read


Kitabu hiki ni mkusanyiko wa baadhi ya mafunzo yake S.A.W. ambayo yanatupa msingi wa yote hayo.

Hadithi Za Mtume (s.a.w.)

Kimetarjumiwa Na:
Ductoor A Kadiri
Taasisi ya Fikra za Kiislamu (Islamic Thought Centre)
Tehran
Islamic Republic of Iran
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu. Mwingi warehema. Mwenye kurehemu.

Sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu Aliyetuokoa na ujahiliya wa zamani. Tunamwomba Atujaalie pia kuutupilia mbali ujahiliya wa kileo. Tuwe ni wenye kufwata barabara maagizo Yake na mafundisho ya Mtume Wake S.A.W. na tuwe ni katika umati bora uliowahi kutokea kwa watu.

Umma wetu wa Kiislamu, kwa kipindi sasa umenyonyorwa mengi: akili, fikra na hata mapato na mwisho kuachiwa mizozo na utengano na kutusahaulisha wajibu wetu. Hivyo, jinsi ya kujua namna ya kujirudishia haki zetu ni kurudi kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Kurani Tukufu) na kwenye mafunzo ya Mtume Wake S.A.W. ambaye ni kiigizo chema kwetu sisi. Kwake yeye ndiko tutapata ufanisi wetu wa mambo yote: uongofu wa akili, malezi ya kiroho, maelekezo ya kiibada, kijamii, kisiasa, kiuchumi na shifaa ya yaliyo nyoyoni.

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa baadhi ya mafunzo yake S.A.W. ambayo yanatupa msingi wa yote hayo, kimetarjumiwa kwa Kiswahili kutoka kile cha Kiarabu kilichotolewa kwa mara ya kwanza hapo mwaka 1982 na DAR EL TAWHEED ya huko Tehran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tunatumai Inshaallah kitakuwa na manufaa kwa sote. Na pia tunataraji kitafaa katika madrassa zetu za Kiislamu huku Afrika Mashariki na hasa kwa watumiao lugha yetu ya Kiswahili.

Na mwisho, tunamshukuru sana Sheikh Abdillahi Nassir kwa kukubali kupoteza masaa yake mengi kupitia mswada wa tarjuma hii na vile vile kwa ushauri wake alio­tupa. Mwenyezi Mungu Amjazi heri.

Taasisi ya Fikra za Kiislamu,
Tehran,
Jamhuri ye KiisIamu ye Iran.

Alisema Mtume Muhammad (SAW):

Aliye mbali mno kufanana nami kati yenu ni bahili, mchafu, mwenye mambo ya aibu.

Nifikishieni haja ya asiyeweza kunifikishia haja yake. Kwani anayemfikishia mtawala haja ya asiye­weza kujifikishia, Mwenyezi Mungu Atathibitisha (Ata­imarisha) miguu yake juu ya Sirati siku ya Kiyama.

Mtu mmoja wa ukoo wa Tamimi anayeitwa Abu Umayya, alimjia Mtume (SAW) na kumuuliza: Ewe Muhammad, walingania watu kitu gani? Akamjibu: "Ninaita kwa Allah kwa ujuzi wa kweli, mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata." Nawalingania watu warudi kwa Ambaye ukipatwa na dhara ukamwomba, Yeye Hukuondolea. Ukimwomba Akusaidie nawe ukatika dhiki, Yeye hukusaidia. Ukimwomba nawe ufukara, Yeye Hukutajirisha. (Abu Umayya) akasema tena: "Niusie ewe Muhammad" Mtume akamwambia: "Usiwe ukikasirika." Abu Umayya akamwambia: "Niongeze." Akaambiwa: "Waridhishe watu kwa unachokiridhia nafsi yako." Akasema: "Niongeze." Akaambiwa: "Usiwe ukiwatusi watu usije ukajiletea uadui." Akasema: "Niongeze." Akaambiwa tena: "Usiache kutenda mema kwa wenyewe." Akasema: "Niongeze." Akaambiwa: "Wapende watu nao watakupenda, kutana na nduguyo - Mwislamu - kwa uso mkunjufu na usiwe ukinuna kusije kununa kwako kukakukosesha ya dunia na ya Akhera.

Mtu mmoja alimjia Mtume (SAW) na kusema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niusie." Akasema (SAW): "Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na chochote hata kama utateketezwa kwa moto, na hata ukiadhibiwa ila moyo wako uwe mtulivu kwa imani. Wazazi wako walishe, uwatendee hisani wakiwa hai au maiti. Wakikuamuru kumwacha mkeo au kuacha mali yako, basi fanya hivyo. Kwani kufanya hivyo ni katika imani. Sala za faradhi usiziache makusudi, maana aachaye sala za faradhi makusudi hutoka katika dhima ya Mwenyezi Mungu. Na tahadhari sana kunywa pombe na chochote cha kulevya, maana hayo ni ufunguo wa kila shari.

Watu walimsifu mtu mmoja mbele ya Mtume (SAW) kwa uzuri sana na kumsema kwa mambo yote mazuri. Mtume (SAW) akawauliza: "Mtu huyo ana akili kiasi gani?" Wakamjibu: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tunakueleza yanayomhusu kulingana na bidii yake katika ibada na heri zinginezo, nawe unatuuliza kuhusu akili yake!" Mtume (SAW) akawajibu: "Mpumbavu hupatwa kwa upumbavu wake, na makubwa kuliko machafu ya mchafu (wa vitendo). Na kesho watu wata­panda daraja kubwa na kuwa karibu na Mola Wao kwa kadiri ya akili zao."

Kipenzi mno wa waja wa Mwenyezi Mungu kwa Mwenyezi Mungu, ni anayewafaa mno waja Wake.

Jilindeni na watu kwa kuwadhania mabaya.

Ukiona ni kisirani, endelea. Ama ukidhani tu, usiendelee. Na ukifanyiwa husuda, usifanye uovu.

Mkimwona mtu asiyejali anayosema au anayosemwa basi huyo ni mwovu au ni shetani.

Umma ukiongozwa na mwovu wao, kiongozi wa umma akiwa ni duni wao na fasiki kuheshimiwa, basi (umma huo) ungojee balaa (kuufika).

Mwenyezi Mungu Akiughadhabikia umma na Asiwateremshie adhabu, basi bei ya bidhaa (nchini mwao) hupanda, umri wao ukawa mfupi, biashara zao zikakosa faida, matunda yakakosa kuzaa (ifaavyo), mito ikakosa maji ya kutosha, mvua Akaizuia na Akawasaliti na waovu wao.

