read

Aya 138-141: Tuliwavusha Wana Wa Israil

Maana

Na tukawavusha bahari wana wa Israil na wakawafikia waliokuwa wakiyaabudu masanamu yao; wakaema: Ewe Musa! Hebu nasi tufanyie waungu kama hawa walivyo na waungu. Akasema: Hakika nyinyi ni watu wafanyao ujinga.

Baadhi ya riwaya zinaeleza kuwa Musa aliendelea miaka ishirini na tatu akipigana jihadi na Firauni kwa ajili ya Tawhid na kuwakomboa wana wa Israil kutokana ukandamizaji. Wakashuhudia miujiza ya kushangaza iliyodhihiri mikononi mwa Musa.

Mwisho wakaona kupasuka bahari kwa fimbo ya Musa, na jinsi zilivyotokea njia kavu kumi na mbili. Kila ukoo ukawa na njia yake. Vile vile waliona jinsi bahari ilivyofungika kwa Firauni na askari wake.

Yote hayo waliyashuhudia, lakini kabla ya kupita muda walisahau miujiza waliyoiona na macho yao yakawa kwa watu wanaoabudu masanamu, wakamtaka Musa awafanyie sanamu la kuabudu. Walitaka haya wakiwa wanajua kwamba Musa ni mtu wa Mwenyezi Mungu na kwamba umuhimu wake wa kwanza ni mwito wa Tawhid na kupiga vita ushirikina. Vile vile walikuwa wakijua kuwa Mwenyezi Mungu alimwangamiza Firauni na jeshi lake, kwa sababu ya ushirikina wake. Baadhi ya wafisri wanasema; "Lau wao wenyewe wangejifanyia mungu, mshangao ungelikuwa mdogo kuliko kumtaka Mtume wa Mola wa walimwengu wote kuwafanyia mungu. Lakini hao ndio Waisrail!

Hakika yaliyo na hawa yatawangamiza na ni bure waliyokuwa wakiyafanya.

Musa (a.s) alianza kuwajibu watu wake kuwa wao ni wajinga na wapumbavu; kisha akawapa habari kwamba mwisho wa washirikina na waabudu masanamu ni hasara na maangamizi.

Akasema je, niwatafutie mungu badala ya Mwenyezi Mungu, hali yeye ameweafadhilisha juu ya walimwengu?

Imepita tafsiri yake katika Juz.1 (2:47)

Kwa vyovyote kufadhilishwa kwao juu ya Firauni na watu wake hakuhisabiwi kuwa ni fadhila kubwa.

Na Tulipowaokoa kwa kaumu ya Firaun waliowapa adhabu mbaya wakiwaua watoto wenu wa kiume na kuwaacha hai wanawake wenu. Na kati- ka hayo ulikuwa mtihani mkubwa uliotokea kwa Mola wenu.

Umepitamfanowakekatika Juz.1(2:49)

وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ {142}

Na tulimwahidi Musa masiku thalathini na tukayazitimiza kwa kumi; ndipo ikatimia miadi ya Mola wake siku arubaini. Na Nabii Musa akamwambia ndugu yake Harun: Shika mahali pangu katika watu wangu na utengeneze wala usifu- ate njia ya waharibifu.

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنْظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَنْ تَرَانِي وَلَٰكِنِ انْظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ {143}

Na alipofika Musa kwenye miadi yetu Na Mola wake akamsemeza, alisema: Mola wangu nionyeshe nikutazame. Akasema: Hutaniona, lakini tazama jabali, kama litakaa pahali pake ndipo utaniona. Basi Mola wake alipojionyesha kwa jabali alilifanya lenye kuvunjika vunjika, na Musa akaanguka hali amezimia. Alipozinduka alisema: kutakasika ni kwako! Natubu kwako na mimi ni wa kwanza wa wanaoamini.

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُنْ مِنَ الشَّاكِرِينَ {144}

Akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteua kwa watu kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu; basi yashike ninayokupa, na uwe miongoni mwa wanaoshukuru.

وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ مَوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ {145}

Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha na ufafanuzi wa kila jambo. Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako washike mazuri yake zaidi. Nitawaonyesha makao ya wafasiki.