read

Aya 160 – 162: Tuliwagawanya Koo Kumi Na Mbili

Maana

Na tukawagawanya katika koo kumi na mbili, mataifa mbalimbali.

Yaani tuliwagawanya waisrael makundi kumi na mawili, kila kundi likiishia kwa wajukuu kumi na wawili wa Yaqub bin Is-Haq bin Ibrahim. Alikuwa na watoto kumi na wawili na kila mtoto alikuwa na kizazi chake.

Na tukampa wahyi Musa walipomuomba maji watu wake kuwa lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikabubujika chemchem kumi na mbili, na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea.

Umetangulia mfano wake katika Juz.1 (2:60).

Na tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia manna na salwa. Kuleni katika vitu vizuri tulivyowaruzuku. Wala hawakutudhulumu bali, wamejidhulumu wenyewe.

Umetangulia mfano wake katika Juz.1 (2:57). PiazinazofuatiamfanowakeukokatikaJuz.1(2:58-59).

وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُمْ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ {163}

Na waulize habari za mji uliokuwa kando ya bahari walipokuwa wakivunja Sabato, samaki wao walipowajia juu juu siku ya Sabato na siku wasiyofanya Sabato hawakuwajia. Kama hivyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya ufuska.

وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ اللَّهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ {164}

Na kikundi katika wao waliposema: Kwa nini mnawaonya watu ambao Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu kwa adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru mbele ya Mola wenu na huenda wakawa na takua.

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنْجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ {165}

Basi walipoyasahau waliyokumbushwa tuliwaokoa waliokuwa wakikataza maovu na tukawapatiliza walio dhulumu kwa adhabu kali kwa sababu walikuwa wakifanya ufuska.

فَلَمَّا عَتَوْا عَنْ مَا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ {166}

Walipoasi waliyokatazwa tuliwaambia kuweni manyani wadhalilifu