read


Kunyoa Ndevu : Ukike Wa Kisasa

Maelezo : Ndevu ( Kwa Kiarabu : Lahya ) inaelezwa kama nywele zinazoota juu ya shavu la uso na taya za sehemu zote mbili (marejeo : al-Qamus al-Muharram t ya al-Fayrazabad ). Inajumuisha na nywele za kipaji cha uso, uoto chini ya mdomo wa chini, nywele za kidevu, na nywele zinazoota sehemu za chini za taya.

Maamrisho ya Kiislamu kuhusu ndevu Kuweka au kufuga ndevu ni Wajib (faradhi) kwa ajili ya wanaume. Hii inayo ushahidi bora katika Sunnah (kama vile itakavyoonyeshwa hapa chini) na ndivyo iliyo maoni ya Ma’ulamaa wa Kiislamu. Baadhi ya Mashekhe wanaidharau hii Sunnah hivyo inawabidi Waislamu wasipotoshwe kwa kuwaona na kuwafuata hao na wala wasipotoshwe kwa kutolewa fatwa zisizo na misingi kwa kujaribu kuthibitisha matendo yao. Kwa kufanya hivyo wao wanawadanganya na kuwapotosha watu kwa kutumbukia katika njia potofu, ambapo Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Yeyote yule anayeianzisha Sunnah nzuri(njia) basi atalipwa mema kwa hayo, zaidi ya kulipwa thawabu sawa na za wale watakaomfuata yeye kwa hayo. Ambapo yeyote yule atakayeianzisha Sunnah mbaya atapata madhambi nayo, na zaidi ya madhambi hayo atapata sawa na za wale watakaomfuata yeye kwa hayo”. (Muslim)

Na vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Allah swt haiondoi ilimu kwa mara moja kutoka mioyoni mwa watu, lakini Yeye huiondoa ilimu kwa kuchukua (maisha ya ) Ma’ulamaa (Ma’ulamaa wa kweli). Wakati ambapo Ma’ulamaa hawapo, basi watu watawachukua majaheli kuwa viongozi wao. Hao ndio watakaowapa fatwa (amri za Dini) bila ya kuwa na ilimu. Kwa kufanya hivyo, wao watapotoka na kuwapotosha wengine pia.” (Al-Bukhari)

Orodha ya ukiukwaji Kunyoa kwa ndevu kunamaanisha kukiuka maamrisho ya Dini ya Kiislamu, kama vile ilivyo dhahiri kutoka Qur’an na Sunnah za Mtume Muhammad s.a.w.w. Ifuatayo ni orodha ( si lazima mpaka mtu azifahamu) ya ukiukwaji huo :

a. Kutomtii Allah swt Kunyoa ndevu ni kutomtii Allah swt. Mtawala wa Yemen, aliyechaguliwa na Mfalme wa Kiajemi Kisraa, alituma majumbe wawili kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kumpelekea mwaliko. Wakati hao walipotokezea mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. , aliwaona hao wamenyoa ndevu na kufuga masharubu (ndevu za mdomo). Kwa hayo yeye alichukizwa kuwatazama hao (kwa sababu ya kuonekana visivyo sawa) na aliwaambia : “Ole wenu ! Je ni nani aliyewaambia kufanya hivyo ?” Wao walimjibu : “Bwana wetu ! (wakimaanisha Kisraa).”

