read

Aya 88-90: Imekuwaje Kuwa Makundi Mawili Katika Habari Ya Makafiri

Maana

Mna nini nyinyi mmekuwa makundi mawili katika habari ya wanafiki.

Aya hii ilishuka kuwahusu wanafiki waliobaki katika mji wa Makafiri na wala wasihame kwenda Madina, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mpaka wahame." Kwa sababu Hijra (kuhama) inakuwa ni kutoka mji wa ukafiri kwenda kwenye mji wa uislam tu. Na kabla ya kutekwa Makka, mji wa Madina pekee ndio uliokuwa mji wa uislam.

Dhahiri ya Aya hii ni wazi kuwa hukumu ya aliyekuwa mnafiki, akabaki katika mji wa ukafiri sio hukumu ya mnafiki anayekaa katika mji wa kiislamu. Kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameamrisha kuuawa hao na kuwateka, kinyume cha hawa.

Kabla ya kushuka amri hii Masahaba walitofautiana, wakagawanyika makundi mawili kuhusu hukumu ya wanafiki ambao wamebaki kwenye mji wa ukafiri.

Kundi moja likaonelea kuwa ni lazima kuvunja uhusiano nao na kuacha kuwasaidia na chochote, tena kuwatangazia vita; sawa na aliyedhihirisha ushirikina na uadui kwa waislamu. Kundi jingine likaonelea kuweko kuvumiliana kuwasamehe na kuwafanyia muamala wa waislamu.

Inaonyesha kuwa Mtume (s.a.w.) alinyamaza kuhusu tofauti hizi mpaka Mwenyezi Mungu alipompa ufumbuzi kwa kusema kwake: “Mna nini nyinyi mmegawanyika makundi mawili katika habari ya wanafiki.”

Yaani haitakikani mtofautiane kuhusu mambo yao, bali ni juu yenu kuwa na kauli moja ya kutovumiliana nao kwa hali yoyote ile; na Mwenyezi Mungu akabainisha sababu ya hilo kwa kusema kwake:

Na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa yale waliyoyachuma.

Yaani amewarudisha kwenye hukumu, ya makafiri wanaopiga vita, ya kujuzu kuwaua na kuwateka. Kwa sababu hao ni kama kafiri anayepiga vita tu, au wana madhara zaidi kwa kubakia kwao kwenye mji wa ushirikina ambao hana faida nao isipokuwa adui wa uislamu.

Upotevu

Je mnataka kumwongoza ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha kupotea.

Hii inafahamisha kwamba lile kundi lililotaka kuwavumila lilikuwa na matumai- ni ya kuwa hao wanafiki watarudi kwenye uongofu, Mwenyezi Mungu akaikata tamaa yao kwa kusema:

Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea hatampatia njia.

Unaweza kuuliza: Kwanza Mwenyezi Mungu -uliotukuka usemi wake - ameeleza kwamba Yeye amewageuza hao wanafiki kwa sababu ya kuchuma kwao na kuchagua kwao kubaki katika mji wa makafiri, kisha tena anasema kwamba Yeye ndiye aliyewapoteza. Kwa hiyo upotevu ameutegemeza kwake baada ya kuutegemeza kwao. Sasa kuna wajihi gani katika kukusanya yote mawili?

Jibu: Makusudio ya aliyeachwa kupotea na Mwenyezi Mungu sio kuwa ni kuumba upotevu kwao, la isipokuwa ni kwamba mwenye kukengeuka na njia ya haki na uongofu kwa matakwa yake akifuata njia ya batili na upotevu kwa hiyari yake, basi Mwenyezi Mungu ataachana naye na atamwacha na mambo yake.

Hapana mwenye shaka kwamba mtu anayeachiwa na Mwenyezi Mungu, hatapata njia ila ya upotevu. Maana haya ndiyo yanayooana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "… Na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa yale waliyoyachuma."

Kwa ufasaha zaidi ni kwamba kila mwenye kufuata njia ya haki, hakika Mwenyezi Mungu anamwingiza katika usaidizi wake na kumchunga kwa tawfiki yake: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wale wanaomcha na wale wafanyao mema." (16:128).

Usaidizi huu, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wanaomcha unaitwa uongofu, tawfiki, mapenzi na utegemezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kila mwenye kufuata njia ya upotevu, Mwenyezi Mungu huachana naye wala ham- rudishi kwenye uongofu kwa kumlazimisha. Kuachana naye huku kunaitwa upotevu, utwezaji na kugeuzwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa ibara moja ni kwamba upotevu kutoka kwa Mwenyezi Mungu maana yake ni ukombo sio usawa: na maana ya uongofu kutoka kwake Mwenyezi Mungu ni upole na upangaji wa mambo. Hapana budi kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) inapelekea upole kwa mja wake na kutoepukana naye; sawa na mama asivyoepukana na mwanawe. Ila itakapokuwa mja ndio sababu inay- owajibisha kuepukana na Mwenyezi Mungu kwa njia ya kumwasi; kama mama anavyoepukana na mtoto wake aliyezidi sana kumwudhi.

