read

Aya 167: Mayahudi Na Adhabu Mbaya

Maana

Qur’an imezungumzia kwa urefu kuhusu waisrael, imezungumzia kufuru yao, na ufisadi wao katika ardhi, kuasi kwao haki. Nasi, kwa kufuatilia Aya tukufu, tumewazungumzia sana, tukataja mifano kadhaa ya sera yao, ikiwa ni ufafanuzi wa Qur’an kuwahusu. Lakini hapa kuna swali ambalo linapelekea shaka na kudangana kuhusu Aya hii na ile isemayo:

ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا {112}

Wamepigwa na udhalili popote wanapokutikana” Juz. 4 (3:112).

Tumelijibu swali hili katika Juz.7 (5:112). Vilevile tumelijibu kwa mfumo mwingine hivi karibuni katika kufasiri Aya 153 ya Sura hii. Hata hivyo hapa tutadokeza kwa ufupi.

Mwenyezi Mungu aliwasalitia waisrael, Mafirauni, kisha wababilon, wafursi, makhalifa wa Alexander kisha manaswara (wakristo).

Imeelezwa katika Tafsir Bahrul-Muhit kuwa kundi la manaswara walifukarika wakawauza wayahudi walio katika mji wao kwa mji ulio jirani yao.

Mwisho mayahudi wakakimbia udhalili na mateso kutaka hifadhi katika miji ya Kiarabu. Wakaishi huko kwa amani. Lakini wao wakavunja ahadi waliyopewa na Mtume (s.a.w.).

Baadhi wakauawa, na Umar bin Al-Khattab akawafukuza waliobaki, wakatawanyika duniani, Mashariki na Magharibi wakiwa ni wenye kufuata tu, bila ya kuwa huru, wakisikiliza amri na kuzitii wakiwa dhalili.
Hatimaye mayahudi wakaona kuwa hawatakuwa na jina isipokuwa wajitoe kwa wakoloni. Kwa ajili hii wakajiuza kwa kila mkoloni mwenye nguvu wamtekelezee njama zake.

Hivi sasa, tukiwa katika majira ya Kusi ya mwaka 1968, imegunduliwa kuwa dola moja ya kikoloni imewashauri mayahudi wa Ulaya Mashariki wafanye mageuzi ya kuendesha miji hiyo chini ya wakoloni. Mayahudi wakaanza kutekeleza njama, lakini njama zao zikafichuka kabla ya kutimia, walikaribia kuuingiza ulimwengu kwenye vita vya tatu.

Kwa ajili ya njama hizo, ndio wakoloni wakatengeneza kikosi cha silaha cha mayahudi katika ardhi ya wapalestine na kukipa jina ya dola la Israel.

Kila mwenye akili anajiuliza. Je, inafaa Israel kuitwa dola kwa maana yake sahihi, ambapo inajuliakana wazi kuwa lau wakoloni watajiepusha nayo siku moja tu, basi haitakuwako.

Je, duniani kuna dola yoyote ambayo haitambuliwi na hata dola moja inayopakana nayo? Ikiwa kweli Israel ni dola kwa nini inaishi kiuadui na kujipanua kwenye nchi jirani?

Dola hasa sio uhaini na silaha; isipokuwa kabla ya chochote, ni kuwa na tabia inayosimamia misingi ya amani, nidhamu inayotilia mkazo haki na msimamo ulio mbali na ubaguzi.

Na tabia ya Israel ni tabia ya kiaskari inayosimama kwa misingi ya vita, nidhamu yake ni kuendeleza uchokozi na msimamo wake ni uzayuni, ubaguzi, chuki, vitimbi na uhaini.

Mwandishi mmoja Mwingereza, Christopher Marlo, anasema katika tamthilia ya Kiyahudi. “Hakika mawazo ya uwezekano wa kuishi pamoja na mayahudi ni aina ya wazimu, wala hawana dawa isipokuwa upanga wenye kukata.”

Je, baada ya yote hayo waarabu wataambiwa ishini kwa amani na mayahudi au mayahudi wataambiwa ni watukufu kwa vile ni kikosi cha silaha kinachoitwa Taifa la Israel kinachoua na kuwafukuza maelfu kwa kusaidiwa na wakoloni? Ikiwa uovu ni ukarimu, basi mayahudi wako katika kilele cha utukufu na ukarimu.

Hatimaye ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayejua hatua itakayofuatia, na mwenye akili hahadaiki na mambo ya dhahiri wala hatapitwa na matukio.

Hakika Mola wako ni mwepesi wa kuadhibu wale waliothibitikiwa na adhabu.

Na hakika yeye ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu.

Yule atakayejing’oa na dhambi zake na akatubia.

وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُمْ بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {168}

Na tukawafarikisha katika ardhi makundi makundi. Miongoni mwao wako walio wema na wengine kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea.

فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِنْ يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِمْ مِيثَاقُ الْكِتَابِ أَنْ لَا يَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ {169}

Na wakafuatia baada yao wabaya waliorithi Kitab wanachukua vitu vya maisha haya duni na wakasema: Tutasamehewa! Na vikiwajia vingine mfano wake, watavichukua. Je, hawakuchukua ahadi katika Kitab kuwa hawatasema juu ya Mwenyezi Mungu ila haki? Nao wamekwishasoma yaliyomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wenye takuwa Basi je, hamtii akilini?

وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ {170}

Na wale wanaoshikamana na Kitab na wakasimamisha Swala, hakika sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.

وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ {171}

Na tulipouinua mlima ukawa juu yao kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika na wakadhani kuwa utawaangukia. Tukawaambia: shikeni kwa nguvu tuliyowapa na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kuwa na takua.