وَإِذَا حُيِّيتُمْ بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا {86}

Na mnapoamkiwa kwa maamkuzi, basi itikieni kwa yaliyo bora au mrejeshe hayo hayo; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila jambo.

اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّهِ حَدِيثًا {87}

Mwenyezi Mungu hapana Mola ila Yeye. Kwa yakini atawakusanya siku ya Kiama, halina shaka hilo na ni nani msema kweli katika maneno kuliko Mwenyezi Mungu?