Umma wangu utakapofanya mambo kumi na matano, watashukiwa na balaa. Akaulizwa: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yapi hayo?" Akasema: "Wakichukua ngawira kwa noba, amana kuwa ngawira, zaka kuiona ni gharama, mume akamtii mkewe na kumwasi mamake, mamake akamtendea wema rafiki yake na akamtupa babake, sauti zikawa juu misikitini, mtu akaheshimiwa kwa kuogopewa shari lake, kiongozi wa umma akawa ni duni wao, hariri zikivaliwa, tembo (pombe) ikanywewa kwa wingi, wakashughulikia nyimbo na ngoma na wa mwisho katika umma huo kuwalaani wa kwanza wake. Baada ya hayo, wajiandalie kupatwa na matatu: upepo mkali mwekundu, kuondolewa na kutupwa.

Itakapokuwa siku ya Kiyama, guu Ia mtu halitatele­za (halitavuta hatua) hadi kwanza aulizwe juu ya mambo manne: umri wake aliumaliza katika nini; ujana wake aliupitisha vipi; mapato yake aliyapata kutoka wapi na aliyatumia katika nini na (alikuwa na kadiri gani ya) mahaba yetu sisi Ahli Bayt.

Ikiwa watawala wenu ni wabora wenu, matajiri wenu ni wasamehevu wenu, mambo yenu ni kwa kusha­uriana baina yenu, basi juu ya ardhi ni bora kwenu kuliko ndani yake. Ama ikiwa viongozi wenu ni wabaya wenu na matajiri wenu, ni mabakhili wenu, basi kuwa ndani ya ardhi ni bora kwenu kuliko (kuwa) juu yake.

Ikiwa uzinifu utazidi baada yangu, vifo vya ghafla vitaongezeka. Na pindi vipimo vikipunjwa, Mwenyezi Mungu Atawachukulia hatua kwa njaa na upungufu (wa matunda). Na wakizuia (wakikataa kutoa) zaka, ardhi nayo itafunga baraka zake za mimea, matunda na madini. Na wakipendelea katika maamuzi, watasaidiana katika dhuluma na uadui. Na wakivunja ahadi, Mwenyezi Mungu Atawasaliti na adui yao. Na wakikata jamaa (zao), mali zitawekwa mikononi mwa watu waovu. Wasipoamrishana mema na kukatazana maovu na wasiwafuate Ahli Bayt wangu ambao ni bora, Mwenyezi Mungu Atawasaliti na waovu wao. Wakati huo wema wao wataomba (Mwenyezi Mungu) na hawa­taitikiwa (dua zao).

Mtu mwovu akisifiwa, Kiti cha Enzi (cha Mwenyezi Mungu) hutingishika na Mwenyezi Mungu kukasirika.

Mambo manne ni katika alama za uovu: ukavu wa macho, ugumu wa moyo, wingi wa tamaa katika kuitaka dunia na kukakawana na dhambi.

Mambo manne aliye nayo yumo katika nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mtu ambaye hifadhi ya mambo yake ni shahada kwa kuwa hakuna mungu ila Allah na kuwa mimi ni mjumbe Wake; na ambaye akipatwa na msiba hunena: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungw na tutarudi Kwake. Na ambaye akipata jema hunena: Alhamdu Lillah. Na ambaye akitokewa na kukosa - hunena Astaghfirullah.

Mambo manne humpasa kila mwenye akili na busara katika umati wangu. Akaulizwa: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yapi hayo?" Naye akajibu: "Kusikiliza elimu, kuihifadhi, kuieneza na kuitumia."

Mhurumieni mheshimiwa aliyedhalilika, tajiri aliye­fukarika na mwanachuoni aliyepotea katika zama za wajinga.

Jilazimisheni siri katika mambo yenu, maana kila mwenye neema huhusudiwa.

Shari itakayolipwa haraka mno ni ile ya dhuluma.

Mhusudiwa wa watu wangu kwangu katika umati wangu ni mtu ambaye hali yake si ya makuu, adumishaye vyema sala, amwabuduye Mola Wake vizuri pamoja na kuwa hajawahi kumwona, ainamishaye macho mbele za watu, ambaye riziki yake ni ya kuwania tu lakini akawa na subira mpaka akafa na hali hiyo, warithi wake wakawa wachahce na (pia) wenye kumlilia (baada ya kufa).

Mbora wenu wa imani ni aliye mbora wenu wa tabia.

Atakayekuwa karibu nami sana Kesho huko Kiyama ni mkweli wenu katika mazungumzo, afikishaye amana, atimizaye ahadi, mbora wenu kwa tabia ujema na wa karibu wenu zaidi kwa watu.

Kichache cha kuwepo Akhiri Zamani (mwisho wa dunia) ni ndugu wa kuaminika na pesa za halali.

Sameheni kuteleza (au makosa) ya wenye msiba.

Kula sokoni ni uanzali (utwevu).

Mkamilifu wa watu kwa akili ni awashindaye katika kumwogopa Mwenyezi Mungu, na awashindaye katika kumtii. Na mpungufu wa watu kwa akili ni awashindaye katika kumwogopa mfalme, na awashindaye katika kumtii.

Je niwaelezeni anayefanana na mimi kwa tabia njema? Wakajibu: kwani, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Ni mbora wenu wa tabia, mpole wenu sana, anayewashinda nyote katika kuwafanyia watu wake wema na anayewashinda nyote kwa uadilifu katika nafsi yake akiwa amekasirika au ameridhika.

Je niwaoneshe bora ya tabia njema za duniani na Akhera? Ni kumwunga anayekukata, umpe anayekunyima na umsamehe anayekudhulumu.

Tambueni! Wabaya kabisa wa umma wangu ni ambao huheshimiwa kwa kuogopewa shari zao. Tambueni! Ambaye ataheshimiwa na watu kwa sababu ya kuogopa shari yake, basi huyo si katika mimi (si mfuasi wangu).

Nimeamuriwa kuelewana na kuwachukulia watu kama nilivyoamrishwa kufikisha ujumbe (kwa watu).

Uaminifu huvuta riziki na hiana huvutia ufukara.

Subira yatokamana na Mwenyezi Mungu na haraka hutokamana na shetani.

Kamili wa imani miongoni mwa waumini ni mbora wao wa tabia njema.

