Aya 103 – 112: Musa Na Firauni
Muhtasari Wa Kisa
Tumepitia Aya kadhaa zinazoeleza kisa cha Nabii Musa (a.s.) na wa Israel. Sasa tunaeleza kisa cha Nabii Musa (a.s.) na Firauni katika Aya hizi tunazofasiri.
Neno ‘Firauni’ ni msimbo wa wafalme wa Misri wa zamani; kama vile msimbo wa Kaizari kwa wafalme wa Roma, Kisra kwa wafalme wa Fursi (Iran ya sasa) na Najashi kwa wafalme wa Uhabeshi (Ethiopia ya sasa).
Imenukuliwa kutoka kwa wale wanaojishughulisha sana na Historia ya Misri ya zamani, kwamba jina la Firauni aliyekuwa wakati wa Nabii Musa ni Munfitah.
Jina La Mamake Musa Na Vigano
Ama Nabii Musa (a.s.) ni mtoto wa Imran ambaye watu wa Kitab wanamwita Imram. Katika Juz.1 (2:51), tumeeleza kwamba jina la Nabii Musa ni maneno mawili yaliyochanganywa: neno ‘Mu’ lenye maana ya maji na ‘Sa ‘ lenye maana ya mti. Kwa sababu mama yake alimweka katika sanduku, akalifunga kufuli na akalitupa katika mto Nile kwa kumhofia Fir’aun.
La kushangaza ni uzushi wa mgunduzi wa kufuli hii, aliyotumia mama yake Nabii Musa kumfungia mwanawe, kuzusha kigano kilichoenea na kutangaa karne kwa karne na ambacho wamekiamini wapuzi wengi.
Nacho ni kuwa hakuna kufuli yoyote ila hufunguka ikisomewa jina la mama yake Nabii Musa. Kwa ajili hii hawalijui jina hilo isipokuwa watu maalum wenye siri.
Siku moja nilikwenda kwa mtu mmoja katika watu wa dini mwenye jina kubwa kati ya watu wake. Nikamkuta anapekua kwa hima sana mijalada ya kitabu Biharul-Anwar cha Allama Majlisi. Nikamwuliza: “Kwani una nini?” Akajibu: “Ninataka kujua jina la mama yake Nabii Musa.”
Miaka miwili iliyopita, bwana mmoja alinifuata akidhani mimi ni katika watu wa siri na kuniuliza jina la mama yake Nabii Musa. Nikamwambia: “Wewe wajua zaidi kuliko mimi,” lakini hakukubali. Nikamwambia: “Lakini huu ni upuuzi.” Akaona kuwa mimi namuhepa tu, sitaki kumfichulia siri hii. Nilipokata tamaa kabisa ya kumtuliza nikamwambia: “Haifai nikufichulie, kwa sababu sikuamini, utaiba mali za watu.” Basi akaapa kwa kiapo kizito kwamba yeye hataiba lakini mimi nikajifanya simwamini.
Siku zikapita nikaingilia kufasiri Qur’an Tukufu, nilipofika Aya hii nikawa narudia rejea mbalimbali, miongoni mwazo ni kitabu Qasasul–Quran kili- choandikwa na waandishi wane wa Kimisri: Muhammad Ahmad Jadul-Maula, Ali Muhammad Al-Bajawi, Muhamad Abul-Fadhl na Sayyid Shahatih, mara nikaona jina la mama yake Nabii Musa Yukabid (Jochebed) lakini watungaji hawakulinasibisha kwenye chimbuko lake.
Baada ya kutoka nje kidogo, turudie kisa cha Musa na Firauni; kama kilivyokuja katika Aya tulizo nazo. Kwa ufupi maana yake ni kwamba Firauni alikuwa akidai uungu badala ya Mwenyezi Mungu na alikuwa akiwakandamiza WaIsrael.
Mwenyezi Mungu akamtuma Nabii Musa na Harun kwa Firauni. Wakaenda na kujitosa kwenye kikao chake bila ya kuhofia usultani na utaghuti wake. Nabii Musa akamkabili na kumwambia: “Ewe Firauni! Mimi ni Mtume kutoka kwa Mola wa viumbe vyote nimetumwa kwako na kwa kila mpizani; na ninayo yanayothibitisha ujumbe wangu. Sasa waache waisrael na uwape uhuru waende watakapo.”
