read

Aya 266: Je, Mmoja Wenu Anapenda…?

Maana

Aya hii inamwambia kila mwenye kufanya amali na akaifuatishia na jambo litakaloon- doa malipo yake na thawabu zake; kama vile masimbulizi, udhia, kujionyesha, ukafiri na shirk. Hali ya kila mmoja katika hawa ni sawa na mwenye shamba analopatia manufaa yeye na watoto wake, likapatwa na janga kubwa, likaangamia wakati ambapo analihi- tajia sana kutokana na uzee wake na udhaifu wa watoto wake ambao hawajaweza kujitegemea; na wala hana kitu kingine zaidi ya shamba hilo.

Mfano huo ni kwamba mwenye kufanya heri, akaiharibu, siku ya Kiyama atakuwa na haja sana ya thawabu za amali alizozifanya, lakini atakuta amali zake zimekwenda bure, kwa vile alipokuwa akizifanya, hakukusudia radhi ya Mwenyezi Mungu; na wakati huo hataweza kufanya lolote; sawa na mzee aliyeunguliwa shamba lake baada ya kuwa mzee, naye ana watoto wanyonge wanaolihitajia. Kwa mfano huu ndio tunapata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

Na uzee ukamfikia, kisha ana watoto walio dhaifu; mara kimbunga chenye moto kik- ifikie kiungue?

Wafasiri wanasema imehusisha kutajwa mitende na mizabibu, kwa sababu ndio matunda mazuri kwa manufaa ya kiafya, ladha na mandhari pia. Lakini jibu hilo lilikuja katika wakati walioishi ambapo hapakuwa na matofaha, Matunda damu wala Machungwa au miwa. Lau wangelikuwa wakati huu wangelisema kuwa zimetajwa kwa sababu ni matunda bora ya wakati huo. Kwa hali hiyo inatubainikia kwamba hukumu juu ya vitu vya mazingira inapasa iwe kwa kulingana na kufungamana na wakati na mahali.

Unaweza kuuliza: Je, maneno hayapingani kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "kitalu cha mitende na mizabibu." na kauli yake: "Naye humo hupata mazao ya kila namna?" (sasa je ni mitende na mizabibu iliyomo au mazao mengine?)

Jibu: Inawezekana kuwa mitende na mizabibu ndiyo mingi zaidi katika kitalu; au inawezekana vilevile kuwa makusudio ya mazao ni manufaa, kwa maana ya kuwa mwenye shamba anapata manufaa yake yote na faida.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنْفِقُونَ وَلَسْتُمْ بِآخِذِيهِ إِلَّا أَنْ تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ {267}

Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyovichuma na katika vile tulivyowatolea ardhini; wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Mwenye kusifiwa.

الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُمْ بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّهُ يَعِدُكُمْ مَغْفِرَةً مِنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {268}

Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili; na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha utokao kwake na fadhila na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mjuzi.