Kila balaa kubwa hulipwa malipo makubwa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Akimpenda mja (Wake) Humpa mitihani. Ambaye moyo wake umeridhia, hupata radhi ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuchu­kia, hupata chuki.

Mwenyezi Mungu Ameharamisha Pepo kwa kila mchafu wa tabia na ulimi, mchache wa haya, asiyejali anayosema au anayosemwa. Mtu aina hiyo hakika ukim­weka popote (kumnasibisha) hutomkuta ila tu ni mwovu au ni mshirika wa shetani. Akaulizwa: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je katika watu kuna mashetani?" Akajibu: "Ndiyo. Je hukusoma neno Ia Mwenyezi Mungu: "Na shirikiana nao katika mali na watoto." 17:64

Mwenyezi Mungu Amewaumba watumwa katika viumbe Wake kwa ajili ya haja za watu. Wanatamani mema na kudhani ukarimu ni heshima. Na Mwenyezi Mungu Hupenda tabia njema.

Mwenyezi Mungu Humchukia mzee mzinifu, tajiri dhalimu, maskini mwenye kuringa na mwombaji mwenye kuchagiza ambaye humharibia mtoaji thawabu zake. Kadhalika Huchukia kiburi, ujuvi na ukedhabu.

Mwenyezi Mungu Hupenda Akimneemesha mja kuona ana athari ya neema Zake Alizompa. Na Huchukia shida na kujitia katika shida.

Mwenyezi Mungu Humpenda karimu katika haki yake.

Mwenyezi Mungu Ana waja ambao hukimbiliwa na watu kwa haja zao. Watu hao ndio wenye kusalimika na adhabu za Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama.

Hakika yeyote anayejifunza elimu ili kubishana na wasiojua, au kupata heshima kwa wanaojua, au kuziele­keza nyuso za watu kwake ili wamheshimu, basi na ajia­ndalie makao yake Motoni. Maana uongozi haustahiki ila kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wanaoustahiki. Na anayejiweka ambapo sipo Mwenyezi Mungu Alipomweka, Mwenyezi Mungu Humkasirikia. Na anayejitukuza kwa kusema 'mimi ndiye mkubwa wenu' hali yeye si hivyo Mwenyezi Mungu Hamtazami mpaka atakapojirudi kwa alilosema na atubu kwa Mwenyezi Mungu kwa alilolidai.

Hakika katika (baadhi ya) mashairi mna maneno ya hekima. Na katika maelezo mna uchawi.

Muumin hutwaa adabu za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Akimpanulia riziki, naye hujipanua. Na Akimfungia, hujizuia.

Sisi, Mitume sote, tumeamurishwa kuzungumza na watu kwa kadiri ya akili zao.

Nauchelea umati wangu mambo matatu: kutii kukutu, kufuata matamanio na (kumfuata) imamu mpotofu.

Hisani hufanyiwa wenye dini au heshima. Jihadi ya wanyonge ni hija, na jihadi ya mwanamke ni kuishi na mumewe kwa wema. Mapenzi ni nusu ya imani. Katu mtu hafukariki akiwa na iktisadi (katika matumizi yake). Na takeni kuteremshiwa riziki kwa kutoa sadaka (kwani) Mwenyezi Mungu Alikataa kuijaalia riziki ya waja Wake waumini kutoka wanapopadhania.

Heri zote hupatikana kwa akili, (hivyo) hana dini asiye na akili.

Kwa hakika ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Hakuna amali yoyote ya kuwakaribisha na Moto ila nimewaeleza na kuwakanya nayo. Na hakuna amali yoyote ya kuwakaribisha na Pepo ila nimewaeleza na kuwaamurisha muifanye. Kwani Roho Mwaminifu alivuvia moyoni mwangu kwamba hakuna nafsi itakayo­kufa mpaka riziki yake ikamilike.

Mola Wangu Aliniusia mambo tisa: Aliniusia (kuwa na) Ikhlasi kwa siri na dhahiri. Kuwa mwadilifu katika furaha na hasira. Kuwa mwangalifu wa matumizi katika ufukara na utajiri. Nimsamehe aliyenidhulumu, nimpe aliyeninyima na nimuunge aliyenitupa. Kunya­maza kwangu kuwe nafikiri. Uzungumzi wangu uwe ni dhikri (kumtaja Mwenyezi Mungu) na kutazama kwangu kuwe ni kwa kuzingatia.

Mikono ni mitatu: wa kuomba, wa kutoa na wa kuzuia. Na mkono bora ni ule wa kutoa.

Imani ni kuitakidi kwa moyo, kunena kwa ulimi na kutenda kwa viungo.

Imani ni nusu mbili: nusu moja ni ya subira na nusu nyengine ni ya kushukuru.

Ogopeni kujinyenyekesha kiunafiki. Nako ni kuone­kana mwili mnyenyekevu, hali moyo si mnyenyekevu.

Kuacha shari ni sadaka.

Sifa tatu mwenye kuwa nazo amejikamilisha imani:
Akifurahi furaha yake haimtii katika batili au makosani; akikasirika hasira zake hazimtoi kwenye haki; na akiwa na mamlaka hatoi kisicho chake.

Nyoyo zimeumbwa kumpenda anayezifanyia hisani na kumchukia anayezitendea uovu.

Kuketi msikitini kungojea (wakati wa) sala ni ibada (kamili) maadam haijatenguka. Akaulizwa: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni kitu gani kinachoten­gua?" Akajibu: "Kusengenya."

Uzuri (wa mtu) u katika ulimi.

Mtu mmoja alimpelekea Mtume (SAW) maziwa na asali anywe. Akasema: "Vinywaji viwili kila kimoja huto­sheleza chengine. Mimi sikinywi wala sikiharamishi ila tu namnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa sababu anaye mnyenyekea Mwenyezi Mungu Humwinua. Anayemkumbuka Mwenyezi Mungu kwa kumtaja, Mwenyezi Mungu Humpa thawabu."

Heshima ambazo lazima kila muumin kuzichunga na kuzitekeleza ni: heshima ya dini, heshima ya adabu na heshima ya chakula.

Uchangamfu huondoa mfundo.

Uzuri wa tabia humfikisha mwenye nayo daraja ya afungaye saumu na kusali sana (usiku wote kila siku). Akaulizwa: "Ni kipawa gani bora alichopawa mtu?" Akajibu: "Tabia njema."