Firauni akadharau akasema: “Lete hayo yanayothibitisha utume wako.” Nabii Musa akaitupa fimbo yake mara ikawa nyoka. Akaweka mkono wake kwenye mfuko wa kanzu yake alipoutoa ukawa unameremeta kwa weupe, na Nabii Musa hakuwa mweupe bali maji ya kunde.
Watu wa Firauni na halmashauri yake wakasema huyu ni mchawi bingwa. Basi Firauni akawakusanya wachawi. Kabla ya kuanza mazingaombwe yao walimwambia Firauni, “Je, tutapata malipo tukimshinda Musa?” Akasema: “Mtakuwa na malipo na kuwa karibu yangu.”
Wachawi wakaanza kutupa kamba na fimbo zao; mara watazamaji wakaona ni kama nyoka wanaotembea. Nabii Musa akatupa fimbo yake, ikameza yote waliyoyabuni. Wale wachawi wakasilimu na kuamini utume wa Nabii Musa. Firauni akawatishia kuwaadhibu na kuwatesa, lakini hawakurudi nyuma na wakathibiti kwenye imani yao. Riwaya nyingi zimeeleza kuwa Firauni alitekeleza vitisho vyake. Na hali ilivyo inalitilia nguvu hilo.
Firauni akawa anampa Nabii Musa na waliokuwa pamoja naye aina kwa aina za adhabu, lakini Nabii Musa aliendelea na mwito wake kwa Mwenyezi Mungu. waisrael wakampigia kelele Nabii Musa: “Tumeudhiwa kabla ya wewe kutujia na baada ya kutujia pia.” Nabii Musa akawaamuru kuvumilia na kuwapa tamaa ya kufaulu.
Mwenyezi Mungu akawaadhibu watu wa Firauni kwa kahati na dhiki. Akawapelekea mvua ya kuharibu mimea na mazao yao, nzinge waliokula vilivyobakishwa na athari ya mafuriko,
chawa waliouma miili yao na vyura walioharibu maisha yao. Zaidi ya haya yote, maji yao yaligeuka na kuwa damu.
Hapo walifazaika kwa Nabii Musa. Wakamwambia: “Mola wako akituondolea adhabu tutakuwa miongoni mwa walioamini.” Mwenyezi Mungu akawaondoloea adhabu ili nao warejee, lakini wakavunja ahadi na wakaendelea na ukafiri. Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwenye bahari na ikakatwa mizizi ya makafiri. Huu ndio muhtasari wa haraka haraka unaoelezwa na Aya tulizo nazo kuanzia Aya (103) mpaka mwisho wa Aya (137). Sasa tufafanue yanayofahamishwa na Aya hizo.
Maana
Kisha baada yao tukamtuma Musa na ishara zetu kwa Fir’aun na wakuu wake lakini wakazikanusha.
Dhamir ya baada yao inawarudia Mitume watano. Nuh, Hud, Swaleh, Lut na Shuaib. Ishara alizotumwa nazo Nabii Musa ni miujiza inayofahamisha utume wake. Wakuu wa Fir’aun, ni wale watukufu wa watu wake ambao mambo yote yako mikononi mwao, wengine ni kufuata na kunyenyekea tu.
Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wafisadi.
Ambao ni Fir’aun na wasaidizi wake waliozikalia shingo za watu. Mwisho huu utaelezwa katika mfumo mzima wa maelezo.
Akasema Musa: Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume nitokaye kwa
Mola wa walimwengu.
Hivindivyoalivyomwita,“EweFirauni”bilayakumtukuzanakumwadhimisha. Kwa sababu Nabii Musa alikuwa akizungumza lugha ya Mwenyezi Mungu na akafiksha ujumbe wa Mwenyezi Mungu ambao unamfanya mdogo mkubwa yeyote.
Kutokana na hivi ndio tunajua siri ya sera ya watu wema, wakijitukuza kwa mafasiki na kuwanyenyekea kwa udhalili na huruma waumin.
Yanipasa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki.
