Aya 94 – 95: Hatukumleta Nabii Yoyote Katika Mji
Maana
Na hatukumtuma Nabii yeyote katika mji wowote isipokuwa huwap- atiliza watu wake kwa tabu na mashaka ili wapate kunyenyekea.
Makusudio ya mji ni ule ambao aghlabu hukaliwa na viongozi.
Katika Aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) maangamivu yaliyowafikia wakadhibishaji katika watu wa Nuh, Hud, Swaleh, Lut, na Shuaib na mwisho wao ulio na mazingatio na mawaidha; na kwamba kheri ndio mwisho wa wenye kumcha Mwenyezi Mungu, na uovu uliwarudia wabatilifu.
Katika Aya hii anabainisha kuwa yaliyowapitia watu wa Mitume hiyo hayahusiki na wao tu peke yao, lakini ni desturi ya Mwenyezi Mungu, inawapitia kila watu wanaomkadhibisha Mtume wao. Anawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa shida na mashaka katika nafsi zao, miili yao na mali zao. Si kwa lolote ila ni kwa ajili wawaidhike na wazingatie wao na watakaokuja baada yao.
Kisha tukabadilisha mahali pa ubaya kwa wema, hata wakazidi na wakasema: Tabu na raha ziliwafikia baba zetu.
Makusudio ya ubaya hapa ni dhiki na uzito na wema ni wasaa na wepesi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwajaribu kwa dhiki na shida ili wawaidhike na kwa wasaa na afya ili washukuru lakini ni wachache wanao waidhika na ni wachache zaidi wanaoshukuru.
Neema ilipowazidi na kizazi kuwa kingi, waliidharau haki na kuwafanyia stihizai watu wake; wakawa wanafasiri desturi ya Mwenyezi Mungu kwa ujinga wao na hawaa zao, wakisema: taabu waliyoipata baba zetu haikuwa ni mateso kutokana upotevu na uharibifu wao; wala raha waliyoipata haikuwa na malipo ya wema wao na uongofu wao, isipokuwa ni sadfa tu iliyokuja shaghala-baghala.
Ikiwa hawa wanaghafilika na kuhukumiwa na Mwenyezi Mungu na hekima yake, basi Mwenyezi Mungu mtukufu hakughalifika nao na vitendo vyao.
Basi tuliwaadhibu kwa ghafla hali hawatambui.
Yakiwa ni malipo ya kughurika kwao na kuwa huru na hawa na malengo yao. Namna hii Qur’an inawahadharisha wale ambao hawachungi haki na kutojali chochote wasiadhibiwe ghafla hali hawatambui.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَٰكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ {96}
أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَنْ يَأْتِيَهُمْ بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ {97}
أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَنْ يَأْتِيَهُمْ بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ {98}
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ {99}
أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِنْ بَعْدِ أَهْلِهَا أَنْ لَوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُمْ بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ {100}