read

Aya 172 –174: Je Mimi Si Mola Wenu?

Ulimwengu wa chembe chembe

Na Mola wako walipowaleta katika wanadamu kutoka migongoni mwa kizazi chao, na akawashuhudiza juu ya nafsi zao. Je, mimi si Mola wenu? Wakasema: Kwanini! Tunashuhudia.” Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na haya.

Katika Waislamu kuna kikundi kinachoamini ulimwengu wa chembe chembe. Maana yake, kinasema, ni kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kumuumba Adam, alitoa mgongoni kwake kila mwanaume na mwanamke watakaozaliwa baadaye kuanzia Adam wa kwanza mpaka mwisho wa ulimwengu. Akawakusanya wote pamoja wakiwa na umbo la chembe chembe, kisha akawaambia. Je, mimi si Mola wenu? Wakasema ndiye Mola wetu. Baada ya kukiri hivi akawarudishia mgongoni mwa Adam.

Sisi tuko tayari kuwaunga mkono wale wanaoamini ulimwengui wa chem- be iwapo watatujibu maswali haya yafuatayo:

Je, ni wapi alikusanya Mwenyezi Mungu chembe chembe hizi. Ni katika ardhi hii au nyingine? Je, ardhi hii iliwatosha kwa sababu walikuwa kwenye umbo la chembe. Je, Adam alikuwa mkubwa kiasi cha kuweza kuchukua kila atakayetoka kwake moja kwa moja na kupitia wengine mpaka siku ya ufufuo?

Kisha je, katika rundo hilo linalozidi idadi ya mchanga anaweza kukum-buka mmoja tu maneno hayo na ahadi hiyo aliyompa Mwenyezi Mungu kwa mdomo? Ikiwa ameisahau kwa sababu ya muda mrefu. Je, Mwenyezi Mungu atakuwa na hoja kwake kwa kitu asichokikumbuka?
Haya ni katika upande wa akili, yaani baadhi ya yanayozunguka akilini. Ama katika upande wa

Aya, ni kwamba inafahamisha kinyume na ulimwengu wa chembe chembe, uliochukuliwa kutoka katika mgongo wa Adam wa kwanza. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema: Mola wako alipowaleta katika wanadamu, na wala hakusema katika Adam. Na ilivyo ni kuwa mwanadamu anaweza kuitwa Adam, lakini Nabii Adam wa kwanza hawezi kuitwa mwanadamu.

Vilevile Mwenyezi Mungu anasema kutoka migongoni mwao na hakuse- ma kutoka mgongoni mwake. Akasema , kizazi chao na hakusaema kizazi chake. Zaidi ya haya ni kwamba Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya pili kwamba amefanya hivi ili asiwe na hoja yeyote ya shirk ya mababa, ambapo mshirikina wa kwanza hawezi kutoa hoja ya ushirikina wa baba yake.

Ikiwa haya yote yanafahamisha kitu, basi kitu chenyewe ni kwamba ahadi ilichukuliwa kwa kila mmoja peke yake baada ya kupatikana kwake, bali na baada ya kuongoka na kutambua kwake.

Sisi hatujui maana nyingine ya ahadi hii, inayochukuliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kutuoka kwa mwanadamu, zaidi ya maumbile na silika ya maandalizi ambayo Mwenyezi Mungu ameipa kila akili, na ambayo lau mtu anakusudia kufahamu, hupambanua baina ya uongofu na upotevu na baina ya haki na batili. Na kwa silika hiyo huongoka kwenye imani ya Mwenyezi Mungu na dini yake ya haki.

Kwa maneno mengine ni kwamba kila mtu ni lazima afikirie ishara za Mwenyezi Mungu na dalili zake.

Wameafikiana Waislamu wote kwa kauli moja kwamba Hadith za Mtume ni tafsir na ubainifu wa Aya za Qur’an. Imethibiti Hadith Mutawatir inayosema: “Kila anayezaliwa huzaliwa katika umbile (safi). Wazazi wake ndio watakaomfanya Myahudi au Mnaswara (Mkristo) au Mmajusi.” Na ile isemayo: “Mwenyezi Mungu anasema: Hakika mimi nimewaumba waja wangu wakiwa wameachana na upotofu, kisha huwajia mashetani na kuwaepusha na dini yao.”

Na akawashuhudiza juu ya nafsi zao. Je, mimi sio Mola wenu? Wakasema: Kwanini! Tumeshuhudia.”
Swali na jawabu yako mpaka leo ni hayo hayo mpaka siku ya mwisho. Kwa sababu ni lugha ya hali na matukio, sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu :

فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ {11}

“Akaiambia (mbingu) na ardhi: Njooni kwa hiyari au kwa nguvu! Zikasema: Tumekujia hali ya kuwa watiifu.” (41: 11).

Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na haya.

Haya, ni Tawhid inayofahamishwa na kauli yake: “Je, mimi si Mola wenu?” Hakuna sababu wala udhuru, si katika maisha haya wala ya akhera, kwa aliyepewa na Mwenyezi Mungu maanadalizi kamili ya kufahamu dalili na hoja juu ya umoja wa Mwenyezi Mungu na ukuu wake, kisha akakufuru na akashirikisha.

Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa kizazi nyuma yao, basi utatuangamiza kwa waliofanya wabatilifu?

Mtu hufuata vitu ambavyo anahitaji kujihusisha navyo na kumaliza miaka kadhaa ya kusoma; kama vile udaktari, uhandisi n.k. Ama utambuzi wa kimaumbile ambao haukalifishi mtu zaidi ya kuzinduka na kuamka, kama vile kuwako Mwenyezi Mungu na umoja wake, yote hayo yako sawa.

Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesimamisha dalili zenye kutosheleza juu ya umoja wake, na akaipa kila akili maandalizi ya kuufahamu kwa wepesi.

Kwa hiyo haikubaki udhuru wa mwenye kusema kuwa yeye amekanusha au kushirikisha kwa kuwafuata wengine wabatilifu. Wala hakuna tofauti kabisa katika mtazamo wa akili baina ya anayefanya bila elimu yake kwa makusudi na yule anayefuata batili kwa ujinga bila ya kukusudia, lakini ana uwezo wa kujua na kupambanua.

Na kama hivyo tunazipambanua ishara, kwa kutaraji kuwa watarejea kwenye akili zao ambazo, kwa vyovyote zikisaidiwa na dalili, zitawapeleka kwenye itikadi ya Tawhid.

Angalia Juz. 7 (6:41) kifungu ‘Mwenyezi Mungu na maumbile.’

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانْسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ {175}

Na wasomee habari za yule tuliyempa ishara zetu, kisha akajivua nazo na shetani akamwandama akawa miongoni mwa waliopotea.

وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِنْ تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَثْ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ {176}

Na kama tungelitaka tungelimuinua kwazo. Lakini yeye akashikilia ardhi na akafuata hawaa yake. Basi mfano wake ni kama wa mbwa, ukimhujumu hutweta na ukimwacha pia hutweta. Huo ni mfano wa watu waliozikadhibisha ishara zetu. Basi simulia visa, huenda wakatafakari.

سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنْفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ {177}

Huu ni mfano muovu kabisa wa watu wanaokadhibisha ishara zetu na wakajidhulumu nafsi zao.