Mtume Muhammad s.a.w.w. aliwaambia : “Lakini Mola wangu, aliye Mkuu na Aliyetukuzwa, ameniamrisha mimi kuibakiza ndevu yangu peke yake na kunyoa masharubu yangu.” [Imerekodiwa na Ibn Jarra-abar, na imeamuliwa na al-Albani kuwa ni Hasan (nzuri) ]

b. Kutomtii Mtume Muhammad s.a.w.w. Kunyoa ndevu ni kutomtii Mtume Muhammad s.a.w.w. Katika Ahadith nyingi, Mtume Muhammad s.a.w.w. amewaamrisha wanaume wafuge ndevu peke yake. Hadith zifuatazo pia zina maana hizi hizi : “Nyoeni masharubu na muziache ndevu”. [ Al-Bukhari na Muslim ]

Kumtii Mtume Muhammad s.a.w.w. ndiko kumtii Allah swt ambaye amesema ( inavyomaanisha) : “Mwenye kumtii Mtume ( Muhammad s.a.w.w.) amemtii Allah swt .” [ An-Nisaa 4 : 80 ]

c. Kupotoka na vile Anavyoonekana na Mwongozo wa Mtume Muhammad s.a.w.w. Mtume Muhammad s.a.w.w. alikuwa akifuga ndevu ndefu [ Muslim ]. Hivyo inambidi kila mtu ajaribu kumfuata Mtume Muhammad s.a.w.w. katika matendo yake, kama vile Allah swt alivyosema : Sura Al-Ahzaab, 33, Ayah ya 21 : ‘Bila Shaka mnao mfano mwema kwa Mtume ( Muhammad s.a.w.w. ) wa Allah swt …’

Na Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Kwa hakika muongozo ulio bora kabisa ni muongozo wa Mtume Muhammad s.a.w.w. .” [ Muslim ]

d. Kupotoka kutoka njia ya Waumini Kunyoa ndevu ni kupotoka kutoka njia ya Waumini. Mitume yote pamoja na Sahabah , Ma’ulamaa wakubwa, na Wachamungu Waislamu wa ‘ummah huu walikuwa wakiotesha ndevu. Hakuna habari ya hata mmoja wao aliyekuwa akinyoa ndevu zake. Hivyo ilivyokuwa njia yao, na Allah swt ndivyo anavyosema katika Sura An-Nisaa, 4, Ayah ya 115 :

‘Na atakayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam (Motoni); napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia.’

e. Kuwaiga wasio Waislamu Kunyoa ndevu ni kuwaiga wasio Waislamu. Swala hili limesisitizwa katika baadhi ya Ahadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. Kwa mfano : “Nyoeni masharubu yenu na muoteshe ndevu zenu. Muonekane tofauti na Wachawi (wafuasi wa dini iliyokuwapo huko Uajemi). [Muslim ] “Nyoeni masharubu yenu na kuziacha ndevu zenu peke yake. Muwe tofauti na Ahlal Kitaab yaani watu wa Vitabu.” [Muslim] Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Muwe tofauti na Mushrikiin (wale wanaowaabudu wengine mbali na Allah swt ) munyoe masharubu yenu na kufuga ndevu. [Al-Bukhari na Muslim ]

Sisi tumeamrishwa kuwa tuwe tofauti na tusifanane na wasio Waislamu, kama vile tunavyoamrishwa na Allah swt katika Sura al-Fatihah. Vile vile Allah swt anatuambia katika Sura Al-Jathiyah, 45, Ayah ya 18 : ‘Kisha tumekuweka juu ya Sharia ya amri yetu, basi ifuate, wala msifuate matamanio ya wale wasiojua (kuhusu Islam).’

Na Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Yeyote anayewaiga watu basi atakuwa mmoja miongoni mwao.” [imerekodiwa na Abu Daud naAl-Albani ameamua kuwa ni kweli.]

f. Kubadili maumbile aliyoyaumba Allah swt bila ya idhini. Mtume Muhammad s.a.w.w. amebainisha kuwa mwanamke anayebadilisha kile Allah swt alichokiumba (kama kwa kuyaondoa nywele kutoka usoni mwao or kuyajaza meno yao (kwa dhahabu) au kuchora mapicha katika miili yao) kwa kutaka kujionyesha, basi wanalaaniwa na Allah swt . [Al-Bukhari na Muslim ]

Hadith hii inawataja wanawake makhsusi kwa sababu wao daima wanajirembesha zaidi ya wanaume. Lakini onyo hili linawahusu wote wanaume na wanawake wote kwa pamoja, kwa sababu sharti la laana limeshabainishwa, na laana hizi zinamhusu yeyote anayetimisha hali hizo.