Tabia nzuri huimarisha mapenzi.

Kutimiza ahadi ni katika imani.

Kuuliza vizuri ni nusu ya elimu. Na upole ni nusu ya maisha.

Kuona haya ni namna mbili: kuona haya kwa akili na kuona haya kwa kipumbavu. Kuona haya kwa akili ni elimu na kuona haya kwa kipumbavu ni ujinga.

(Kuwa na) haya ni katika imani.

Siku moja, Mtume (SAW) alitoka na kuwakuta watu wanalivunja jiwe. Akawaambia: "Shujaa mwenye nguvu kuwashinda nyote ni anayejimiliki nafsi yake wakati akihamaki. Na mstahamilivu kuliko nyote ni anayesamehe wakati ana uwezo (wa kuadhibu)."

Mambo mawili hakuna wema wa juu kuyashinda: kumwamini Mwenyezi Mungu na kuwafaa waja wa Mwenyezi Mungu.
Na mambo mawili hakuna shari za kuyashinda: kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwadhuru waja wa Mwenyezi Mungu.

Vishawishi viwili huwafitini watu wengi: siha na faragha.

Mwema atokana na wema mwenye kuufanya. Na mshari atokana na shari mwenye kuitenda.

Bora wenu ni bora wenu kwa tabia njema, wanaozoea (watu) na kuzoewa.

Dunia ni duara. Mazuri uliyo nayo yalikujia pamoja na udhaifu wako. Na mabaya yaliyokushukia hukutumia nguvu zako kuyazuia. Anayekata tamaa kwa aliyoya­kosa, mwili wake hupumzika. Na anayeridhia alilopewa na Mwenyezi Mungu, jicho lake hutulia.

Dunia ni kifungo (jela) kwa muumin na Pepo kwa kafiri.

Kichwa cha akili baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu ni kuingiliana na watu. Lakini pasi na kuacha haki.

Mwenyezi Mungu Amrehemu mja ambaye hunena ya heri akajipatia (fungu), au akanyamaza akasalimika.

Umati wangu umeondolewa (kuchukuliwa makosa kwa) mambo tisa: kukosa, kusahau, waliotenzwa nguvu, wasiyoyajua, wasiyoyaweza, waliyolazimika, kijicho, kisirani na kuwadhania watu kwa wasiwasi maadamu ulimi haukutamka (dhana hiyo).

Kuyachukia ya dunia (kwa utawa) ni kuipunguza tamaa, kushukuru kila neema (ya Mungu) na kujiweka mbali na kila Aliloharamisha Mwenyezi Mungu.

Aliulizwa (SAW): "Nani mwenye balaa kubwa zaidi humu duniani?" Akajibu: "Ni manabii, kisha wanaofanana nao (kwa matendo mazuri), kisha wanao­fanana nao. Muumin hujaribiwa (na Mwenyezi Mungu kulingana na kadiri ya imani yake na uzuri wa matendo yake. Ambaye imani yake ni sahihi na matendo yake ni mazuri, balaa zake huzidi. Ama ambaye imani yake ni hafifu na matendo yake ni dhaifu, huyo balaa zake hupungua.

Ulizeni wanazuoni; zungumzeni na wenye hekima na ketini na mafukara.

Mtakuja kuwa na tamaa ya uongozi kisha iwageuke na kuwa hasara na majuto. Mwanzo ni furaha na mwisho ni karaha.

Mwendo wa haraka haraka huondoa heshima ya muumini.

Sunna ni namna mbili: sunna moja ni katika faradhi. Hiyo kuiendeleza baada yangu ni uongofu na kuiacha ni upotofu. Sunna nyengine ni katika yasiyo ya faradhi. Hiyo kuiendeleza ni fadhila na kuiacha si hatia.

(Kuwa na) tabia mbovu ni kisirani.

Kutenda mema ni kuyaacha maovu yote. Sadaka ya siri huzima ghadhabu za Mwenyezi Mungu. Kuunganisha jamaa ni kujiongezea umri. Kila wema ni sadaka. Wenye kutenda wema humu duniani watakuwa ndio wakirimiwa huko Akhera. Na waovu humu duniani ndio wa kutupwa huko Akhera. Na wa kwanza kuingia Peponi ni wale wenye kutenda mema.

Watu wawili katika umati wangu wakitengenea, umati wangu nao utatengenea. Na wakiharibika, umati wangu nao utaharibika. Akaulizwa: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Watu gani hao?" Akajibu: Wanazuoni na viongozi.

Ungeni jamaa zenu hata kama ni kwa salamu peke yake.

Sauti mbili Mwenyezi Mungu Huzichukia: kulia kwa mayowe wakati wa msiba, na nyimbo na zumari wakati wa neema.

Mwenye kufunga saumu (wakati wote) huwa katika ibada hata kama amelala kitandani mwake maadamu hakumsengenya Mwislamu.

Mwenye kula anayeshukuru ni bora kuliko mwenye saumu asiyeshukuru.

Heri na furaha ni kwa anayeacha matamanio yaliyomjia kwa sababu ya kuogopa ahadi (za Mwenyezi Mungu) ambazo hakuziona.

Ibada ina mafungu saba. Bora kuliko yote ni kuta­futa halali.

Ajabu iliyoje ya muumin! Mwenyezi Mungu Haachi kumkidhia haja zake ila huwa ni heri kwa mia huyo, limempendeza hilo au limemchukiza. Akimjaribu huwa ni kafara ya dhambi zake. Na Akimpa au Akimkirimu huwa Amempenda.

Elimu ni hazina. Funguo zake ni kuuliza (wanaojua). Basi ulizeni (wajuao) na Mwenyezi Mungu Atawarehemu. Maana ni wanne wapatao malipo: muuli­zaji, msemaji, msikilizaji na anayewapenda hao (watatu).

Elimu ni kipenzi cha muumin. Upole ni waziri wake. Akili ni kiongozi wake. Amali ni unyofu wake. Subira ni amiri jeshi wake. Upole ni mzazi wake. Wema ni ndugu yake. Ukoo ni Adam. Cheo ni ucha Mungu na murua ni kuitengeneza mali uzuri.

Alama kuwa Mwenyezi Mungu Yu radhi na viumbe vyake ni bidhaa kuwa rahisi (nchini mwao) na watawala wao kuwa waadilifu. Na alama ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe Vyake ni watawala wao kuwa wajeuri na bidhaa zao kuwa ghali (nchini mwao).

