read

Aya 113 – 126: Wakaja Wachawi

Maana

Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Tutapata ujira ikiwa tutashinda? Akasema, ndiyo, nanyi hakika mtakuwa miongoni mwa wanaokurubishwa.

Wachawi hawa waliojiuza kwa Firauni dhidi ya Nabii Musa walikuwa wanawakilisha dini katika zama zao. Nao wana mifano kila wakati. Wanauza dini yao na dhamiri kwa kila mwenye kutoa pesa. Siku hizi Wazayuni na Wakoloni wamewanunua wengi wenye kofia na vilemba wakawalipa na kuwashika sawasawa wasaidie ukoloni na unyonyaji kwa kuwavunga watu na kuwapoteza. Wakaanzisha jumuia mbalimbali na vitengo kwa jina la dini kwa lengo hilo. Lakini ni haraka mno kufedheka na kuwa kwenye midomo ya dharau ya kila mwenye mwamko mwenye ikhlasi.

Wakasema: Ewe Musa! Utatupa wewe au tutatupa sisi?

Walimuhiyarisha kuanza au waanze wao kwa kutegemea uchawi wao kuwa watashinda na kutomjali Nabii Musa (a.s.). La kushangaza ni kauli ya Razi, kwamba wachawi walimuhiyarisha Nabii Musa kwa kumheshimu.

Akasema: Tupeni! Akiwadharauwaonauchawiwao.

Walipotupa waliyazuga macho ya watu na wakawaogopesha, na wakaleta uchawi mkubwa.

Kunasibisha kuzuga kwenye macho ya watu ni dalili kwamba uchawi wao si tukio la kweli, isipokuwa ni kuwavunga watu tu.

Kuwaogopesha, ni kwamba wachawi waliwatisha watazamaji na wakaleta uchawi mkubwa katika kuzuga na kupoteza si katika uhakika au hali halisi.

Tukampelekea wahyi Musa kwamba tupa fimbo yako. Mara ikavimeza walivyovibuni. Ukweli ukasimama na yakabatilika waliyokuwa wakiyabuni.

Nabii Musa alihofia wajinga wasihadaike na mizungu ya wachawi na upotevu wao. Mwenyezi Mungu akamfunga mkanda na kumpa wahyi kwamba yuko pamoja naye; na kwamba waliyoyaleta si chochote ni mizungu tu.
Akamwamrisha atupe fimbo. Alipoitupa ikameza yale waliyoyabuni kukabatilika kujifanya kwao ikadhihiri haki machoni kwa wote.

Firauni akaduwaa kwa mshtuko uliompata mbele ya umma wa watu. Amewaleta wachawi kutoka kila pembe ili wakilinde kiti chake na awathibitishie watu uwongo wa Nabii Musa na uzushi wake. Leo mambo yamebadilika kichwa chini miguu juu. Wote wakiwemo wachawi wameamini ukweli wa Nabii Musa na uaminifu wake na kukadhibisha uwongo wa Firauni na hiyana yake.

Kwa hiyo hapo walishindwa wakageuka wakawa wadogo baada ya kiburi kile.

Lau mambo yangeishia hivyo hivyo, kidogo Firauni angelipumua, lakini alishtukiziwa kwa jambo zito na chungu. Na wachawi wakapomoka wakasujudu. Wakasema: Tumemwamini Mola wa waliimwengu (wote), Mola wa Musa na Harun si Firauni aliyewaleta kubatilisha mwito wa Mwenyezi Mungu na wa haki.

UtaulizakunamakusudioganiyakauliyaWachawi‘Molawa Musana Harun’ ambapo ingelitosha tu kusema ‘Mola wa walimwengu’? Jibu: Firauni alikuwa akiwaambia watu:

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ {24}

“Mimi ndiye Mola wenu mkubwa (79: 24)

مَا عَلِمْتُ لَكُمْ مِنْ إِلَٰهٍ غَيْرِي {38}

“Simjui kwa ajili yenu Mungu asiyekuwa mimi” (28: 38).

Lau wachawi wangelitosheka na kusema Mola wa walimwengu, basi Firauni angeligeuza na kujisifu yeye na kusema wananikusudia mimi Mola wa walimwengu. Ndipo wakaikata njia ya majisifu yake na kubadilisha kwake mambo.

Uchawi

Katika Juz.1 (2:103) Tulizungumzia kuhusu uchawi kwa anuani ya ‘Uchawi na hukumu yake’, Tukasema katika tuliyoyasema, kwamba sisi tuko pamoja na wale waonao kuwa uchawi hauna chochote na tukatoa dalili ya hilo. Kuunganisha yaliyopita hapa tunaongezea haya yafuatayo:

Kauli yake Mwenyezi Mungu Wakayazuga macho ya watu ni dalili wazi kwamba uchawi hauna kitu chochote, na kwamba ni ujanja na kiini macho.

Ama kauli yake Mwenyezi Mungu: wakaleta uchawi mkubwa maana yake ni kwamba walifika kikomo cha ujanja na kubadilisha mambo. Maana haya yafafanuliwa na kusisitizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu.

فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِنْ سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ {66}

“Mara kamba zao na fimbo zao zikadhaniwa mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinapiga mbio.” (20:66).

Hazikuwa zikienda hasa, bali ni dhana na mawazo tu. Mtume mtukufu (s.a.w.) amesema: “Mwenye kumwendea mchawi au kuhani na mwongo akamsadiki, basi amekufuru aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu.”

