read

Vyombo vya habari na kuwapiga chapa Waislam

Kwa kuzingatia haya tuliyoyasema hapo juu, hakuna uhalali wa kuhusisha tukio la Septemba 11 na ile dhana ya Jihadi ndogo katika Uislam.

Hata hivyo, tumesikitishwa sana kuona kwamba vitengo Fulani vya vyombo vya habari, hususan vipindi vya mazungumzo ya maonyesho vya radio bado vinazidi kuchochea chuki dhidi ya
Waislamu, Waarabu na ile imani Tukufu ya kuamini Mungu mmoja ya Uislam. Hii ni licha ya ukweli kwamba Waislamu kiulimwengu walikishutumu kile kitendo cha kigaidi cha Septemba kumi na moja ambamo yalipotea maisha ya watu wasio na hatia.

Kuwalenga Waislam au Waarabu kulikoegemea kwenye hatia kwa ushiriki ni makosa kabisa. Huu undumilakuwili katika vyombo vya habari kwa kweli unatisha. Hebu fikiria japo kwa muda:

Wakati bomu lilipolipuka mnamo siku za mwanzoni za mwezi wa Septemba 2001 huko Ireland ya Kaskazini karibu na shule ya katoliki katika eneo jirani la Protestante, hakuna hata mtu mmoja aliyeilaumu jamii nzima ya Waprotestanti kama “magaidi na wauaji”. Wakati wanaharakati wa IRA walipofanya vitendo vya ugaidi huko Ireland ya Kaskazini au Uingereza, hakuna hata mtu mmoja katika vyombo vya habari va Magharibi ambaye aliipachika Imani ya Katoliki jina kama “Dini ya Ugaidi.”

Pale Dr. Goldstein Mloweziwa Kiyahudi huko Israeli, alipoingia kwenye msikiti wa huko Habron miaka michache iliyopita na akawapiga risasi wafanya ibada wa Kipalestina, hakuna mtu aliyesema kwamba Wayahudi wote ni “magaidi.” Wakati Wa-Serbia walipowaua Waislam kikatili huko Bosnia, vyombo vya habari kamwe havikulilaumu Kanisa la Orthodox kwa jambo hilo ingawa baadhi ya Wahubiri wa Kanisa hilo walikuwa wakiwabariki wanamgambo wa Serbia kabla wao hawajaingia katika kuwaua wafungwa wa Kiislam.

Hata hivyo bado tunaona kwamba wakati Waarabu au Waislamu wachache wanapofanya vitendo vya kuogofya, Waislam wote na Waarabu wote wanapewa jina la “magaidi na wauaji” moja kwa moja. Kama Waislam, tunaviomba vyombo vya habari kutenda haki na sio jingine lolote.

Vyombo vya habari vinapaswa kutambua kwamba wale wateka nyara ambao walitumia ndege zile kama silaha hawakuteka nyara tu zile ndege na kuua maelfu ya watu wasio na hatia huko
Marekani; vile vile wamewaonea na kuwaathiri Waislam bilioni moja na ambao sasa wamepewa au kupachikwa jina kama “wauaji na magaidi.”