Fadhila za elimu ni bora kwangu kuliko fadhila za ibada. Na bora ya dini yenu ni ucha Mungu.

Nasara mmoja kutoka Najrani alikwenda Madina. Alikuwa ni mtu mwenye heshima na haiba. Mtume (SAW) akaambiwa: 'Nasara huyo ana akili sana!' Mtume (SAW) akamfokea aliyesema maneno hayo. Akamwambia: 'Nyamaza! Aliye na akili ni yule ampwekeshaye Mwenyezi Mungu na kutenda amali za kumtii.

Kusoma Qur'ani katika sala ni bora kuliko kusoma Qur'ani nje ya sala. Kumtaja Mwenyezi Mungu ni bora kuliko kutoa sadaka, na kutoa sadaka ni bora kuliko kufunga saumu ambapo saumu ni wema. Kisha akanena: Hakuna kauli (inayosifika) ila kwa (kufuatana na) amali. Hakuna kauli wala amali ila kwa nia. Na hakuna kauli, amali wala nia ila kwa kulingana na sunna (ya Mtume SAW).

Mwenyezi Mungu Amegawanya akili mafungu matatu: Ambaye atakuwa na yote, akili yake hukamilika. Na ambaye hanayo, basi hana akili: kuwa na maarifa mazuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuwa mtiifu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuwa na subira na amri ya Mwenyezi Mungu.

Idhibitini elimu kwa kuiandika.

Mtume (SAW) alisimama katika msikiti wa Kheef akanena: Mwenyezi Mungu Amnusuru mja anayesikia maneno yangu akayahifadhi na kuyafikisha kwa ambaye hakuyasikia. Huenda mtu aliyebeba fiqihi akaenda nayo kwa anayeijua kumshinda. Na huenda aliyeibeba fiqihi akaenda nayo kwa asiye faqihi. Matatu hauyakii moyo wa Muumini: kuwa na ikhlasi katika kufanya amali za Mwenyezi Mungu, kuwanasihi viongozi wa Waislamu, na kushikamana na umoja wao. Waumini wote ni ndugu. Damu zao zatoshana, na wote ni mkono mmoja kwa asiyekuwa wao, mnyonge wao aweza kwenda na dhima yao.

(Mtume) Isa bin Maryam (AS) aliwaambia wanafunzi wake: Jipendekezeni kwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha Kwake. Wakamwuliza: Ewe Roho ya Mwenyezi Mungu! Tutajipendekeza na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kitu gani? Akawajibu: Kwa kuwachukia wenye kutenda maasi. Hivyo, takeni radhi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwakasirikia. Kisha wakamuuliza: Ewe Roho ya Mwenyezi Mungu! Tuwe tukikaa na nani? Akawajibu: Muwe mkikaa na yule ambaye kumwona (kumwangalia) kunawakumbusha Mwenyezi Mungu, maneno yake yanawazidishia amali zenu (njema) na vitendo vyake vinawapendekezea Akhera.

Mwenyezi Mungu (SAW) Amesema: Hii dini Nimeiri­dhia Mimi Mwenyewe binafsi. Na haitaistawisha ila ukarimu na uzuri wa tabia. Kwa hiyo, iheshimuni kwa mawili hayo maadamu mkali wafuasi wake.

Mtu mmoja alimwambia Mtume (SAW): 'Niusie kitu ambacho Mwenyezi Mungu Atanifaa kwacho. Mtume (SAW) akamwambia: 'Kithirisha kuyakumbuka mauti litakufanya ushike mwendo mzuri. Kuwa na shukurani maana huzidisha neema. Kithirisha dua kwani hujui ni lini utaitikiwa. Ogopa uovu wa aina zote kwa sababu Mwenyezi Mungu Amekwishaamua kwamba atakayefanyiwa uovu Atamnusuru. Alisema katika Surah Yunus aya 23: “Enyi watu, jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe.' Na tahadhari na kufanya vitimbi (au hila) maana Mwenyezi Mungu Ameamua kwamba: 'Kitimbi kibaya hakitamzunguka ila mwenyewe.’

Mtu mmoja alimwambia Mtume (SAW): 'Niusie.'
Akamwambia: 'Linda ulimi wako.' Akamwambia tena:
'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, niusie.' Naye akakariri: 'Linda ulimi wako.' Akamwomba tena: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: niusie.' Akamjibu: 'Ala! Una nini! Watu wangeweza kutupwa Motoni isipokuwa kwa sababu ya mavuno ya ndimi zao!!'

Mtu mmoja alimwendea Mtume (SAW) na kumwambia: 'Niusie.' Mtume (SAW) akamjibu: 'Usiwe ukikasirika.' Kisha akamuuliza tena amuusie, naye akajibu 'Usiwe ukikasirika.' Kisha akanena: 'Nguvu si kwa kumenyana mieleka. Bali mwenye nguvu ni yule anayejimiliki nafsi yake wakati akishikwa na ghadhabu (hasira).'

Mtu mmoja alimuuliza Mtume (SAW) 'Uthabiti ni nini?' Akamjibu: 'Ni umshauri mwenye rai (nzuri) kisha umtii (kwa alilokushauri.)

Mtume (SAW) alimwambia mwanawe Ibrahim naye ajitoa mhanga: 'Lau yasingekuwa yaliyopita ni malipo ya yaliyosalia na kuwa la mwisho litafuatia la kwanza, tungekuhuzunikia (sana) ewe Ibrahim.' Hapo machozi yakamlengalenga. Akasema (SAW) 'Macho yanalengalenga machozi na moyo unahuzunika wala hatuneni ila Anayoyaridhia Mwenyezi Mungu, lakini tuna huzuni sana ewe Ibrahim.'

Siku moja Mtume (SAW) alimuuliza Abu Dharri: Ni imani ipi inayoaminika? Akamjibu: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wanaojua. Akamwambia: Kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kufanya uadui kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Mtume (SAW) alimwambia mtu aliyemuuliza kuhusu umati wake, akamjibu: Umati wangu ni wale wenye haki japo ni wachache.