Hivi ndivyo ilivyo kwa kila Mtume aliyeaminiwa na Mwenyezi Mungu juu ya wahyi na kumchaguwa kuwa ni mjumbe wake.
Nimewajia na dalili wazi itokayo kwa Mola wenu.
Inayofahamisha kuwa mimi ni Mtume kutoka kwa Mola wa walimwengu.
Basi waache wana wa Israel waende nami.
Firauni alikuwa amewafanya waisraili watumwa na kuwatumia katika kazi ngumu. Ndipo Nabii Musa akataka waachiwe huru waende popote watakapo.
Akasema: Ikiwa umekuja na ishara, basi ilete ukiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.
Inaonyesha kuwa Firauni alikuwa akidhani kuwa Nabii Musa ni mwongo katika madai yake, akataka kumfedhesha mbele ya wakuu, akamwambia: “Ilete hiyo hoja kama ni mkweli.” Nabii Musa akamziba mdomo wake kwa hoja mkataa.
Akatupa fimbo yake, mara ikawa nyoka dhahir, yaani nyoka halisi. Hapo Firauni akafazaika, lakini akajikaza kwa vile alikuwa akidai kuwa yeye ni Mungu Mkuu.
Nabii Musa tena akamshutukizia na muujiza wa pili. Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao na mkono wa Nabii Musa ulikuwa rangi ya kahawia, sasa umekuwaje mweupe bila ya ugonjwa wowote?
Fir’aun akahisi unyonge na udhalili, akajiona yuko chini kabisa. Wale waliokaa naye wakatambua hilo kwamba Nabii Musa amewangusha kutoka juu. Wakasema wakuu wa watu wa Firauni: Hakika huyu ni mchawi mjuzi.
Hiyo ndiyo hoja ya mwenye kushindwa nayo ni kutuhumu watu wema. Kisha wakuu wakaendelea kusema:
Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Yaani Nabii Musa anataka kuwaondoa kwenye ufalme. Fir’aun aliposikia hivi akasema: Basi mnatoa shauri gani? Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake kwa sababu ukiwaua, watu watakasirika na utawala wako utakuwa hatarini. Na uwatume mijini wakusanyao Yaani askari Wakuletee kila mchawi mjuzi.
Watu wa Historia wanasema kuwa nchi ya Misri wakati wa Mafir’aun ilikuwa ikichemka na uchawi. Makuhani na waangalizi wa miungu ndio waliokuwa wakiendeleza kazi ya Uchawi. Anasema Aqqad katika Kitabu Iblisi kwenye kifungu cha Maendeleo ya Kimisr:
“Mafirauni wenyewe walikuwa wakikimbilia wachawi kwa kushindana na roho zilizojifiicha. Na tunayo mabaki ya visa vya uchawi ambayo hawakuyachagua wanaokusanya athari, lakini waliafikiana kuwa ni kazi za kichawi.
Walikuwa wakiugawanya uchawi kwenye mafungu: Kuna ule unaosaidiwa na uwezo wa mungu wa kheri dhidi ya mungu wa shari na ule unaosaidiwa na uwezo wa shetani mkubwa dhidi ya shetani mdogo.”
Kuenea uchawi wakati wa Firauni kunatufasiria sisi fimbo ya Nabii Musa na unatilia nguvu msingi unasema kuwa kila mwujiza wa Mtume ulikuja kulingana na aina iliiyoenea wakati wake, ili ushindi uwe mkubwa katika hoja na kukata kila udhuru – hoja mkataa.
Kwa hiyo Nabii Musa alivunja uchawi kwa vile ulienea zama zake.
Nabii Isa akafufua wafu, na Nabii Muhammad akawanyamazisha wanafasihi, kwa lengo hilo hilo.
وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِنْ كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ {113}
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ {114}
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَنْ تُلْقِيَ وَإِمَّا أَنْ نَكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ {115}
قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ {116}
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ {117}
فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {118}
فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانْقَلَبُوا صَاغِرِينَ {119}
وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ {120}
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ {121}
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ {122}
قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنْتُمْ بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكْرٌ مَكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ {123}
لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ مِنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ {124}
قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنْقَلِبُونَ {125}
وَمَا تَنْقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ {126}