read

Aya 91: Mtawakuta Wengine

Hakuna Kuuana Wala Vita Katika Uislam

Aya zilizotangulia zimeonyesha namna mbali mbali za wale ambao Mtume (s.a.w.) alipata kutoka kwao aina za vitimbi na uasi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Aya hii inaonyesha sura nyingine ya kundi la watu ambao ni wengi kila wakati na kila mahali. Yaani wale wenye dhambi ambao hawana msimamo isipokuwa kugeukageuka tu; wanaamini msimamo fulani kwa muda tu; kisha wanaukanusha.

Sisi hatukatai kuwa binadamu anageuka kutokana na hali zake, hilo hutokea mara nyingi kama tulivyoeleza katika kufasiri 2: 143, kifungu cha 'Kubadilika hulka na fikra.' Lakini pamoja na yote haya tunaitakidi - kulingana na hali ilivyo - kwamba baadhi ya watu wana tabia ya kigeugeu wanabadilika kutoka hali hii hadinyingine,hatakamawakiwakatikahalimojatu.

Mtawakuta wengine wanataka wapate amani kwenu na wapate amani kwa watu wao; kila wakirejezwa kwenye fitna hudidimizwa humo.

Makusudio ya kurejezwa ni kuitwa, fitna ni ukafiri na kudidizwa ni kuingia. Maana yake ni kuwa kundi hili kila linapoitwa kwenye ukafiri na kurtadi wanakubali na kuwa wabaya zaidi ya kafiri uliyethibiti ukafiri wake. Maelezo mazuri hasa kuelezea hali yao, ni yale waliyoyasimulia baadhi ya wafasiri kuwa, wao walikuwa wanaporudi kwa watu wao, mmoja wao huambiwa sema kombamwiko (mende) ni Mungu wangu na nyani ni Mungu wangu, naye hukubali na kusema hivyo hivyo.

Kadiri wanavyofikia watu hawa katika hali ya kuporomoka, kukosa utu, na kigeugeu baina ya ukafiri na imani, lakini Uislam unawaacha tu na mambo yao, maadam hawajafanya uadui wala vita. Ikiwa watafanya uchokozi na wakapigana, basi uislam unaamrisha kupigana nao popote walipo, ikiwa watakuwa wanaendelea na vita. Haya ndiyo aliyoyakusudia Mwenyezi Mungu kwa kusema kwake.

Wasipojitenga nanyi na kuwapa amani wala kuzuia mikono yao, basi wakamateni muwaue popote muwakutapo.

Hii ni dalili miongoni mwa dalili kadhaa zinazoelezewa na Qur'an na Hadith za Mtume kwamba msingi wa dini ya Kiislamu ni kutoua wala kupigana vita ila kwa kumzuia mwenye kupigana na kueneza ufisadi duniani.

Kwa hivyo basi uislamu umeruhusu vita kwa namna ile ile iliyoruhusu sheria za zamani na za sasa na kukubaliwa na akili zote.
Pamoja na dalili zote hizi, maadui wa uislamu bado wanang'ania kusema kuwa uislam ni dini ya upanga; sawa na yule aliyesema: "Ni mbuzi tu hata kama akiruka."

Angalia Aya iliyotangulia kisha uikutanishe na hii, utaona kila moja inatilia mkazo kuwa vita havikukubaliwa katika sharia ila kwa kujikinga na kuondoa ufisadi.

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَنْ يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَنْ قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَنْ يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِنْ كَانَ مِنْ قَوْمٍ عَدُوٍّ لَكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ ۖ وَإِنْ كَانَ مِنْ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ مِيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِنَ اللَّهِ ۗ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا {92}

Wala haiwi kwa muumini kumwua muumini (mwenzake) ila kwa kukosea. Na mwenye kumwua muumini kwa kukosea, basi amwache huru mtumwa mwislamu na atoe diya kwa watu wake ila watakapoifanya sadaka. Na ikiwa ni mmoja wa watu walio maadui zenu, naye ni muumin, basi ni kuacha huru mtumwa muumini. Na ikiwa ni katika watu ambao baina yenu nyinyi na wao pana ahadi, basi ni diya kwa watu wake na kumwacha huru mtumwa muumini. Na ambaye hakupata basi ni kufunga miezi miwi li yenye kufuatana. Ni kitubio kitokacho kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hekima.

وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا {93}

Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo; na Mwenyezi Mungu amemughadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa.