read

Maswali kuhusu Maiti

*********
Jarida hili lina maswali machache kuhusu mambo yanayomhusu maiti.

*********
SWALI LA KWANZA: Umeuliza swali kuhusu

JARIDATAIN :
 
Jibu:
Jarida ni matawi ya mti bila majani. Hayo ni matawi mawili ama kutokea mti wa mkomamanga, au mti fulani kama mzambarau ( plum) au mti unaota kandokando ya maji au Mkunazi au mtende. Vikikosekana hivyo, matawi ya mti wowote ule unafaa. Kiasi cha urefu wa mkono takriban 20”
• Kipande cha upande wa kulia uguse kwapani.

• Ama kipande cha upande wa kushoto kiwekwe juu ya kwapa.

Kwa hakika kuweka Jaridatain ni Sunnah kwani imesisitizwa mno na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Maimamu a.s. kuweka Jaridatain yaani matawi hayo mawili pande zote mbili za maiti. Sababu imeelezwa kuwa, wakati wote ule utakaokuwa matawi hayo yapo mabichi hayajakauka, basi marehemu huyo atapona Fishari Qabr ( mabano ya kaburi ).
Juu ya kila tawi hili huandikwa:
       Kalimah Shahada zote 3 yaani Shahada ya Allah swt, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Maimamu ambao ndio Makhalifa baada ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
       Jina la marehemu na jina la baba yake
       Majina ya Maimamu a.s. 12
       Kunyunyiziwa kidogo udongo wa Karbala.
Mwishoni maiti huvikwa sanda.
 
Swali La # 2
 
2. mambo yanayo fanyiwa mayyiti badda ya mazishi ni yapi baada ya siku ngapi.haraka iwezekanayo.ghudahafisi.
 
SWALI LA PILI : Mambo yanayo fanyiwa mayyiti baada ya mazishi ni yapi baada ya siku ngapi.
 
JIBU :
Kwa hakika umeuliza swali moja ambalo linahitaji majibu marefu mno, lakini kwa mukhtasari ninakuorodheshea kama yafuatavyo:
• Kusali Sala ijulikanayo kama Salat Hadyail Mayyit au Salat wahshat baada ya mazishi

• Kusali Sala zote ambazo marehemu hakusali, anadaiwa, haraka iwezekanavyo

• Kufunga saumu zote ambazo marehemu hakufunga, anadaiwa, haraka iwezekanavyo

• Kulipa madeni yote ambayo marehemu anadaiwa, haraka iwezekanavyo

• Kutimiza Hijja iwapo marehemu alikuwa anadaiwa katika uhai wake, haraka iwezekanavyo

• Kumfanyia mema kwa jina lake mfano kutoa sadaqa, misaada, kusomewa Quran, n.k., daima

• Kufuata na kutekeleza yale yaliyo katika usia wake,daima

• Kuwalea na kuwatunza wale wote aliokuwa akiwatunza na kuwalea na kuwasaidia marehemu

• Kufuata nyao nzuri za marehemu

 
Ama katika kutimiza Sala, Saumu na Hijja unaweza kuwalipa watu wakakutimizia iwapo wewe mwenyewe huwezi kufanya hivyo. Mfano iwapo marehemu alikuwa akidaiwa Sala au Saumu za miaka 2, na wewe huwezi kutimiza hivyo, unawalipa watu, utaratibu wake pia upo katika Shariah, wakakutimizia haki hiyo.
 
Natumai kwa mafupi haya yatakuwa yamekupatia mwanga na kwa ajili ya kutaka kujua zaidi naomba urejee vitabu vya Fiq-h katika sura inayozungumzia maiti. Au ukawauliza Mashekhe na Maulamaa waliokaribu nawe.
 
Wabillahi Tawfiq,
 
Amiraly M.H.Datoo 3/5/2003
Bukoba ( datooam@hotmail.com )