read

Aya 168-171: Tukawajaribu Kwa Mema Na Mabaya

Maana

Na tukawafarikisha katika ardhi makundi makundi.

Mwenyezi Mwenye aliwatawanya Waisraili makundi na vipote mbalimbali, hawana nchi inayowaweka pamoja wala dola inayowalinda.

Uzayuni umejaribu kuwawekea dola kutoka mto Naili hadi Furat kwa kunyang’anya kimabavu. Wanafikiria kuwa uadui wa Israil utapata unayoyataka, wakisahau kuwa dola ya Israili ni ya kupandikizwa tu na kwamba iko siku litawatokea la kuwatokea na mambo yote ya viumbe yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu, sio mikononi mwa uzayuni na ukoloni.

Miongini mwao wako walio wema na wengine kinyume cha hivyo.

Kwa dhahir ni kuwa makusudio ya wema hapa ni imani na kinyume cha hivyo ni wasiokuwa waumini. Umetangulia mfano wake katika Aya 159 ya Sura hii.

Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea.

Makusudio ya mema ni afya na raha, na mabaya ni kinyume chake. Lengo la kupewa mema na mabaya ni kulipwa uongofu wao na kutubia kwa Mola wao.

Na wakafuatia baada yao wabaya waliorithi Kitab wanachukua vitu vya maisha haya duni na wakasema: Tutasamehewa! Na vikiwajia vingine mfano wake, watavichukua.

Makusudio ya maisha haya duni, ni dunia na vitu vya maisha duni; kama riba na rushwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja kwamba wakati wa Nabii Musa (a.s.) kulikuwa na watu wema miongoni mwa wana wa Israil na wengine wasiokuwa wema, aliendelea kusema kuwa wote hao wameacha kizazi kilichojua halali ya Tawrat na haramu yake, lakini wakawa wanahalalisha haramu na wakiharamisha halali, huku wakisema: Mwenyezi Mungu atatughufria wala hatatuadhibu na kitu chochote. Kwa sababu sisi ni watoto wake wapenzi na ni taifa lake teule.

Unaweza kuuliza: Kwanini Mwenyezi Mungu amesema: “Wanachukua vitu vya maisha haya” tena akasema: “Vikiwajia mfano wake, wanachukua?” pamoja na kuwa kauli mbili ziko kwenye maana moja? Je, kuna lengo gani la kukaririka huku?

Lengo ni kuwakanya kwa vile wao wanang’ang’ania madhambi makubwa na kuyarudia mara kwa mara bila ya kujali na huku wakisema kuwa Mungu atatusamehe. Ikiwa kuendelea na madhambi madogo yanageuka kuwa makubwa, je kuendelea na makubwa itakuwaje?

Je, hawakuchukua ahadi katika Kitab kuwa hawatasema juu ya Mwenyezi Mungu ila haki? Nao wamekwishasoma yaliyomo humo.
Hili ni kemeo la pili kwao. Anawakemea kwa madai yao kuwa wao wana- iamini Tawrat na kwamba wameisoma na kuyafahamu yaliyomo. Na katika yaliyokuja katika Tawrat ni kwamba Mwenyezi Mungu anamsamehe mwenye kutubia na akayang’oa madhambi yake. Ama mwenye kung’ang’ania basi yeye ni katika walioangamia.

Vilevile Tawrat imechukua ahadi kuwa kila mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na hiyo Tawrat, basi asimzulie Mungu uwongo. Na waasi hao wanajua hakika hii, lakini bado wanaendelea na madhambi makubwa huku wakisema: “Mungu atatusamehe.” Huku ni kuvunja ahadi na kumzulia Mungu.

Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wenye takua hawarukii maisha ya dunia hii wala hawasemi uwongo na uzushi kuwa Mungu atatusamehe.

Basi je, hamtii akilini?

Vipi atatia akilini ambaye akili yake imetekwa na matamanio yake na moyo wake ukatiwa maradhi na hawaa yake?

Na wale wanaoshikamana na Kitab na wakasimamisha Swala, hakika sisi hatupotezi ujira wa watendao mema.

Wanoshikamana na kitabu ni wale wanaotenda kulingana nacho. Anayeshikamana na kitu hasa ni yule anayetenda, kwa sababu anahisi uthabiti na azma ya kufanya.

AmeunganishakushikamananaKitabnakusimamishaSwalakatikahali ya kuungania mahsus kwenye ujumla, kwa sababu ya siri iliyowajibisha mahsus.

Aya inawataaradhi Mayahudi ambao wameamini Tawrat na wasitumie hukumu zake. Vilevile kumtaaradhi kila mwenye kunasibika kwenye dini na akapuuza hukumu zake; hasa Swala ambayo ndiyo nguzo ya dini, lakini vijana wa sasa wameiweka pembeni.

Na tulipouinua mlima ukawa juu yao kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika na wakadhani kuwa utawangukia. Tukawaambia: Shikeni kwa nguvu tuliyowapa na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kuwa na takua.

Mwenyezi Mungu aliwainulia wana wa Israil mlima ukawa kama kiwingu kilichowafunika, kuwahofisha ili wamche Mungu, lakini Waisraili ni Waisraili tu… UmetanguliamfanowakekatikaJuz.1(2:63).

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آدَمَ مِنْ ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنْفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَٰذَا غَافِلِينَ {172}

Na Mola wako alipowaleta katika wanadamu kutoka miongoni mwa kizazi chao, na akawashuhudiza juu ya nafsi zao. Je, mimi si Mola wenu? Wakasema: Kwa nini! Tumeshuhudia. Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na haya.

أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِنْ بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ {173}

Au mkasema, baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa kizazi nyuma yao, basi utatuangamiza kwa waliyofanya wabatilifu.

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {174}

Na kama hivyo tunazipambanua ishara, kwa kutaraji kuwa watarejea.