Wanapenda lau mngekufuru kama walivyokufuru wao mkawa sawasawa.

Kila mtu anapendelea watu wote wawe upande wake. Imetangulia tafsiri yake katika 2: 109.

Basi msifanye katika wao marafiki mpaka wahame katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya kuhama Mtume (s.a.w.) kwenda Madina. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwajibisha kuhama (Hijra) kwenda Madina kwa kila mwislamu ila akishindwa au kupewa idhini na Mtume kubaki kwa masilahi yanayowarudia waislam.

Miongoni mwa Aya zilizohimiza kuhama ni: "Na wale walioamini lakini hawakuhama hamna haki ya kuwalinda hata kidogo mpake wahame …" (8:72)

Siri ya hilo - kama uonavyo - ni kwamba Waislamu walikuwa wachache kabla ya kutekwa Makka. Kama wakitengana huku na huko watakuwa wanyonge na maadui watavamia. Lakini kama wakikusanyika mahali pamoja karibu na Mtume (s.a.w.) watakuwa na nguvu na kuogopewa. Zaidi ya hayo kuna faida nyingi zinazotokana na kuwa pamoja na mshikamano.

Kukaendela kuhama kwenda Madina ni wajibu mpaka ilipotekwa Makka na Mtume, Mwenyezi Mungu akamnusuru mja wake na maadui zake na kuingia watu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi, na kukawa hakuna sababu ya kuhama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema "Hapana kuhama baada ya kutekwa (Makka)."

Wakikataa wakamateni na muwaue popote muwakutapo.

Yaani hao wanafiki kama hawatawacha mji wa ukafiri na kuhama kwenda Madina na kuungana na Mtume na waislamu, basi wakamateni na muwaue popote mtakapowapata.

Wala msifanye katika wao rafiki wala msaidizi.

Yaani achaneni nao kabisa, msiwasaidie wala kuwalinda katika chochote. Unaweza kuuliza: Uislamu ni dini ya uhuru na kuvumiliana na vikundi vyote na watu wa dini zote na sharia yake, ikilinda maisha ya watu, tena watu wote, na haki zao za kimaana na kimaada, bila ya kuangalia rai, maoni yao na itikadi zao. Sasa imekuwaje hapa unaamrisha kuwateka wanafiki na kuwaua popote watapopatikana?

Jibu: Kuna tofauti baina ya makundi na watu wa dini, bali hata na walahidi wanaotangaza maoni yao na itikadi zao kwa watu na wasidhamirie uadui kwa watu wala wasipange njama au kuwasaidia wanaovunja haki; kuna tofauti kubwa sana baina ya hawa na wanafiki ambao wamedhihirisha uislamu na kufichika na neno la uislamu na wakabaki katika mji wa makafiri kwa makusudio ya kuwafanyia vitimbi waislamu, kuwafanyia njama na kuwasaidia maadui.

Kwa hiyo amri ya kuwateka na kuwaua ni malipo ya uadui wao na njama zao kwao. Ama kuvumiliana kwa uislamu na vikundi vingine na watu wa dini nyingine, kunafungamana na msingi wake katika kuuhami uhuru wa kila mtu na kuacha kulazimisha katika maoni na itikadi, iwe ya haki au ya batili, maadamu kila mtu ana mzigo wake, na watu wako katika amani.

Swali la pili lililotokana na jibu la swali la kwanza: Uislam unavumiliana na wanafiki; sawa na unavyovumilia na makundi mengine na watu wa dini nyingine kwa dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake kujipurukusha nao; kama ilivyotangulia katika Aya 63 ya Sura hii: "Basi achana nao na uwape mawaidha…"

Jibu: Aya hiyo ilishuka kwa wanafiki waliokuwa pamoja na Mtume (s.a.w.) Madina. Hawakuwa na wasaa wa kushirikiana na washirikina kwa kuwa mbali nao na kuwa karibu na Mtume na vile vile nguvu za waislamu. Na Aya tuliyonayo (89) ilishuka kwa wanafiki waliong'anga'nia kubakia katika mji wa makafiri kwa ajili ya kuwachimba waislamu. Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume kuwafanyia amani wanafiki wakati waislamu walipokuwa dhaifu wenye wasaidizi wachache. Kisha akamwamrisha kuwaua baada ya

kuwa uislamu una nguvu na wasaidizi (Ansari) wengi; sawa na alivyowaamu- ru kuvumilia kule Makka na kupigana jihadi walipokuwa Madina.

