read

Aya 78: Wanapinda Ndimi Zao Kwa Kitabu

Aya hii ni mwendelezo wa Aya 75. Makusudio ya kupinda ni kugeuza. Kuna Aya nyingi zinazoelezea kugeuza kwao maneno ya Mwenyezi Mungu, "Miongoni mwa hizo ni: Mmekifanya kurasa mlizoonyesha baadhi na kuficha nyingi."(6:91) "Baadhi yao walikuwa wakisikia maneno kisha wakiyabadili baada ya kuwa wameyafa- hamu." (2:75)

Mtu atakayeiona Tawrat yao, atakubali kuwa wamezua, ambapo Mwenyezi Mungu amenasibishiwa kula na kupigana hata miereka; kama ambavyo mitume wamenasibishiwa ulevi, na kuzini na mabinti zao. Kugeuza kunathibiti kwa kuongeza au kupunguza; kama kuzidisha katika maandishi au kupunguza. Vilevile kunathibiti kwa kugeuza irabu, kama kumfanya mtendaji kuwa ndiye mtendwa.

Pia kugeuza kunaweza kuthibiti kwa tafsir; kwa kufasiri kiuhakika badala ya kimajazi; mfano mkono wa Mwenyezi Mungu badala ya uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Wafasiri wametofautiana kuhusu aina ya mageuzi iliyokusudiwa katika Aya hii.Sheikh Muhammad Abduh amesema kuwa makusudio ya kugeuza hapa ni kugeuza tafsir na kulipa tamko maana yasiyokusudiwa; akatoa mfano wa hilo kwa neno liliosemwa na Masih (Baba yetu aliye mbinguni) akiwa na makusudio ya huruma na upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, lakini baadhi ya wakubwa wa kikristo wamefasiri kuwa Mwenyezi Mungu ni baba wa Isa (Yesu) kiuhakika.

Tunavyoona sisi katika tafsir ya Aya hii ni kwamba kikundi hicho cha watu wa kitabu kilikuwa kikipindua tamko lenyewe na kuzusha fikra nyingine na kuwafanya watu wafikirie kuwa ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ili wawe na itikadi ya batili.

Kwa hiyo, tamko la kwanza la Kitabu katika Aya ni kinachodaiwa kuwa ni kitabu; na tamko la pili na la tatu ni sifa ambayo. Kukadiri kwake ni wanapinda ndimi zao kwa kinachodaiwa kuwa ni Kitabu ambacho kimegeuzwa, ili nyinyi watu, mkifikirie kuwa kinatokana na Kitabu cha hakika cha asili, na wala sio Kitabu kamwe.

Ama kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na wanasema hayo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu, ni kutilia mkazo kauli yake: na wala hayatokani na kitabu. Imesemekana kuwa hayo ni kutilia mkazo upande wa kuunganisha ujumla juu ya umahusus. Kwa sababu kitabu kinahusika na wahyi ulioteremshiwa Mtume. Ama yale yanayotoka kwa Mungu yanakuwa ni Hadith za Mtume na hukumu ya kiakili.

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَنْ يُؤْتِيَهُ اللَّهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِي مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلَٰكِنْ كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنْتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنْتُمْ تَدْرُسُونَ {79}

Haiwezekani kwa mtu aliyepewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hekima na Unabii, kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. "Kuweni watumishi wa Mwenyeezi Mungu. Kwa kuwa mnafundisha Kitabu na kwa sababu mnakisoma.

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَنْ تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُمْ بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنْتُمْ مُسْلِمُونَ {80}

Wala hatawaamrisha kuwafanya Malaika na manabii kuwa waungu. Je, atawaamrisha ukafiri baada ya kuwa nyinyi waislamu?