read

Aya 191 – 198: Je, Wanawashirikisha Wasioumba Kitu?

Maana

Je, wanawashirikisha wale ambao hawaumbi kitu, hali wao wameumbwa?

Kuumba na amri ni ya Mwenyezi Mungu tu ndiye ambaye kukiambia kitu kuwa kikawa. Yoyote asiyekuwa Yeye, yakiwemo masanamu, anamhitajia Yeye katika asili ya kupatikana kwake na katika kuendelea kuweko kwake.
Wala hawawezi kuwasaidia wala kujisaidia wenyewe.

Usaidizi, ushindi, utukuzaji na udhalilishaji, yote hayo yako chini ya uwezo wa Mwenyezi Mungu. Masanamu yanayokojolewa na paka na mbwa hayawezi kusaidia wala kujisaidia.

Na kama mkiwaita kwenye uwongofu hawatawafuata. Ni sawa ikiwa mtawaita au mtanyamaza.

Haya masanamu hayaumbi, hayasaidii wala hayajisaidii, hayaongoki wala hayaongozi, hayamwiti yeyote wala hayaitikii mwito wa yeyote. Pamoja na yote haya yanaabudiwa!
Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu. Hebu waombeni nao wawaitikie ikiwa nyinyi mnasema kweli.

Mmedai nyinyi washirikina kwamba masanamu ni miungu; na Mungu hunufaisha na kudhuru, hutoa na kuzuia, basi waombeni ili tuone kuwa je, wataitikia maombi yenu?

Je, wao wanayo miguu ya kuendea? Au wanayo mikono ya kushika? Au wanayo macho ya kuonea? Au wanayo masikio ya kusikiliza?

Huku ni kuamshwa na kuzinduliwa washirikina kwamba wao ni bora kuliko masanamu wanayoyaabudu. Kwa sababu wao wana akili za utambuzi, macho ya kuona, masikio ya kusikia, miguu ya kutembelea, mikono ya kushika na ndimi za kutamka.

Lakini masanamu hayana chochote katika hayo. Sasa imekuaje aliye duni ndiye anayeabudiwa badala ya aliye mkamilifu?

Sema: Waiteni hao mnaowashirikisha kisha nifanyieni vitimbi wala msinipe muda.

Anaambiwa Nabii Muhammad (s.a.w.) awaambie washirikina, ikiwa masanamu yenu yana kitu, kama mnavyodai, basi mimi ninayadharau pamoja na nyinyi, basi kama mnaweza shindaneni wala msingoje.

Hakika mtawala wangu ni Mwenyezi Mungu aliyeteremsha Kitab naye ndiye awalindaye wafanyao mema.

Baada ya Mtume (s.a.w.) kuwakana washirikina na miungu yao aliwaam- bia kuwa nyinyi mnawatawalisha masanamu na mimi ninatawalisha Mungu aliyeniteremshia Qur’an iliyo na ubainifu wa kila kitu yake. Yeye vilevile anasimamia hifadhi yangu nani mlinzi wangu.

Je, masananu yenu yana kitabu? Je, yanawalinda? Natija ikawa, kama wanavyojua wote, ni kudhalilika washirikina na kutukuka Uislam na waislamu.

Na wale mnaowaabudu badala yake hawawezi kuwasaidia wala kuji- saidia wenyewe.

Imetangulia punde katika Aya 192. Kumekuja kukaririka kwa sababu Mtume (s.a.w.) alishindana na masanamu, kuwa yampe madhara, ndipo ikanasibu kuishiria kwamba hayo hayawezi hata kujisaidia yenyewe.

Na kama mkiwaita kwenye uongofu hawatasikia.

Vilevile imetangulia katika Aya 193. kukiwa kukaririka ni kwa lengo hilo hilo.

Na unawaona wanakutizama, nao hawaoni.

Inafahamisha nasi hii kwamba masanamu yalikuwa sawa na masanamu haya yaliyomo makanisani. Na kwamba Waarabu walikuwa ni wasanii wa kuchonga. Kwani wao waliyafanya masanamu yao yaonekane kama yanaona ukiyatazama haraka haraka.
Utauliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu amerudiarudia katika Aya zinazo fanana kwamba masanamu hayadhuru wala hayanufaishi, hayasaidii wala hayajisaidii na kwamba hayana mikono wala miguu wala macho, mpaka kufikia Aya tisa ambapo ingeotosha tu kusema hayo ni mawe?

Jibu: Fikra ya kuabudu mizimu na masanamu ilitawala sana katika akili za waarabu na ikachanganyika na roho zao na damu zao kwa vizazi na karne. Imani yao hii ilikuwa na nguvu kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu waliyemfanya ni mshirika wa masanamu.

Kwa hiyo haikuwa rahisi kubadili itikadi yao hii. Wao walikuwa wakijitolea kwa pumzi zao zote, kama ikitajwa kwa ubaya imani yao hiyo.
Ndipo ikalazimika kukaririka huko na kusisitiza na kufananua. Hebu tufaradhie mtu mmoja wa kanisa ajaribu kuondoa picha na sanamu ndani ya kanisa. Je, itatosha aseme tu, hizi ni karatasi na mawe au itabidi atoe hotuba ndefu na pana?

خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ {199}

Shika usamehevu na amrisha mema na achana na wajinga.

وَإِمَّا يَنْزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ {200}

Na kama uchochezi wa shetani ukikuchochea, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu; hakika yeye ndiye asikiaye na ajuaye.

إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُمْ مُبْصِرُونَ {201}

Hakika wale wanye takuwa zinapowagusa pepesi za shetani huzinduka.

وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ {202}

Na ndugu zao wanawavutia katika upotofu kisha wao hawaachi.

وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِمْ بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِنْ رَبِّي ۚ هَٰذَا بَصَائِرُ مِنْ رَبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ {203}

Na usipowaletea ishara, husema: "Kwa nini hukuibuni?" Sema: Hakika nafuata niliyopewa wahyi kutoka kwa Mola wangu tu. Hizi ni busara zitokazo kwa Mola wenu na ni uwongofu na rehema kwa watu wanaoamini.