Unyoaji wa ndevu unaangukia katika onyo hili, kwani ni ovu kabisa kuliko hata Nam (uondoaji wa nywele za usoni) inavyofanywa na baadhi ya wanawake. Hivyo inamaanisha kuwa ni kumtii Shaitani ambaye amesema, Sura An-Nisaa, 4, Ayah ya 119 : “Na nitawapoteza na nitawatumainisha na nitawaamrisha wabadili walivyoumbwa na Allah swt.’

g. Kuwaiga wanawake Ndevu ndiyo tofauti mojawapo iliyo kuu baina ya mwanamke na mwanamme. Kunyoa ndevu kunaondoa utofautisho huu, na hivyo inamaanisha kuwaiga wanawake. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Allah swt anawalaani wanaume wale wanaowaiga wanawake, na Allah swt anawalaani wanawake wale wanaowaiga wanaume.” [Al-Bukhari]

h. Kunyoa ndevu kunapingana na maumbile halisi. Mtume Muhammad s.a.w.w. amezitaja sifa kumi zinazodalilisha maumbile mema na safi [Muslim]. Sifa mbili miongoni mwao ni kunyoa mashurubu na kuotesha ndevu.

Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. anatuambia kuwa kila mtoto azaliwaye huzaliwa na maumbile safi na toharifu, ambayo hapo mbeleni inaharibiwa kwa vishawishi vya mazingara na malezi. [Al-Bukhari na Muslim]

Maumbile ya Waislamu wengi yapo katika nyayo za wasio Waislamu, kwa masikitiko, yameharibiwa mno kiasi kwamba wanamwona mtu aliye nyoa ndevu kuwa ni smati na mtu mzuri apendezaye kuliko yule mtu ambaye ameweka ndevu – kwa hakika ni kinyume kabisa na yale aliyoyasema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Hadith !

Maumbile haya kamwe hayabadiliki kwa muda : Allah swt amesema katika Sura Ar-Rum, 30, Ayah ya 30 : ‘…… ndilo umbile Allah swt Alilowaumbia watu. … Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Allah swt.’

Ama kunyoa ndevu zao, baadhi ya wanaume wanatoa visingizio kuwa wake zao wanapenda hivyo ! Kama kwamba madhumuni ya maisha yao humu duniani ni mwelekeo potofu wa wake zao badala ya kufuata maamrisho bayana ya Allah swt na Mtume Muhammad s.a.w.w.

Wengine wanadai kuwa kufunga ndevu kunaleta mwasho na kujikuna. Haya hayawezi kumzuia mtu kujidhatiti katika maumbile halisi, lakini inawezekana ikatokea hali kama hiyo kwa sababu za kutojiweka msafi na kuosha vizuri na wudhuu ilivyoamrishwa katika Sunnah.

Kile wakisemacho `Ulamaa na Maimamu Ma’ulamaa wote wa `ulamaa of as-Salaf u- li, wakiwemo Maimamu wanne, walikubaliana kuwa kunyoa ndevu ni haraam. Wao wamechukulia unyoaji wa ndevu kama ni uvunjaji wa Shariah usioruhusiwa, kama vile ilivyoripotiwa kuwa ‘Umar bin ‘Abdul-‘Aziz. Wao walikuwa wakimchukulia mwanamme aliyenyoa ndevu kuwa ni kikike. Wengi wao walikuwa hawakubali ushahidi uliokuwa ukitolewa nao au hawakukubaliwa kuongoza sala (kuwa Imamu wa sala).

Allah swt atuongoze kushikamana na Dini Yake, na kuzingatia Sunnah za Mtume Muhammad s.a.w.w., na kuwa miongoni mwa wale waliobarikiwa humu duniani na Aakhera.