Wafasiri wengi wamesema kuwa wachawi wa Firauni walifanya hila ya kutingisha kamba na fimbo kwa kuziwekea Zebaki ili zitingishike na joto la jua.

Vyovyote iwavyo tunaamini kwa imani isiyo na shaka kwamba mchawi ni mwongo hakuna anayemsadiki ila mpuzi; na kwamba waliyoyafanya wachawi wa Firauni na wanayofanya wahindi na wengineo ambayo yanashangaza, yana sababu bila ya shaka yoyote.
Na sisi ijapokuwa hatujui sababu yenyewe, tunaamini kwa yakini kabisa kwamba uchawi hauwezi kubadilisha kitu, vinginevyo basi mchawi angeliweza kujizuia yeye na madhara na kujinufaisha na kutawala ulimwengu wote kwa kutaka kwake na matabano yake; na angelikuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu katika milki yake Mwenyezi Mungu. Ametukuka kabisa na hayo Mwenyezi Mungu.

Akasema Firauni: Je, mmemwamini kabla sijawaruhusu?

Unaona mantiki hii? Anawataka wamwombe ruhusa katika mambo ya nyonyo zao imani, mapenzi na chuki. Hata mtu ulimwenguni asiutawale moyo wake mwenyewe! Lakini hiyo ni mantiki ya kitaghuti.

Hakika hizi ni njama mlizozipanga mjini ili muwatoe wenyewe, lakini punde mtajua.

Firauni anawaelekezea wachawi tuhuma hizi kuwa kumwamini kwao Nabii Musa hakukuwa kwa hoja na kukinaika, isipokuwa ni hila na hadaa tu walizozipanga pamoja kabla na kwamba lengo la njama hizi ni kuwatoa watawala na kuwavua utawala wao katika Misri.

Firaunialisemamanenohayaakiwaanajuakwambayeyenimwongo katika kauli yake, lakini alitaka kuwababaisha watu akihofia wasimwache yeye wakamwamini Nabii Musa, lakini watu wanajua kwamba wachawi hawakuamini isipokuwa kwa kuona na kukinai. Vilevile watu wanajua kwamba Nabii Musa hakuwa pamoja na wachawi. Kwa sababu Firauni aliwakusanya huku na huko.

Nitawakata mikono yenu na miguu yenu kwa kubadilisha, kisha nitawasulubu nyote.

Kukata kwa kubadilisha ni kukata mkono wa kuume na mguu wa kushoto, na kinyume.

Hiyo ndiyo silaha ya mataghuti katika kuikabili haki. Anasema Masud katika kitabu Muruju-dhahab: “Katika mwaka 59 (A.H.) Muawiya ali- wakusanya watu ili wambai mwanawe Yazid. Akasimama kuhutubu mtu mmoja kutoka Azdi akasema:

“Akifa huyu akimwonyesha Muawiya basi ni huyu, akimwonyesha Yazid. Na atakayekataa basi ni huu, akautingisha upanga. Muawiya akamwambia: “Kaa, wewe ni hatibu bora kuliko watu wote.”

Wakasema: Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu.

Fanya utakavyo hatukujali wewe wala kuua kwako. Sisi tuna yakini ya kukutana na Mola wetu na uadilifu wake.

Kila mwenye kuamini kukutana na Mwenyezi Mungu anakuwa na msimamo huu bali anaona kufa shahidi ni kheri na nyenzo ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu zake. Ama wale ambao wanaoogopa mauti katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanaamini kinadharia tu; ama kimatendo wao wanakanusha.

Na wewe hutufanyii kisasi ila kwa sababu tumeziamini ishara za Mola wetu zilipotujia.

Kauli yao hii ina madhumuni ya kumtisha Firauni. Kwa sababu maana yake ni kwamba wewe hutuchukulii kisasi isipokuwa unamchukulia kisasi Mwenyezi Mungu na Mtume Muhammad (s.a.w.) wake hasa. Kwa sababu hatuna kosa sisi ila kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake Nabii Musa:

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّهُ مَنْ يُحَادِدِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَأَنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ{63}

“Je hawajui kwamba anayeshindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi yeye atapata moto wa Jahanam.” (9:63).

Ewe Mola wetu tumiminie subira. Katika msimamo huu.

Unasifiwa uvumilivu (subira) kwa kuuliwa na kuadhibiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Walimuomba Mungu awaruzuku fadhila hii kwa kuhofia wasilegeze mkanda na kurudi nyuma watakapohisi upanga ukipenya milini mwao.

Na utufishe hali ya kuwa ni waislamu, wanyenyekevu kwako na kwa Mtumewakotukiwaradhinaadhabunamatesokatikanjiayako.

وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ {127}

Na wakasema wakuu wa kaumu ya Firauni: Je, utamwacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na kukuacha wewe na waungu wako. Akasema: Tutawauwa watoto wao wa kiume na tutawaacha hai wanawake wao. Na hakika sisi ni wenye nguvu juu yao.

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ {128}

Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu na subirini. Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu atamrithisha amtakaye katika waja wake na mwisho ni wa wenye takuwa.

قَالُوا أُوذِينَا مِنْ قَبْلِ أَنْ تَأْتِيَنَا وَمِنْ بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَنْ يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ {129}

Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia na baada ya kutujia. Akasema: Huenda Mola wenu atamwangamiza adui yenu na kuwafanya makhalifa katika ardhi aone jinsi mtakavyokuja fanya.