read

Aya 69-71: Wanajipoteza Wenyewe

Uislamu Ni Dini Yenye Nguvu.

Kikundi katika watu wa Kitabu wanapenda kuwapoteza, wala hawapotezi ila nafsi zao na hali hawatambui.

Makusudio ya kikundi katika watu wa Kitab ni viongozi wa dini zao. Aya hii inaambatana kabisa na wahubiri wa kikiristo. Wao wanafanya kadiri wawezavyo wawaingize waislamu kwenye ukristo. Wakishindwa basi wanajaribu kuwapoteza na kuwatia shaka kubwa katika uislamu, ili wabakie bila dini. Kwa kufanya hivyo wanajifanyia ubaya wao wenyewe bila ya kutambua. Kwa sababu kuudhoofisha uislamu, kama dini inayoelekeza kuweko Mwenyezi Mungu mpangaji mwenye hekima, kunamaanisha kushindwa dini zote na viongozi wake walio na fikra hiyo waki-wemo wakristo. Hii ndiyo tafsir ya hawapotezi ila nafsi zo na hali hawatambui.

Sijui ni kwa nini wafasiri hawayazingatii maana haya pamoja na uwazi wake, ambapo wamesema kuwa makusudio ya watu wa Kitab kujipoteza wao wenyewe, ni adhabu yao kesho kwa sababu ya kujaribu kuwapoteza waislam. Ama Sheik Muhammad Abdu na Razi, wamefasiri kujipoteza wao kuwa ni jaribu lao la kuwapoteza waislam bila kufanikiwa, kwamba hakuna mwislamu yeyote aliyekubali au kudanganyika na upotofu wao.
Lakini usahihi hasa ni tulioueleza. Kudhoofisha uislamu ni kudhoofisha dini zote na watu wake. Vyovyote ilivyo uislamu pamoja na misingi yake una nguvu kiasi ambacho si rahisi kutingishwa na ukristo au na dini nyingine.

Waabudu masanamu, milima na watu wa Kitabu wameingia kwa makundi katika uislamu kwa radhi yao na kukinai, wakiwemo wanavyuoni wao wakubwa. Sijui kama kuna Mwislamu wa kikweli kweli aliyeujua uislamu kiuhakika, ambaye ameuacha Uislamu.

Mwandishi wa kifaransa Henry Descarte anasema katika kitabu chake" Al-Islam sawani wa khawatwir," kifungu cha Uislamu Algeria anasema, ninamnukuu:

"Tumeshuhudia Uislam ukionyesha nguvu zake na uhai wake kwa kupata waabudu mizimu wengi katika Afrika na kuwafanya ni jeshi moja chini ya bendera ya Qur'an na hakuna katika watu Waislamu anayeweza kwenda kwenye dini nyingine."

Kwa mnasaba wa haya tunaleta kisa hiki kizuri cha kuvutia: Katika kumi la atatu la karne ya 20 kundi la wahubiri wa kikristo lilikwenda mji wa Amara ulioko Iraq ambao wakazi wake wote ni waislamu Shia. Jamaa hao walikwenda kwa lengo la kuwageuza wawe wakristo.

Wakaanzisha mashule, na Zahanati, wakafanya matangazo na kuweka hafla wakamwaga mapesa. Mhubiri wao kila alipopanda jukwaani na kuelezea miujiza ya Yesu, Waislamu walikuwa wakipaza sauti"

Salawatullah ala Muhammad wa Ali bayt Muhammad" (Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Muhammad na watu wa nyumba ya Muhammad). Lilipokaririka hilo, walikata tama. Mapesa, shule, zahanati hazikulea manufaa yoyote kwao, wakarudi mikono mitupu.

Enyi watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa ishara za Mwenyezi Mungu na hali nyinyi mnashuhudia?

Makusudio ya Ishara za Mwenyezi Mungu hapa ni dalili za utume wa Muhammad s.a.w.w ukweli wa Qur'an na utukufu wa mafunzo ya kiislamu.

Enyi watu wa Kitab Mbona mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali mnajua.

Makusudio ya haki hapa ni yale yaliyowabainikia watu wa Kitabu kuhusu ukweli wa uislamu na nabii wake. baadhi ya watu wa kitabu walikuwa na bado wako wanaojaribu kuupaka matope uislamu na waislamu, wakimnasibisha Mtume pamoja na Qur'an uwongo na uzushi, kwa mfano wanadai kuwa Muhamamd anawalingania watu wamwabudu yeye kwa sanamu ya dhahabu, kwamba Muhammad alikuwa akipiga ngoma na nzumari na kwamba yeye ana ugonjwa wa kupagawa n.k. Yote ni chuki na kutojiamini.1

Dkt Zakiy Najib anasema katika kitabu chake Ayam fi Amrika kwamba yeye alipokuwa Amerika alihudhuria tamthilia iliyojaa dharau na kebehi kwa Quran na Uislam. Hiyo ndiyo nchi iliyoendelea ambayo inadai kuwa inabeba nembo ya dini na huku inatupa makombora kwa wanyonge kwa madai ya kupiga vita ulahidi.

وَقَالَتْ طَائِفَةٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنْزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {72}

Kikundi katika watu wa kitabu kilisema: Yaami nini yale waliyoteremshiwa wale walioamini mwanzo wa mchana na yakataeni mwisho wake, huenda wakarudi nyuma.

وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَنْ تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّهِ أَنْ يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِنْدَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ ۗ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {73}

Wala msimwamini ila yule anayefuata dini yenu. Sema hakika uongozi hasa ni uongozi wa Mwenyezi Mungu. Kuwa atapewa yeyote mfano wa mliyopewa nyinyi au wawahoji mbele ya Mola wenu. Sema hakika fadhila iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mjuzi.

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ ۗ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ {74}

Humhusisha husisha na rehema yake amtakaye.Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.
  • 1. Upuuzi huu na mwingine uko katika utangulizi wa Kitab cha Decastre akiunukuu kutoka kwa watunzi wengi wa Magharib waliouweka kwa njia ya kupaka matope Uislamu; kisha akaupinga na kuujibu kwa nguvu za hoja. Amesema kweli Mwenyezi Mungu. "Na katika watu wa kitabu yuko ambaye ukimwamini na mrundo wa mali atakurudisha na yuko ambaye ukimpa amana ya dinar moja hakurudishii"