read

Aya 75-76: Kuna Waaminifu Na Wahain I Katika Watu Wa Kitabu

Maana

Na katika watu wa Kitabu yuko ambaye ukimwamini na mrundo wa mali atakurudishia katika wao. Na yuko ambaye ukimpa amana ya dinar moja hakurudishii.

Makusudio ni kwamba katika watu wa Kitabu kuna ambao wako katika upeo wa uaminifu, hata ukiwaamini na mali nyingi, basi watatekeleza amana. Na pia wako walio katika upeo wa hiyana hawaaminiki hata kwa dinar moja tu. Umetajwa uaminifu wa mali, kwa sababu ndiyo mtihani sahihi wa kujua ubovu na uzima wa moyo wa mtu.

Hakuna Maisha Ila Kwa Ukakamavu Wa Kutojali Mauti

Isipokuwa ukimsimamia.

Mwenye hiyana hutaka zaidi ya haki yake wala hatekelezi haki ya watu, kwa sababu ni maiti wa dhamiri. Wala hakuna njia ya kuipata haki kutoka kwake isipokuwa kwa kumsimamia, kama alivyosema mwenye hekima kubwa. Maana ya kumsimamia mwenye hiyana mnyang'anyi ni kumsonga na kugombana naye kwa silaha yoyote uliyo nayo. Walikwishasema wahenga: "Uhuru huchukuliwa, wala hautolewi."

Kumsonga mhaini ni faradhi ya lazima; vinginevyo ufisadi ungelienea duniani. Kosa la kunyamaza mdhulumiwa, ni sawa na kosa la dhalimu. Kwa sababu wote wawili wanaandaa kueneza dhulma na ufisadi. Lau dhalimu angelijua kuwa mdhulumiwa ana hisia za kutojali kufa kugombea haki yake, basi asingelidhulumu.

Majaribio yametufahamisha kuwa hakuna haki katika Umoja wa mataifa wala Baraza la usalama isipokuwa kwa kutumia nguvu; na kwamba hakuna maisha katika karne ya ishirini hasa Mashariki ya kati na hasa hasa waarabu, isipokuwa kwa ukakamavu wa kutojali mauti.

Hayo ni kwa kuwa walisema: Hatuna lawama kwa wasiojua kusoma.

Maana yake ni kuwa watu wa Kitabu walijihalalisha mali za waarabu, kwa sababu wao wal- idai kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hatawaadhibu kwa unyang'anyi huo.1

Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu uzushi wao, kwa kusema: Na wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo na hali wanajua. Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu kwa kukusudia, hiyana yake ni kubwa na kosa lake ni ovu zaidi.

Unaweza kuuliza: Mataifa yote na watu wa dini zote, bali hata walahidi pia, kuna waamini- fu na wenye hiyana; wakweli na waongo. Kuna walahidi kadhaa walio wakweli na kutekeleza amana kuliko wanaofunga na kuswali. Sasa kuna wajihi gani wa kuwahusisha watu wa Kitabu na kifungu hiki?

Jibu: Kwanza, katika Aya Mwenyezi Mungu amesema kuwa baadhi ya watu wa Kitab wanataka kuwapoteza, akasema tena wanataka kuamini asubuhi na kukufuru jioni. Na katika aya hizi anabainisha kuwa kuna waaminifu na wahaini. Na hii haimaanishi hakuna wengine wasiokuwa hivyo.
Pili: Inawezekana tuadhanie watu wa Kitabu wote wana hiyana; ndipo Mwenyezi Mungu akaondoa tuhuma hii, kwamba wao ni kama vikundi vingine na watu wa dini nyingine.

Si hivyo, bali anayetimiza ahadi yake na akamcha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu huwapenda wacha mungu.

Ni kuthibitisha yale waliyoyakana watu wa Kitabu waliposema: Hatuna lawama kwa wasiojua kusoma na kwamba wao ni waongo katika madai haya.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuthibitisha njia ya mwenye kujihalalishia mali za watu, anaeleza kuwa mwenye kutekeleza ahadi na akaogopa yaliyoharamishwa, basi yeye ni mwenye kupendeza mbele ya Mwenyezi Mungu. Imepokewa Hadith, Mtume amesema: "Hakuna kitu kilichokuwa wakati wa ujahiliya isipokuwa kiko chini ya wayo wangu, isipokuwa amana; kwani hiyo inatekelezewa mwema na muovu".

Imam Zainul-abidin (a.s.) anasema: "Lau aliyemuua baba yangu Hussein ataniwekea amana upanga aliomuulia baba yangu, basi nitamtekelezea amana yake." Imam Jaffer Assadiq (a.s.) anasema: "Mambo matatu hayana udhuru kwa yeyote: Kutekeleza amana kwa mwema au muovu, kuwatendea wema wazazi wawili wema au waovu na kutekeleza ahadi na mwema au muovu."

Kwa sababu hiyo ndipo mafakihi wa Shia Imamia wakaafikiana kuwa Kafiri akitangaza vita na waislam, ni halali damu yake lakini haijuzu kumfanyia hiyana. Kwa mfano lau alikuwa ametoa mali yake kwa mwislam, ni lazima arudishe amana pamoja na kujua kuwa inajuzu kumuua na kuchukua mali yake, lakini sio ile aliyoi- weka amana.

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ وَلَا يَنْظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ {77}

Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo. Hao hawatakuwa na sehemu yoyote akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao wala hatawatazama siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu iumizayo.
  • 1. Sijui haya mataifa ya Ulaya yanayopora mali ya mataifa ya kiarabu yanatokana na kizazi kilichosema hivyo! Dinari aina ya pesa itumikayo Bara Arabu.