Siku moja Mtume (SAW) alisema: Enyi watu! Mwenye ndege mbaya katika nyinyi ni nani? Wakamjibu: 'Ni mtu kufa asiache mtoto.' Akawajibu: 'La. Bali mwenye ndege mbaya kikweli ni mtu kufa na awe hakutoa mtoto wake yeyote kwa Mwenyezi Mungu. Huyo ndiye mwenye kisirani japo atakuwa na watoto wengi baada yake.' Kisha akauliza tena: 'Nani mkata katika nyie?' Wakamjibu: 'Ni asiye na mali.' Akawajibu: 'La. Bali mkata wa kikweli ni ambaye hakutoa chochote katika mali yake kwa Mwenyezi Mungu japokuwa ataacha mengi baada yake.' Akawauliza: 'Mbabe katika nyinyi ni nani?' Akajibiwa: 'Ni shujaa mwenye nguvu ambaye hawezekani kuangushwa.' Akanena: 'La. bali mbabe wa kikweli ni ambaye shetani amemkalia moyoni, ghadhabu na hamaki zikampanda kisha yeye akamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuweza kuzuia hasira zake.'

Aliulizwa (SAW): ‘Ni rafiki yupi bora?’ Akajibu: Ni ambaye ukikumbuka jambo hukusaidia. Na ukisahau hukukumbusha. Akaulizwa tena: Ni mtu yupi mbaya zaidi? Akajibu: Ni wanazuoni wakifisidika.

Mtume (SAW) alimwandikia Maadh kumtanzia kwa ajili ya kifo cha mwanawe: "Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kwa Maadh bin Jabal: Salamun Alaikum (Amani juu yenu): Ninamhimidi Mwenyezi Mungu Ambaye hapana mola ila Yeye. Ama baad: Nimepata habari umeshtuka sana kutokana na kifo cha mwanayo aliyechukuliwa na Mwenyezi Mungu. Mwanayo alikuwa ni zawadi na amana ya Mwenyezi Mungu kwako. Mwenyezi Mungu Akakustarehesha kwaye kwa muda na kumtwaa tena kwa muda maalum (alioupanga). Sote ni wa Mwenyezi Mungu na sote tutarudi kwake. Nakusihi, mshtuko wako usije kukuharibia ujira wako, lau ungekuwa umeutangulizia thawabu msiba wako, ungejua kuwa msiba huo umekuwa mdogo sana ukilinganisha na thawabu kubwa zilizoandaliwa wenye kukubali amri (ya Mwenyezi Mungu) na subira.

Kisha wapaswa kujua kushtuka hakumrudishi maiti wala hakuondowi kudura. Hivyo, omboleza vyema. Masikitiko yako yasije kukuondolea ambayo ni lazima kwako na kwa viumbe wote. Hayo yatawafika viumbe wote kutokana na kudura Yake Mwenyezi Mungu. Wassalamu alaikum warahmatullahi wabarakaatuhu.

Mavazi hudhihirisha utajiri, kumfanyia hisani mtumishi humzima adui.

Mtakuwaje wanawake wenu watakapofisadika, vijana wenu kuharibika na msiamrishane mema wala kukatazana maovu? Akaulizwa: Kweli yatatokea hayo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akajibu: Ndiyo! Tena mabaya zaidi ya hayo. Akawaambia: Mtakuwaje mtaka­poamrishana maovu na kukatazana mema? Akaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kweli yatakuwa hayo? Akajibu: Ndiyo! Na mabaya zaidi ya hayo! Akawauliza tena: Mtakuwaje wakati mkiona mema kuwa ni maovu na maovu kuwa ni mema?

Usifanye jambo lolote Ia heri kwa kujionesha. Wala usiliache kwa kuona haya.

Usibishane na nduguyo na kumfanyia mzaha, wala usimpe ahadi kisha ukaihalifu.

Mja hafikii daraja ya wachaji Mungu kabisa, mpaka kwanza aache lisilo na neno kwa kutahadhari na lililo na neno.

Haingii Peponi ila ambaye ni Mwislamu. Abu Dharri alimuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Islamu ni nini? Akajibu: Islamu ni kitu ambacho kiko uchi, mavazi yake ni kumcha Mungu. Fulana yake ni uongofu. Shati lake ni kuwa na haya. Uwezo wake ni kuepuka haramu. Ukamilifu wake ni dini, matunda yake ni amali njema. Kila kitu kina msingi wake, na msingi wa Islamu ni kutu­penda sisi Ahli Bayt.

Mwenye kuibiwa haachi kumtuhumu asiye na makosa mpaka mwisho huwa na dhambi kubwa kushinda mwizi mwenyewe.

Hautafaulu umati wowote unaotegemezea mambo yake kwa mwanamke.

Mtume (SAW) alipoteremshiwa aya: Wala usivikodolee macho yako tulivyowastareheshea watu wengi miongoni mwao. Alisema: Asiyejitukuza kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu, nafsi yake hujihasiri mwenyewe. Na anayetazama kwa jicho Ia kutamani vya watu ambavyo ni vya kidunia, majonzi yake huzidi.

Lau dunia ingekuwa sawa na ubawa kwa Mwenyezi
Mungu na ubawa wa mbu Hangempa kafiri wala mnafiki chochote humo.

Utajiri si wingi wa mali, bali utajiri ni utajiri wa moyo.

Si katika sisi anayepunja Mwislamu au kumdhuru au kumfanyia hila.

Hakuiamini Qur'ani mtu ambaye huhalalisha haramu zake (hiyo Qur'ani).

Muumin hapatwi na taabu, ugonjwa wala huzuni, hata hamu ila Mwenyezi Mungu Humfutia kwayo maovu yake.

Utaratibu hauwi katika kitu ila hukipamba. Na ubaradhuli hauwi katika kitu ila hukivuruga tu.

Sikukataza kitu chochote baada ya (kukataza) kuabudu masanamu kama nilivyokataza kubishana na watu.

Muumini huwa ni mtu mchangamfu wa kufanya dhihaka na kuchezacheza na watu. Na mnafiki huwa ni mtu wa kukunja uso na kughadhabika.

Muumini ni haramu yote (kuitweza) heshima yake, mali yake na damu yake.

Muumini ni mithili ya suke. Mara huinama na mara husimama wima, na mfano wa kafiri ni mithili ya mpunga. Hauachi kuwa wima daima.

Mtenda wema anayetukanwa anafaa kurehemewa (kuonewa imani).

Kuingiliana na watu ni nusu ya imani. Na kuwachu­kulia upole ni nusu ya maisha.

Murua wetu sisi Ahli Bayt, ni kusamehe wanaotu­dhulumu na kuwapa wanaotunyima.

Amelaaniwa anayewasukumia watu uzito wake.