Baada ya kuamrisha Mwenyezi Mungu kuadhibiwa hao wanafiki maadui, ali- wavua kutokana nao sehemu mbili:

Sehemu ya Kwanza ni wale aliowaashiria kwa kauli yake:

Ila wale waliofungamana na watu ambao baina yenu na wao mna ahadi.

Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakusudia kwamba katika hao wanafiki mwenye kukimbilia kwa watu ambao wana mkataba wa amani na waislamu, basi mkim- bizi huyu hatatekwa wala kuuawa kwa sababu yeye - katika hali hii - anakuwa ana salama na waislamu, sawa na aliyekimbilia kwao. Kwa hiyo hawatamwingilia.

Ni vizuri hapa tumnukuu Razi, anasema: "Jua kwamba hii inadhamini bishara kubwa kwa watu wenye imani. Kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliondoa upanga kwa aliyewakimbilia waislamu, basi kumwondolea adhabu huko akhera aliyekimbilia kwenye mahaba ya Mwenyezi Mungu na mahaba ya Mtume wake ni zaidi."

Hapana mwenye shaka kwamba kuwapenda Ahlul bait wa Mtume ni kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema: "Siwaombi malipo yoyote isipokuwa kuwapenda ndugu(kizazi changu) ." (42: 23)

Sehemu ya pili Mwenyezi Mungu amewaashiria kwa kusema.

Au wakawajia hali ya kuwa vifua vyao vina dhiki kupigana na nyinyi au kupigana na watu wao.

Yaani wale ambao wanaona uzito kupigana na waislamu pamoja na watu wao washirikina au kupigana na watu wao pamoja na waislamu, na wakaja kwa Mtume (s.a.w.) kutaka awaridhie wawe katika msimamo usiofungamana na upande wowote, hawa vile vile wataachwa, hawatauawa wala hatatekwa yey- ote katika wao. Kwa sababu hao si wapiga vita.

Mfano bora unaofasiri Aya hii ni ule uliokuja katika Majmaul-bayan kuwa jamaa katika Ashjai walikuja kwa Mtume (s.a.w.) wakamwambia: "Nyumba yetu iko karibu na yako na tunachukia kukupiga vita na kuwapiga vita watu wetu; na tumekuja il tupatane. Akawakubalia na akapatana nao; wakarudi.”

Hakuna nguvu na ukweli wa dalili ya kuwa uislamu ni amani kwa mwenye amani na inampiga vita mwenye kupiga vita, kuliko dalili hii.

Lau Mwenyezi Mungu angelitaka angewasaliti nao wakapigana nanyi.

Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hajiingizi kwa matakwa yake ya Takwin1

Katika mambo ya watu isipokuwa anakusudia kwa kauli yake hii kuwakum- busha waislamu fadhila zake kwao na kwamba inawezekana kuwakusanya wote kwa maadui wa waislamu, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwaondolea hilo kwa wao kuwa na msimamo wa kutofungamana na sehemu yoyote. Kwa hiyo kusema kwake Lau Mwenyezi Mungu angelitaka angewasaliti nao wakapigana nanyi, maana yake ni angeliwafanya wawashambulie na wala asingewajalia na moyo wa kupatana. Na hii si katika matakwa ya Takwin, bali ni matakwa yaTawfiki kama sikosei.

Watakapojitenga nanyi, wasipigane nanyi na wakawapa amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwafanyia njia ya kupigana nao.

"Hakika njia iko kwa wale wanaodhulumu watu na wakawafanyia jeuri katika ardhi pasipo haki …" (42: 42)
"Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia hisani na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya dini wala hawakuwafukuza katika nchi zenu …" (60: 8) "Na wakielekea katika amani, nawe pia ielekee." (8: 61).

Na Aya nyinginezo zinatoa mwito wa mapenzi, udugu na usawa, vilevile kusaidiana katika kila jambo lenye masilahi ya watu kwa njia yoyote. Kuchunga zaidi kwa haki kuliko katika uislamu ni kwamba unazingatia kuutumikia ubinadamu kuwa ndio uti wa mgongo wa dini, bali ndio njia pekee ya kumwelekea Mwenyezi Mungu.

سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَنْ يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِنْ لَمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُبِينًا {91}

Mt awakut a wengine wanataka wapate amani kwenu na wapate amani kwa watu wao; kila wakirejezwa kwenye fitna hudidimizwa humo. Wasipojitenga nanyi na kuwapa amani wala kuzuia mikono yao, basi wakamateni muwaue popote muwakutapo; na hao ndio ambao tumewafanyia hoja zilizo wazi juu yao.
  • 1. Tumezungumzia matakwa ya Mwenyezi Mungu 'Takwin' na Tashrii katika kufasiri (2: 26 - 27)