read

Aya 158 – 159: Mtume Wa Mwenyezi Mungu Kwenu Nyote

Maana

Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote.

Aya hii imeshuka Makka katika Sura ya Makka. Inakadhibisha wale waliosema kuwa Nabii Muhammad (s.a.w.) alipokuwa dhaifu, alisema mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu wa Makka na walio viungani mwake, na baada ya kuwa na nguvu, eti ndio akasema mimi ni Mtume wa watu wote. Tumewajibu hao kwa jibu mkataa katika kufasiri Juz.7 (6:92).

Amabaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, hapana Mola ila yeye, ndiye ahuyishaye na ndiye afishaye.

Aya hii na nyingine nyingi inatilia makazo na kusisitiza kuwa hakuna wa katikati baina ya Mwenyezi Mungu na waja wake, na kwamba milki na amri ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.

Kwa hiyo Nabii Muhammad (s.a.w.), ingawaje ni Mtume wa watu wote, wakati wote na mahali popote na ni mtukufu wa viumbe na mwisho wa Mitume na bwana wao, lakini yeye mwenyewe hajimiliki chochote, sikwambii mwingine tena.

Mwenyezi Mungu anasema:

قُلْ لَا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۗ{49}

“Sema sijimilikii nafsi yangu madhara wala kwa manufaa ila apendavyo Mwenyezi Mungu” (10: 49)

Maana haya yamekaririka katika Aya kadhaa, na makusudio yake ni kuwafahamisha waislamu hakika ya Nabii Muhammad (s.a.w.) na kwamba yeye ni mtu kama wao, ili wasijingize sana kwake waislamu kama walivyojingiza Wakristo kwa Bwana Masih (a.s.).

Tamko Lailaha illallah nabii Muhammadu-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Nabii Muhammad ni Mtume wa mwenyezi Mungu) wanalolikariri Waislamu usiku na mchana, linatosha kuwa ni dalili ya kuepukana Waislamu na kujingiza sana, na vilevile kuamini kwao kuwa Nabii Muhammad (s.a.w.) hamiliki jambo lolote zaidi ya Utume na kufikisha (tabligh).

Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyesoma wala kuandika ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni ili mpate kuongoka.

Kusema kwake mfuateni baada ya kusema kwake basi mwaminini, ni dalili kwamba imani tu haitoshi kitu bila ya kuwa na vitendo vinavyofuata Kitab cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake. Rudia Juz.2 (2:212) kifungu ‘hakuna imani bila ya takuwa.’

Uzayuni Na Uyahudi

Na katika kaumu ya Musa kuna umma unaoongoza kwa haki, na kwayo hufanya uadilifu.

Razi anasema: “Wametofautiana kuhusu umma huo, ulipatikana lini, na wapi? Ikasememkana kuwa ni Mayahudi waliomwamini Nabii Muhammad (s.a.w.), kama vile Abdallah bin Salam na bin Suria. Na imesemekana kuwa ni watu waliothibiti kwenye dini ya Nabii Musa bila ya kugeuza, kama walivyofanya wengineo waliozusha mambo.”

Sisi tuko katika upande wa hao wasemao kuwa ni waliokuwa katika wakati wa Nabii Musa, kisha wakaisha, kama linavyodokeza neno lake Mwenyezi Mungu: Na katika kaumu ya Nabii Musa. Ama bin Salam na bin Suria hao wawili wala kumi mfano wao hawawezi kuitwa umma au kundi.

Kwa vyovyote iwavyo, Qur’an katika Aya kadhaa imewapa Mayahudi kila sifa mbaya, na kuiambatanisha historia yao kuwa ya aibu. Kwa hiyo linalofahamika kutokana na kauli, katika kaumu ya Nabii Musa ni kuwa katika desturi yoyote kunapatikana nadra; na nadra haibadilishi kawaida, baliinatilia nguvu.

Hata kama tutaifungia macho Qur’an Tukufu yenye hekima, kwani ufisadi na upotevu uko mbali na tabia na sera ya Mayahudi? Je, Mayahudi wametakata na upotevu na kujifanya? Bali historia ya Mayahudi ina kitu hata kimoja kinachotambulisha kheri? Pengine mtu anaweza kusema kuwa ufisadi ni sifa inayolazimiana na uzayuni kwa vile ni harakati za siasa za ubaguzi na ufashisti zenye lengo la kuhudumia na kueneza ukoloni. Lakini Uyahudi ni dini tu, kama dini nyingine.

Jibu. Kwanza, kwani hatujui kuwa chimbuko la tofauti hii ni Mayahudi wenyewe ili wajikinge na historia yao ya zamani na sasa, ya aibu, inayoambatana nao. Rudia Juz.6 (5:64).

Pili, kukadiria kuweko na tofauti baina ya Uyahudi na Uzayuni, ni jambo ambalo haliwezekani. Je, Mayahudi kwa ujumla wanauridhia au wanachuikia Uzayuni ambao umejisheheneza silaha, kwa jina la Israel, wenye lengo la kuuhami ukoloni na kupinga ukombozi?

Kwa nini basi Mayahudi wameusaidia Uzayuni kwa hali na mali na kujitolea wake kwa waume, baada ya kujifundisha silaha kali, katika vita vya tarehe 5 Juni 1967?
Tena je, si Mayahudi wanaoamini kidini na kiitikadi kwamba wao ni taifa teule la Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu yuko upande wao dhidi ya watu wote, na kwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha damu zao na kuwahalalalishia wao damu za watu wengine wote, na kwamba wao wameweka kanuni zao na nidhamu zao juu ya misingi hii na watekelezaji ni Israel?

Baada ya hayo, Uyahudi ni dini kama dini nyingine, iliyoteremshwa kwa Nabii Musa (a.s.), lakini imekwisha na wamekwisha watu wake, hakuna aliyebakia; kama zilivyokwisha dini nyingine. Uyahudi wa leo ni Uzayuni isipokuwa nadra sana, na kama tulivyotangulia kusema kuwa nadra sio kipimo.

وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانْبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَشْرَبَهُمْ ۚ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنْزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِنْ كَانُوا أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ {160}

Na tukawagawanya katika koo kumi na mbili, mataifa mbalimbali. Na tukampa wahyi Musa walipomuomba maji watu wake kuwa lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikabubujika chem-chemi kumi na mbili, na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea. Na tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia manna na salwa. Kuleni katika vizuri tulivyowaruzuku. Wala hawakutudhulumu bali, wamejidhulumu wenyewe.

وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَٰذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ {161}

Na walipoambiwa kaeni katika mji huu na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na ingieni katika mlango (wake) kwa kunyenyekea na semeni: Tusamehe. Tutawasamehe makosa yenu na tutawazidishia wale wafanyao mazuri.

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ {162}

Wakabadilisha wale walio dhulumu kauli isiyokuwa ile waliyoambiwa. Na ndipo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kubwa kutoka mbinguni kwa vile walivyokuwa wakidhulumu.