Mtu akiwafanyia jambo zuri, basi muwe mkimtu­nuku zawadi. Msipokuwa nayo basi msifuni, kwani kusifu ni jaza.

Mtu akiwafanyia jambo zuri, basi muwe mkimtunuku zawadi. Msipokuwa nayo basi msifuni, kwani kusifu na jaza.

Anayetangaza maovu ni kama anayeyatenda.

Anayemridhisha mtawala kwa yanayomuudhi Mwenyezi Mungu, hutoka katika dini ya Mwenyezi Mungu.

Anayepambazukiwa katika umati wangu na hamu yake haiko kwa Mwenyezi Mungu basi si katika watu wa Mwenyezi Mungu. Asiyejishughulisha na mambo ya Waislamu si katika wao, na anayekubali kutii unyonge si katika sisi Ahli Bayt.

Anayepambazukiwa na kuingiliwa na jioni hali Akhera ndiyo hamu yake kuu, Mwenyezi Mungu Humja­alia ukwasi moyoni mwake na kumkusanyia mambo yake. Na katu haondoki duniani mpaka riziki yake ikamilike. Ama anayepambazukiwa na kuingiliwa na jioni hali dunia ndiyo hamu yake kuu, Mwenyezi Mungu Humwekea umaskini machoni mwake na kumtawanyia mambo yake. Na katu hapati chochote duniani ila Alichomgawanyia.

Anayepewa manne hanyimwi manne: Apewaye kuomba msamaha, hanyimwi maghfira. Anayepewa kushukuru hanyimwi ziada. Anayepewa mwafaka wa kutubu hanyimwi kabuli, na anayepewa mwafaka wa kuomba hanyimwi kuitikiwa.

Anayewapa watu fatwa pasina ujuzi, hulaaniwa na malaika wa mbinguni na wa ardhini.

Anayekula anachopenda, akavaa anachopenda na kupanda anachopenda, Mwenyezi Mungu Hatamtazama (siku ya Kiyama) mpaka aondoe au aache.

Atupaye buibui Ia haya hana (makosa kwa) kusenge­nywa.

Anayeingiliwa na jioni na kupambazukiwa akiwa na (mambo) matatu huwa amekamilikiwa na neema humu duniani: mwenye kuingiliwa na jioni na kupambazukiwa na afya mwilini, usalama njiani na ana chakula cha siku nzima. Na akiwa na Ia nne, huwa amekamilikiwa na neema duniani na Akhera: nalo ni imani.

Anayefikia hadi pasi na haki huwa miongoni mwa waliokia.

Anayejifukarisha hufukarika.

Anayenyokewa na mkono, ni haki juu yake kutoa zawadi. Asipoweza naasifu tu. Asipofanya hilo, basi atakuwa amekufuru.

Unayemfaa hukufaa. Asiyejiandalia subira kwa matatizo ya zama hushindwa (na maisha). Anayekopesha watu nao humkopesha. Anayewaacha, wao hawamwachi. Akaulizwa: basi nifanye nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akajibu: Wakopeshe ulivyonavyo kwa ajili ya siku utakayofukarika.

Aliyenyimwa upole huwa amenyimwa heri zote.

Mtu kutafuta kumridhi kiumbe kwa kumkasirisha Mwumbaji, Mwenyezi Mungu Humsaliti na kiumbe huyo.

Mwenye kuhesabu ajali (yake) kuwa ni kesho huwa amekosea namna ya kujiandaa kwa mauti. (Yatakikana uwe tayari wakati wote).

Anayetenda jambo pasina ujuzi nalo, anayoharibu huwa ni mengi kushinda anayotengeza.

Anayeamiliana na watu asiwadhulumu, akawazungumzia asiwadanganye, na akawaahidi asihalifu ahadi hiyo, basi huyo ni katika aliyekamilikiwa na murua wake, umedhihiri uadilifu wake, amewajibika kupata malipo, na ni haramu kumsengenya.

Yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi naatazame ahadi anazotoa.

Anayezidiwa na hamu mwili wake hushikwa na maradhi. Anayeharibika tabia zake moyo wake husono­neka. Na anayewahimiza watu wasiyotaka, murua na heshima yake huisha.

Asiyeona haya kutafuta halali hujifaa mwenyewe na kujipunguzia gharama na kujiondolea kiburi. Anayeri­dhia riziki chache kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Naye Huridhia uchache wa amali zake. Mwenye kuridhika na dunia na tamaa yake ikazidi, Mwenyezi Mungu Humpofua moyo wake kwa kadiri ya tamaa yake. Anayejitenga na mambo ya kidunia, asiwe na tamaa nayo, Mwenyezi Mungu Humpa elimu pasina kujifunza na uongozi pasina mwongozi. Akamwondolea upofu (wa moyo) na kumfanya aone. Ila tu baada yangu watakuwako watu ambao ufalme hautatulia kwao ila tu kwa kuua na udikteta. Utajiri hautatulia kwao ila kwa ubahili. Na mahaba ya watu hayatatulia kwao ila kwa kufuata matamanio ya nafsi.

Mtu ambaye amehamishwa na Mwenyezi mungu kutoka kwenye unyonge wa maasi hadi kwenye utukufu wa twaa, Mwenyezi Mungu Humtajirisha bila mali, Akamtukuza bila ukoo na Akampumbaza bila mpumba­zi. Anayemwogopa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Humfanya akawa anaogopewa na kila kitu. Na asiyemwogopa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Humfanya akaogopa kila kitu. Anayeridhia riziki chache kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Naye Huridhia uchache wa amali zake. Asiyeona haya kutafuta maisha ya halali, gharama na baa zake huwa tahfifu na watu wake huneemeka. Anayejitenga na ya dunia, Mwenyezi Mungu Huimarisha hekima moyoni mwake na kuitamkisha ulimini mwake na Akam­wonesha aibu za kidunia - zikiwa ni maradhi au dawa yake - na Humwondoa duniani hali yu salama, na kumpeleka Nyumba ya Milele.

Aliyeahidiwa thawabu na Mwenyezi Mungu kwa amali aliyoitenda, Mwenyezi Mungu Atamtimizia. Na anayemwahidi adhabu kwa amali aliyoitenda, (Mwenyezi Mungu) Ana hiari.

Kati ya alama za Kiyama ni wasomaji kuwa wengi na mafaqihi (kati yao) kuwa wachache. Viongozi kuwa wengi na waaminifu kuwa wachache. Mvua kuwa nyingi na mimea kuwa michache.

