read

Aya 20 – 23: Kumtii Mwenyezi Mungu Na Mtume

Maana

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msi- jiepushe naye hali mnasikia.

Mwito huu umekuja baada ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na kwa hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na waumin.” Lengo lake ni kumuelezea Mumini ambaye atapewa ushindi na Mwenyezi Mungu na atakayekuwa naye Mwenyezi Mungu popote alipo.

Huyo ni yule ambaye anamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika wanayomwamrisha na wanayomkataza na kwamba mwenye kumhalifu na kuasi; basi amestahiki adhabu na hizaya kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wala msiwe kama wale wanaosema: Tumesikia; na kumbe hawasikii.

Mara nyingi kusikia kutumiwa kwa maana ya kukubali; kama vile mtu kusema: Mimi sikuzikilizi; yaani sikukubalii. Au kama vile kusema: Wenye kusikia sana uwongo; yaani wenye kuukubali

Haya ndiyo maana yaliyokusudiwa katika Aya hii. Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawakataza waumini kuwa kama wanafiki wakidhihirisha kumkubalia Mtume na kutii amri yake na huku wakificha uhalifu na uasi.

Hakika wanyama waovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.

Kiziwi hasikii na bubu hasemi. Wanyama wana masikio ya kusikia, lakini hawafahamu maneno wanayoyasikia na wana ndimi lakini hawasemi. Kwa hiyo hawafahamu wala hawafahamiwi.

Mwenye kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume kisha asiongoke kwayo, basi mfano wake ni kama mfano wa mnyama kiziwi aliye bubu, husikia maneno, lakini hanufaiki nayo.

Mwenye Kutafuta Haki Na Mwenye Kutafuta Windo

Na kama Mwenyezi Mungu angelijua wema wowote kwao angeliwasikilizisha; na kama angeliwasikilizisha wangeligeuka wakipuuza.

Watu ni aina mbili:

1. Ni yule mwenye kuitafuta akiwa hana lengo lolote. Huyu hawezi kuamini msingi wala kuona rai yoyote ila baada ya utafiti na kutilia manani dalili kisha hujenga rai yake juu ya dalili hizo.

2. Ni mwenye kutafuta windo fulani. Haamini isipokuwa dhati yake na maslahi yake. Hukaribisha yale yanayoafikiana na maslahi yake, hata kama ni batili na hukataa yale yanayopingana nayo, hata kama ni haki.

Mwenyezi Mungu huwasikilizisha mwito wa haki wote wawili kwa njia ya sawa sawa, kuweka hoja. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا {15}

“Na hatukuwa ni wenye kuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.” (17:15).

Baada ya ubainifu unaotumiza hoja kwa wote, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anazidisha nasaha na mwongozo kwa wale wanaoitikia na kunufaika nao

وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ {17}

“Na wale wanaokubali kuongoka huwazidishia uongofu.” (47:17).

Ama wale ambao hawaitikii isipokuwa manufaa yao ya kidhati, basi Mwenyezi Mungu huachana nao, maadamu nasiha haziwafai chochote. Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na kama angejua wema wowote angeliwasikilizisha.”

Hilo linafahamika kutokana na kauli yake moja kwa moja bila ya kuingia kati kitu kingine: “Na kama angewasikilizisha wangeligeuka wakipuuza.” Yaani lau angeliwasikilizisha haki, wangeliachana nayo, kwani haikubaliani na hawaa zao.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ {24}

Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita kwenye lile litakalowapa uhai. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba mtakusanywa kwake.