Aya 90 – 93: Mkimfuata Shuaib
Maana
Na wakuu waliokufuru katika kaumu yake wakasema: Kama nyinyi mkimfuata Shuaib, hapo hakika mtakuwa wenye hasara.
Washirikina kwanza walimkabili Shuaib, mwenye mwito, walimtisha na kumkamia. Walipokata tamaa naye waliwageukia wale waliomuamini wakijaribu kuwafitini na dini yao, wakasema miongoni mwa waliyoyase- ma: “Nyinyi mtakuwa wenye hasara mkifuata Shuaib.” Hii ndiyo desturi ya asiye na hoja ila kupoteza tu.
Ukawanyakua mtetemeko wakaamkia majumbani mwao wamejifudikiza.
Hili ndilo jibu sahihi kwa mpinzani na akakataa ila upotevu. Imetangulia Aya hii kwa herufi. Aya ya 78, ya Sura hii.
Wale waliomkadhibisha Shuaib wakawa kama kwamba hawakuwako.
Iliwajia adhabu kwao na kwenye majumba yao na athari zao zote, kama kwamba maisha haya hawakuyajua nayo yamewajua. Kila mtu atalipwa alilofanya sasa au baadaye.
Wale waliomkadhibisha Shuaib ndiyo wenye hasara.
Washirikina waliwaambia wale walioamini nyinyi mtakuwa kwenye hasara, lakini wao mwisho ndio waliokuwa wenye hasara na maangamizi na waumini wakafaidika na kuokoka.
Mwenye akili hawezi kumwambia mwenye kiburi ‘Pongezi’ na kumwambia mnyonge ‘Ole wako’ kwa sababu zama zinaficha na kuleta mambo ghafla. Na mambo huzingatiwa kwa mwisho wake.
Imekaririka jumla “wale waliomkadhibisha Shuaib” kwa kutilia mkazo hasara yao na maangamizi yao.
Basi (Shuaib) akaachana nao na akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika nimewafikishia ujumbe wa Mola wangu na nikawanasihi, basi vipi nihuzunike juu ya watu makafiri.
Vipi nihuzunike na yule aliyejiangamiza mwenyewe kwa kung’ang’ania kumkufuru Mwenyezi Mungu, vitabu vyake na Mitume yake; na kumfanyia stizai aliyemwamini na kufuata njia yake ya sawa. Umetangulia mfano wake katika Aya 79 katika Sura hii.
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ {94}
ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوْا وَقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ {95}