read

Isomwapo Qur’an Isikilizeni Aya 204 – 206

Maana

Na isomwapo Quar’an isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemiwa.
Alipotaja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya iliyotangulia kwamba hii Qur’an ni busara na uwongofu na rehema, anaamrisha katika, Aya hii, kuisikiliza na kunyamaza ili kuzingatia uwongofu na dalili zilizomo. Hapana shaka kwamba mwenye kuizingatia vyema Qur’an na akawaidhika nayo, basi yeye anastahiki rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi zake.

Wameafikianamafakihi,isipokuwawamadhebuyaDhahiriya,kwamba kuinyamazia Qur’an ni sunna na wala sio wajibu kwa asiyekuwa Maamuma anayeswali nyuma ya Imam. Wamehitalifiana kuhusu Maamuma, kuwa je, ni wajibu asikilize na amnyamazie Imam akiwa anasoma Qur’an? Kuna kundi lililosema kuwa ni wajibu na wengine wakasema si wajibu.

Kwa hali yoyote iwavyo, ni kwamba amri katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Isikilizeni’ na nyamazeni’ ni ya kupendekeza sio ya wajibu. Kwa sababu amri hii hukumu yake ni kama hukumu ya Aya inyofuatia (Na mtaje Mola wako moyoni mwako…) Kwa sababu, zote mbili zimekuja katika mfumo mmoja. Na amri ya kutaja ni ya sunna, kwa hiyo pia amri ya kusikiliza na kunyamaza.

Zaidi ya hayo ni kwamba kumnyamazia kila msomaji ni jambo zito na lenye mashaka; hasa hivi sasa ambapo kusomwa Qur’an katika vipaza sauti ni kama mchezo na nyimbo; watu hupaaza sauti kukiwa na tukio na hata kama hakuna.

Na mtaje Mola wako nafsini mwako kwa unyenyekevu na hofu na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni.

Msemo katika ‘Mtaje’ unaelekezwa kwa Nabii Muhammad na makusudio ni kwa wote. ‘Bila ya kupiga kelele’ maana yake ni mtaje Mola wako kwa sauti ya katikati baina ya sauti kubwa na ndogo. Na asubuhi na jioni ni fumbo la kudumu kumtaja na kumkumbuka.

Kauli yake Mwenyezi Mungu ‘Bila ya kupiga kelele’ inafahamisha wazi kwamba mtu anayeinua sauti yake kwa kusoma Qur’an basi ameacha mapendekezo na kufanya kinyume; hasa ikiwa ni kwa kuwasumbua wali- olala.

Wala usiwe miongoni mwa walioghafilika na kumtaja Mwenyezi Mungu katika nafsi yako.

Kwa sababu kumtaja kwa ulimi tu, kunafanana na maneno matupu yasiyo kuwa na maana. Maana ya kumtaja Mwenyezi Mungu mtukufu katika nafsi ni kujua kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye muumba mwenye kuruzuku mwenye kutoa uhai na mwenye kufisha na mwenye kuanzisha na kurud- isha.

Kumtaja kuliko bora ni kuogopa mtu kumfanyia ubaya ndugu yake binadamu kwa kuhofia mateso ya Mwenyezi Mungu; na bora zaidi kwake ni kumfanyia wema kwa kutaraji thawabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tunasema bila ya kusita kuwa haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu; Na kwa hakika kumbuko la Mwenyezi Mungu ni (jambo) kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyatenda.” (29:45). Kauli yake: “anajua mnayoyatenda” baada ya kusema “na kumbuko la Mwenyezi Mungu ni kubwa”, kunatilia nguvu kuwa kumtaja na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni kuwafanyia wema waja wa Mwenyezi Mungu.

Na mwenye hasara zaidi katika watu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayefanya Tahlili na takbira, na huku anafanya ufisadi katika nchi kwa kudanganya na hadaa na kuwasaidia mataghuti na wakoloni dhidi ya waja wanyonge wa Mwenyezi Mungu wasio na hatia.

Hakika wale walioko kwa Mola wako hawajivuni wakaacha kumwabudu na wanamtakasa na wanamsujudia.

Wafasiri wanasema kuwa Mwenyezi Mungu amewakusudia Malaika. Wametoa dalili ya neno walioko kwa Mola wako. Kwa sababu walioko kwa Mwenyezi Mungu ni Malaika.
Lakini inawezekana kwamba makusudio ni kila mwenye nafasi na jaha mbele ya Mwenyezi Mungu; ni sawa awe ni Malaika au mwanadamu.

Wametofautiana mafakihi, kuwa je ni wajibu, kusujudu wakati wa kusomwa Aya iliyo na neno
‘Wanasujudi’, kama hii?

Amenukuu Tabrasi kauli kutoka kwa Hanafi kuwa ni wajib na kutoka kwa Shafii na Shia Imamiya kuwa ni sunna yenye kutiliwa mkazo.

Ikumbukwe kuwa Shia Imamia wamewajibisha kusujudi msomaji na msikilizaji zinaposomwa Aya zilizo katika Sura nne: 32, 41, 53 na 96.