read

Aya 134-137: Ilipowaangukia Adhabu

Maana

Katika Aya iliyotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja aina tano za adhabu alizowaadhibu watu wa Firauni. Na walikuwa kila inapowapata adhabu hutawasali kwa Musa kutaka kuondolewa adhabu hiyo kwa karamu yake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Walikuwa wakijiwekea ahadi wao wenyewe kwa Musa kuwa akifanya, basi wataitikia mwito wa haki. Mwenyezi Mungu naye alikuwa akiwaondolea adhabu kwa muda fulani ili wajiandae na toba na kuwasimamishia hoja. Lakini walikuwa wakivunja ahadi, hawakutekeleza wanayoyasema.

Hapo Mwenyezi Mungu huwateremshia mara ya pili. Tena wanarudia kunyenyekea na kutawasali, na Mwenyezi Mungu huwaondolea. Ikawa namna hii mpaka adhabu ya tano, au jaribio la tano, ndipo akawatesa na kuwatupa ndani ya bahari.

Baada ya muda mrefu kupita tangu kufamaji Firauni na kufariki Musa na Harun, alitokea katika waisrail, Daudi na Suleiman wakafanya dola yenye mipaka mashariki na magharibi.

Lakini haraka sana dola iliyeyuka na Waisrail wakatawaliwa na Ebuchadnezer, wafursi na makhalifa wa Alexandria kisha wa Roma.

وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَهُمْ ۚ قَالُوا يَا مُوسَى اجْعَلْ لَنَا إِلَٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ {138}

Na tukawavusha bahari wana wa Israil na wakawafikia waliokuwa wakiyaabudu masanamu yao; wakaema: Ewe Musa! Hebu nasi tufanyie waungu kama hawa walivyo na waungu. Akasema Hakika nyinyi ni watu wafanyao ujinga.

إِنَّ هَٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {139}

Hakika waliyona hawa yatawangamiza na ni bure waliyokuwa wakiyafanya.

قَالَ أَغَيْرَ اللَّهِ أَبْغِيكُمْ إِلَٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ {140}

Akasema je, niwatafutie mungu badala ya Mwenyezi Mungu, hali yeye ameweafadhilisha juu ya walimwengu?

وَإِذْ أَنْجَيْنَاكُمْ مِنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُمْ بَلَاءٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَظِيمٌ {141}

Na Tulipowaokoa kwa kaumu ya Firaun waliowapa adhabu mbaya wakiwaua watoto wenu wa kiume na kuwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa uliotokea kwa Mola wenu.