Katika ufanifu wa mtu ni kumtaka shauri Mwenyezi Mungu na kuridhika na aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Na katika uovu wa mtu ni kuacha kumtaka shauri Mwenyezi Mungu na kuchukia aliyokidhiwa na Mwenyezi Mungu.

Kujuta ni toba.

Mtoto kuwaangalia wazazi wake kwa mapenzi ni ibada.

Bora ya msaidizi katika kumcha Mwenyezi Mungu ni utajiri.

Muumini kumpenda muumini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika sehemu kubwa ya imani. Apendaye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu akachukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, akatoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuzuia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu huwa ni katika wasafi (wa roho na matendo).

Zawadi ni namna tatu: zawadi ya kutunuku, zawadi ya kujifanya na zawadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Watu watafikiwa na zama ambapo mtu hatajali yanayoharibika katika dini yake maadamu dunia yake inamwitikia (inamtengenekea).

Mtu hukonga na kuzeeka kwa mawili: pupa na tamaa.

Hotuba ya Mtume (SAW) aliyotoa katika Hija ya kuagana.

Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu. Tunamhimidi na kumwomba msaada. Tunamwomba maghfa na kutubia Kwake. Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu na shari za nafsi zetu na maovu ya matendo yetu. Aongozwaye na Mwenyezi Mungu hapana wa kumpotoa. Na Ampotoaye hapana wa kumw­ongoza. Na ninashuhudia kwamba hakuna tnungu ha Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mtumwa Wake na ni Mtume Wake.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Nawausieni kumcha Mwenyezi Mungu na kuwahimiza kutenda amali za kumtii. Na ninaanza (kuwaambia maneno ya) Mwenyezi Mungu kwa lililojema. Ama Baad! Enyi watu! Nisikilizeni ninayowafafanulia, maana sijui pengine siVa­kutana nanyi tena baada ya mwaka huu mahali hapa.

Enyi watu! Damu zenu na heshima zenu ni haram (kuvunjwa) hadi mtakapokutana na Mwenyezi Mungu. Kama ambavyo siku yenu hii ya leo na nchi yenu hil ni haramu (kuvunjwa heshima yake). Je nimefikisha (ujumbe wa Mwenyezi Mungu ama la?).

Walijibu 'Ndiyo umefikisha.' Akasema: Ewe Mola! Shuhudia! Basi aliye na amana nairudishe (salama) kwa wenyewe.

Hakika riba imeondolewa. Na riba ya kwanza nina­yoanza nayo kuiondoa ni riba ya Abbas bin Abdul Muttalib. Na hakika (malipo ya) damu za Zama na Ujinga yanaondolewa; na damu ya kwanza ninayoanza nayo kuiondolea malipo ni damu ya Amir bin Rabia bin al-Harith bin Abdul Muttalib. Na athari (zote) za Zama za Ujinga zimeondolewa isipokuwa ulindaji Kaaba na unyweshaji maji. Na (kuua) makusudi (malipo yake) ni kisasi; na kifo kisichofanana na makusudi ni kilichouliwa kwa fimbo au jiwe na malipo yake ni ngamia mia. Kina­chozidi hapo, basi ni cha Zama za Ujinga.

Enyi watu! Tayari shetani amekwisha kata atamaa ya kuabudiwa katika ardhi yenu hii. lakini ameridhia kutuwa kwa yasiyokuwa hayo kati ya mnayoona nyinyi kuwa ni duni.

Enyi watu! hakika kuchelewesha (miezi mitukufu) ni kuzidi katika ukafiri; kwayo hupotezwa wale walioku­furu. Wanauhalalisha (mwezi mtukufu) mwaka mmoja na kuuharamisha niwaka mwengine ili waifanye sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Mwenyezi Mungu. Na zama zimezunguka kama mfano wa siku ya kuumbwa mbingu na ardhi. Idadi ya miezi mbele ya Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbil~ katika elimu ya Mwenyezi Mungu (tangu) siku Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne iliyo mitukufu - mitatu imefuatana, na mmoja uho peke yake: Dhul Qaadah, Dhul Hijjah na Muharram; na Rajab uko baina ya Jamada na Shaaban. Je nimefikisha? Ewe Mola! Shuhudia.

Enyi watu! Wake zenu wana haki zao kwenu na nyinyi mna haki zenu kwao. Haki zenu kwao ni wasim­laze yeyote mnapolala, wasimwiingize yeyote msiyemtaka nyumbani mwenu ha kwa idhini yenu, na wasifanye chafu lolote. Wakiyatenda hayo, Mwenyezi Mungu Amewapa idhini ya kuwawaidhi na kuwapiga kipigo kisicho cha kuumiza sana. Wakikoma na kuwatii mtapaswa kuwalisha na kuwavisha kwa wema. Mliwatwaa kuwa ni amana ya Mwenyezi Mungu, mka­halalishiwa uchi wao kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Hivyo, nicheni Mwenyezi Mungu kuhusu wanawake na mwausie hen.

Enyi watu! Waislamu ni ndugu. Si halali kwa Mwislamu mali ya ndugu yake ila kwa nia na roho safi. Je nimefikisha? Ewe Mola! Shuhudia. Basi msirejee kuwa makafiri mkakatana shingo wenyewe kwa wenyewe. Kwani nimewaachia ambayo mkishikamana nayo hamwezi kupotea: Ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na AhIi Bayt wangu. Je nimefikisha? Ewe Mola! Shuhudia.

Enyi watu! Mola wenu nyote ni mmoja. Nyote mwatokana na Adam, na Adam atokana na udongo. Bora wenu nyote mbele ya Mwenyezi Mungu ni amchaye zaidi. Na Mwarabu hana ubora juu ya siye Mwarabu ila (ubora ni) kwa ucha Mungu. Je nimefikisha (ama Ia?) Walijibu: 'Ndiyo.' Akasema: Basi aliyepo amfikishie (habari hizo) asiyekuwepo.

Enyi watu! Mwenyezi Mungu Amempangia kila mrithi fungu lake Ia urithi. Na haifai mrithi kuusiwa zaidi ya thuluthi. Mtoto ni wa godoro, na mzinifu lake ni jiwe. Anayedai baba asiye wake, na anayetawalisha asiye mtawala wake, atapatwa na laana ya Mwenyezi Mungu, malaika Wake na watu wote. Na Mwenyezi Mungu Hatamkubalia toba wala wema. Amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu.