read

Aya 23-25: Mayahudi Tena

Je huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaitwa kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao, kisha baadhi yao wanageuka wanakikataa.

Wafasiri wanasema: Makusudio ya wale ambao wamepewa sehemu ya Kitabu ni mayahudi. Hapa Mwenyezi Mungu anasema waliopewa sehemu ya kitabu, na wala hakusema waliopewa Kitabu au watu wa Kitabu; kama ilivyo katika sehemu nyingine, kwa sababu mayahudi waliomhoji Mtume (s.a.w.) na akawaita kwenye Tawrat iwahukumie, hawakuwa wamehifadhi Tawrat yote, isipokuwa walihifadhi baadhi tu, kama walivyosema wafasiri wengi. Au walihifadhi matamko tu, bila ya kuzingatia maana yake; kama alivyosema Sheikh Muhammad Abduh.

Wengi wao ni wale ambao wanalingania kwenye kuamini vitabu vya Mwenyezi Mungu na msimamo wa kibinadamu, lakini wanasema tu, bila ya kutekeleza kwa vitendo.Na, wakihojiwa, basi hubabaisha. Mifano ya hao ni mingi sana haina idadi. Kama vile watu walioanzisha vita na kuuwa mamilioni, wanadai kwamba wao ni watetezi wa amani. Miongoni mwazo ni zile dola ambazo zinawakandamiza watu huru na zinajigamba kuamini haki nauadilifu. Mfano mwengine ni mayahudi ambao Mtume (s.a.w.) aliwaita kwenye Kitabu chao Tawrat na kuwaambia nendeni kwenye kitabu hicho, kwani ndani yake mna sifa zangu, lakini walikipa mgongo na kufanya inadi, ndipo ikashuka Aya hii.

Kuna kundi la wafasiri waliosema kwamba Aya hii ilishuka kwa ajili ya yahudi mmoja aliyezini na yahudi mwenzake, na mayahudi wakatofautiana katika suala hilo katika makundi mawili. Kundi moja likataka apigwe mawe mpaka afe na kundi jingine likataka ipunguzwe adhabu hiyo. Mzozo ulipozidi wakenda kwa Mtume kuamuliwa; Mtume akahukumu kuwa apigwe mawe, lakini lile kundi la pili likakataa, ndipo Mtume akawakumbusha Tawrat ambayo imeelezea pia habari ya kupiga mawe mzinifu, lakiniwakakataa.

Kwa vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya hii, kwa hakika ina maana ya jumla na kumgusa yeyote mwenye kutangaza jambo, lakini yeye mwenyewe akajitia hamnazo na kulikataa. Kwa sababu linalozingatiwa ni matendo, sio alama na maneno matupu. Imam Ali (a.s.) anasema: "Hatafuzu kwa kheri ila mwenye kuifanya, wala hatalipwa mtu malipo ya shari isipokuwa mwenye kuifanya."

Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu, na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

Mwenyezi Mungu ameeleza aina nyingi za uovu wa mayahudi katika kitabu chake kitukufu; kama vile kuua kwao mitume, kuabudu ndama, kusema kwao kuwa watakaoingia peponi ni mayahudi tu, kusema kuwa wao ni wana wa Mungu na wapenzi Wake na kudai kuwa moto utawagusa siku chache tu.

Mwenye Tafsir al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba yeye amesema: "Katika vitabu vya mayahudi walivyonavyo hamna kiaga chochote cha akhera."

Imenakiliwa kutoka kwa watu wanaochunguza na kufuatilia mambo kuwa Mayahudi hawaamini akhera, lakini kunukuu kunapingana na kauli ya Qur'an kwa mayahudi: "Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu," na kule kusema kwao: "Hataingia peponi isipokuwa Yahud."

Si jambo la kushangaza kusema kuwa wahenga wa Kiyahudi walikuwa wakiamini akhera; kisha waliofuatia wakageuza na wakaondoa katika vitabu vyao kila linalofungamana na akhera. Katika Tafsir Al-manar akinukuliwa Sheikh Abduh, anasema: "Watafiti wa kiulaya wamethibtisha kuwa Tawrat imeandikwa baada ya nabii Musa (a.s.) kwa miaka nenda miaka rudi. La kushangaza zaidi kuliko yote hayo ni madai ya mayahudi, kwamba Mwenyezi Mungu anawapendelea wao na kwamba Mwenyezi Mungu amewaumba watu wengine kwa ajili ya kuwatumikia wao na kwa masilahi yao, sawa na wanyama. Kwa ajili ya fikra hii ndio wakajiita "Taifa la Mungu lilochaguliwa." Au "Taifa teule la Mungu"

Tukiachilia mbali muhali wa madai haya na kutoingilika akilini, pia tunavyoona ni ndoto na ni kumhukumia Mwenyezi Mungu, kwani hakuna jambo lolote la ghaibu linaloweza kuju- likana bila ya wahyi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na, wahyi umekwisha walaani, kuwafedhehesha na kutaja adhabu yao.

Fedheha hiyo na adhabu itafichuka siku ambayo hawatakuwa na hila yoyote ya kuikinga, kwa hivyo ndipo Mwenyezi Mungu akasema:

Basi itakuwaje tutakapowakusanya siku ambayo hapana shaka kuja kwake na itakapolipwa kila nafsi kwa ukamilifu kile ilichokichuma na wao hawatadhulimiwa.

Thawabu za mtiifu hazitapunguzwa na huenda zikazidi, lakini adhabu haitazidishwa kabisa bali huenda ikapunguzwa na huenda Mwenyezi Mungu akasamehe kabisa.

Mimi nina yakini kabisa kwamba mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu katika dunia yake hii, na wala asimtarajie mwengine amtegemee Yeye tu katika matatizo yote kwa hali yoyote itakayokuwa, akiwa na imani kwamba asiyekuwa Mwenyezi Mungu si chochote isipokuwa ni njia na chombo tu; mwenye kuwa hivi nina yakini kuwa bila shaka atakuta yanayomrid- hisha kwa Mungu hata kama atakuwa ana maovu.

قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {26}

Sema Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote humpa ufalme umtakaye na humwondolea ufalme umtakaye. Na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye. iko mikononi mwako kila kheri. Hakika wewe ni muweza wa kila kitu.

تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَنْ تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ {27}

Huingiza usiku katika mchana na huingiza mchana katika usiku na humtoa aliye hai kutoka aliye maiti na humtoa maiti kutoka aliye hai. Na humruzuku umtakaye bila ya ya hisabu.